Leo jumapili kulikua na mkutano wa ccm kata ya Themi Arusha tawi la Fire.
Mkutano huu ulipangwa kufanyika jana ila ulihairishwa kwasababu wakazi wa maeneo husika waligoma kujitokeza na hapo ndipo ccm walipoamua kukusanya kina mama kutoka kata ya daraja mbili na maeneo mengine ambayo sio ya wapiga kura wa kata ya Themi na kuamua kufanya mkutano huo leo.
Mkutano huu uligubikwa na vituko vya aina yake ambapo wahudhuriaji walikua wachache sana na kila mmoja aliambulia elfu 2.
Kuna mpita njia alionyesha alama ya vidole viwili aliambulia kipigo kikali kutoka kwa makada wa ccm ambao ni majambazi maarufu wakiongozwa na Jumanne Mjusi, Mojaa, kabelwa, Ali Maumba, Iddy Mkuluu, Rama Mkuluu n.k.(Wote hawa ni wakazi wa daraja mbili na sio wapiga kura wa Themi)
Kituko kilicho waacha hoi wakazi wa Fire ni pale baada ya mkutano Mwigulu alipokua akipita na gari yenye bendera ya CCM kulikua na kundi kubwa la kina mama na vijana wakiwa wamesimama chini ya mti pembeni ya barabara na walipomuona Mwigulu walimuonyesha alama ya vidole viwili na kumzomea kwa kumuita muuaji.
Mwigulu alionyesha hali ya mshtuko na kufunga kioo chake na dereva alizidisha speed kali sana kumnusuru Nchemba na aibu hii ya machalii.
My Take:
Kuitetea CCM inahitaji uwe na akili ya maiti.
NB: CCM arusha mnachezea pesa zenu bure.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums