Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Mganga njaa tu huna lolote! Chadema inajimaliza yenyewe haiwezekani chama kiwe chini ya viongozi ambao wazinifu; waongo na wezi ambao wanajali maslahi yao zaidi kuliko ya chama halafu eti utegemee chama kiwe imara!

Vipi we kah.aba wamezini na wewe mpaka uwaite wazinifu?
 
Kumbe Wanaijua Nyota ya Dr. Slaa ndio maana hawalali kupandikiza Masalai, tunguli nk?

Nawaakikishia, Mwigulu Nchemba atakufa
yeye Akifanya URODA kabla ya CHADEMA. Chadema ni movement ya Watanzania millioni 44. Kwa hiyo ili CHADEMA kife, ni bora awaue watanzania hao wanaoishabikia CHADEMA. Mbona akili zao zinawaza CHADEMA tu na sio mke wao wa Ndoa CUF?

Muke Ya Muzungu

Mhhhh Nani kaudanganya CHADEMA inashabikiwa na watanzania wote nyambaff!!!!! mbona bungeni muko less than sixty MP's
 
550145_329787750473081_384773229_n.jpg
384559_274967445899615_1525162735_n.jpg

NI WAZI SASA HISTORIA YA KUANGUKA VYAMA VYENYE NGUVU SASA INATIMIA KWA KASI.
Historia kawaida yake huwa inajirudia mfano mwaka 1984 mh jumbe alidai serikali tatu akafukuzwa urais sasa 2014 jambo lilelile limejirudia
hata mwalimu alidai katika hotuba yake maarufu juu ya Ubaguzi,UKANDA na udini akisema ni vitu hatari ni historia imeonyesha yoyote alievikumbatia alipata matatizo makubwa.
sasa chadema hivi sasa wapo njia panda
NGUVU WALIZOKUANAZ0 MWAKA 2010 zimepotea ghafla mfano ni uchaguzi uliopita ambapo chadema walitumia hadi helikopta wakapata kata 3 vilevile katika kura za ubunge kupata chini ya asilimia tano ya kura zote zilizopigwa kule kalenga na katika jimbo la kikwete.
note
hakika ni bora mjinga kuliko mpumbavu kwan mjinga hujifunza lakini mpumbavu hajifunzi kutokana na makosa bali hujaa kiburi na kujiona.
HUENDA ACT IKACHUKUA ICHI IKALETA UKOMBOZI KWA TAIFA
10339565_1394511934167453_5688644330524812460_n.jpg
 
chadema inakufa kwa kasi sana! Ni zaidi ya vyama vyote vya siasa vilivyowahi kufa tanzania. Tatizo mbumbumbu wengi mle
 
Binafsi sielewi kwa nini CHAMA kilicho madarakani KIPAMBANE na upinzani kwa kutumia mbinu ZA KUUA upinzani badala ya kunadi SERA za kutafuta uhalali wa kubakia madarakani. KUUA UPINZANI katika demokrasia ya ushindani wa vyama vingi kuna nafasi gani katika democracy? Au tuachane na democracy na kutumia CCM-cracy?
Mnyukano wa ki-sera katika harakati za KUENDELEZA TAIFA ni kipimo cha ukomavu kisiasa. Tofauti za SERA sio uadui. MAENDELEO ya TAIFA letu ni jukumu letu wote hata kama tunatofautiana kimtazamo. Ridhaa ya nani aongoze nchi inatolewa na WANANCHI chini ya usimamizi wa KATIBA BORA na siyo wewe MWIGULU au chama chako na wala mtu mwingine, kichaa au asiye kichaa hata kama ni wa CHAMA cha UPINZANI. Tafuta nukuu ya Prof. Kabudi - TANZANIA ni kubwa kuliko chama chochote na watu wake!
Ndio maana inasikitisha mno kila siku kusikia maneno ya wehu!
 
Hawa magamba vigeu geu walisema chadema itakufa last year, then after last year wakasema kitakufa this year now baada ya njama zao kuvuja wanasema next year. ..sasa hivi mwigulu mchemba anasema after 2015
Kila mtu anabwatuka...tu
 
Nashangaa hawa viongozi wenu,yaani kiongozi wa serikali unakaa kwenye ofisi ya umma anaaza kuponda ohoo..chadema hawa,mara watayeyuka 2015!why not TLP,UDP?.Mnaongea hayo kwasb hicho chama kinawachima usingizi
:flame:
 
Chama ambacho tayari hakipo mioyoni mwa raia wakawaida ni CCM!Kiukweli kinaendelea kuwepo kwa sababu ya nguvu ya dola.
 
Wana jamvi ccm wamerogwa na makada wao mwiguru na wasira kwa kuwaaminisha viongozi wao na wana ccm kwa kauli zao kuwa chadema itakufa kabla ya 2015,sasa wakati wakibwete kwa kauli zile tamu na matumaini kwao huku walio zitoa wakipiga pesa za maana toka ccm wamepata hofu kubwa baada ya kugundua chadema haifi inakua kwa haraka kwa kuchomoza chaguzi za wilaya kila pembe ya tanzania,wakati kabla ya chaguzi za wilaya chadema walianza misingi,matawi na kata,sasa wana hamia mikoa baada ya majimbo mwisho kabisa taifa na kwahakika mawakala wao wote mamruki wamefyekwa kona zote pia wameingia vijana wapya wasomi sasa ccm wana haha kuleta propaganda,mimi nawaambia wamechelewa wasipambane na chadema makada wao walio tabiri chadema yafa waliwahadaa lengo lao ni kupiga pesa toka ccm lakini pia wassira bado anadamu ya upinzani so hawezi kuangamiza upinzani kwakua ccm walimtisa sana wakati ule so atakua anaimaliza ccm kimya kimya;karibuni mjadalani
 
nchemba.jpg

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba

CHAMA Cha Mapinduzi kimekitabiria kifo Chadema baada ya uchaguzi wa 2015 kikieleza kuwa CCM ikishinda, chama hicho kitakuwa hakina nguvu tena kwa kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa atakuwa amechoka.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kinapoteza umaarufu kadri siku zinavyokwenda hasa kutokana na siasa zake za uchochezi na mwaka 2015 ndio itakuwa mwisho wa chama hicho.

Alisema kitakufa na kitasahaulika kabisa, akisema sasa hivi vijana wameshaanza kuwakimbia, na kwamba anaamini pia baada ya 2015 hakuna diwani ambaye atagombea kupitia chama hicho.

Alisema pia ni mwaka ambao Katibu wa Chadema Willibrod Slaa amestaafu kwa kuwa alishatangaza asiposhinda atastaafu na Chadema haiwezi kushinda hivyo mwisho wa Dk Slaa ndio utakuwa umefika kwa kuwa nyota yake haitang'aa tena.

"Nguvu ya Dk Slaa aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita sio aliyonayo sasa na mpaka mwaka 2015 atakuwa ameisha kabisa." alisisitiza.

Pia Mwigulu aliyataka makundi yaliyojichomoza ndani ya CCM ikiwa ni harakati za kuwania urais mwaka 2015 kuheshimu ilani ya chama hicho kwa kuitekeleza na kuisimamia kwa kutoleta vurugu ndani ya chama wala kujenga chuki kwa wale ambao hawawaungi mkono.

|"CCM ina utaratibu wake wa kupata mgombea na hatumzuii mtu kugombea, sisi kama kamati ya utendaji tunatekeleza maagizo aliyotoa mwenyekiti tutayasimamia kwa nguvu zote anayetaka kugombea ahakikishe havurugi chama na asitengeneze chuki kwa ambao hawamuungi mkono."

Wakati huohuo Naibu Katibu huyo wa CCM na Mbunge wa Iramba Mashariki aliwataka wakazi wa Mtwara kuachana na propaganda zinazoenezwa na wapinzani kuhusu rasilimali ya gesi na badala yake wafanye kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

"Rasilimali iliyopo ni ya taifa na watafaidika, hakuna rasilimali ya wilaya fulani, bomba la gesi ni lazima lijengwe tutawaelimisha wakazi wa Mtwara, kwani hata Ziwa Victoria bomba lilijengwa kwenda Shinyanga badala ya Kwimba, kwa nini basi halikujengwa kwenda Kwimba wakati pale ni karibu zaidi.

"Utajiri unategemea na jitihada, wasitegemee kwa vile tuna rasilimali ya gesi basi wakae wategemee watapata utajiri bila ya kufanya kazi haiwezekani, wasisubiri kupewa vya bure, ni kama mikoa yenye madini halafu wakazi wa pale wategemee Serikali itawapa vocha za kuweka kwenye simu kwa vile madini yao kwao, haiwezekani ni lazima wafanye kazi.

Source: Mwananchi

My take:

- Attention ya CCM ni Dr. Slaa.
Ni sawa kutoa maoni yako ndugu miguu chemba!! Tunakuonya tu usije kuwa unapanga kutumia mabomu tena kama ulivyowatahadharisha wanaArusha kuwa wakihudhuria mikutano ya CDM watakufa. Kweli bomu likaua watu watatu!! Wakati huu tutachukua hatua kwa vile policcm wako nawe!! usiulize hatua gani!
 
cdm inakufa kwa kudhani katiba ndio inawazui kuingia ikulu. wameacha agenda ya kupigania utawala bora iliyokua inawapa chati na kudhani serikali tatu bila kujali adhari ya kuvunjika muungano itawapa chati.
 
nchemba.jpg

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba

CHAMA Cha Mapinduzi kimekitabiria kifo Chadema baada ya uchaguzi wa 2015 kikieleza kuwa CCM ikishinda, chama hicho kitakuwa hakina nguvu tena kwa kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa atakuwa amechoka.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kinapoteza umaarufu kadri siku zinavyokwenda hasa kutokana na siasa zake za uchochezi na mwaka 2015 ndio itakuwa mwisho wa chama hicho.

......................
............

"Nguvu ya Dk Slaa aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita sio aliyonayo sasa na mpaka mwaka 2015 atakuwa ameisha kabisa." alisisitiza.

......................
.........

Wakati huohuo Naibu Katibu huyo wa CCM na Mbunge wa Iramba Mashariki aliwataka wakazi wa Mtwara kuachana na propaganda zinazoenezwa na wapinzani kuhusu rasilimali ya gesi na badala yake wafanye kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

"Rasilimali iliyopo ni ya taifa na watafaidika, hakuna rasilimali ya wilaya fulani, bomba la gesi ni lazima lijengwe tutawaelimisha wakazi wa Mtwara, kwani hata Ziwa Victoria bomba lilijengwa kwenda Shinyanga badala ya Kwimba, kwa nini basi halikujengwa kwenda Kwimba wakati pale ni karibu zaidi.

"Utajiri unategemea na jitihada, wasitegemee kwa vile tuna rasilimali ya gesi basi wakae wategemee watapata utajiri bila ya kufanya kazi haiwezekani, wasisubiri kupewa vya bure, ni kama mikoa yenye madini halafu wakazi wa pale wategemee Serikali itawapa vocha za kuweka kwenye simu kwa vile madini yao kwao, haiwezekani ni lazima wafanye kazi.

Source: Mwananchi

My take:

- Attention ya CCM ni Dr. Slaa.

Hayo ndiyo maoni ya viongozi wetu vijana wasomi! Je, ni kweli kuwa tunaweza kuingia katika ushindani wa kimataifa iwapo viongozi wetu twatumainiao wanafikiria upuuzi kama huo? Obvious ni kuwa CHADEMA ikifa, viongozi wengi CCM watakuwa hawana la kufanya tena kwa vile itakuwa "mission completed."
 
Back
Top Bottom