Mwigulu Nchemba azomewa Themi-Arusha

Mwigulu Nchemba azomewa Themi-Arusha

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
62,188
Reaction score
128,284
Leo jumapili kulikua na mkutano wa ccm kata ya Themi Arusha tawi la Fire.

Mkutano huu ulipangwa kufanyika jana ila ulihairishwa kwasababu wakazi wa maeneo husika waligoma kujitokeza na hapo ndipo ccm walipoamua kukusanya kina mama kutoka kata ya daraja mbili na maeneo mengine ambayo sio ya wapiga kura wa kata ya Themi na kuamua kufanya mkutano huo leo.

Mkutano huu uligubikwa na vituko vya aina yake ambapo wahudhuriaji walikua wachache sana na kila mmoja aliambulia elfu 2.
Kuna mpita njia alionyesha alama ya vidole viwili aliambulia kipigo kikali kutoka kwa makada wa ccm ambao ni majambazi maarufu wakiongozwa na Jumanne Mjusi, Mojaa, kabelwa, Ali Maumba, Iddy Mkuluu, Rama Mkuluu n.k.(Wote hawa ni wakazi wa daraja mbili na sio wapiga kura wa Themi)

Kituko kilicho waacha hoi wakazi wa Fire ni pale baada ya mkutano Mwigulu alipokua akipita na gari yenye bendera ya CCM kulikua na kundi kubwa la kina mama na vijana wakiwa wamesimama chini ya mti pembeni ya barabara na walipomuona Mwigulu walimuonyesha alama ya vidole viwili na kumzomea kwa kumuita muuaji.
Mwigulu alionyesha hali ya mshtuko na kufunga kioo chake na dereva alizidisha speed kali sana kumnusuru Nchemba na aibu hii ya machalii.

My Take:
Kuitetea CCM inahitaji uwe na akili ya maiti.


NB: CCM arusha mnachezea pesa zenu bure.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Muda si mrefu Mwigulu ataibukia jf kusema 'sikuzomewa'.

Ama kweli la kuvunda halina ubani...

Mpaka kieleweke!
 
Sijui Lamecky anatafuta nini,usimba wa Yuda chamani? anataka aonekane amepiga kazi na ameirudisha Chuga ccm? anapaka rangi upepo,cjui magamba wamemlipa au wamemuahidi nini? sifa za kijinga kabisa
 
jana nilisema mwigulu ni mwongo. hapa arusha hawezi kuachwa kuzomewa. mbweha kweli huyu
 
kazi ipo...ila arusha watu si wanafki watakipata wanachokitafuta siku ya uchaguzi si aliona arumeru
 
hiyo ndiyo Arusha naamini bado hajasahau yale ya arumeru.
cc Mtela Mwampamba
 
Kadanganywa na kale kakofia ka kichina akidhani wanaarusha watabadirika.
 
Kuipenda CCM ni kukubali kuwa upstairs kwako hakuna usalama!
 
Atakwenda kuchukuwa Kikosi chake cha Mbeya kwenda kuongeza Nguvu
 
Hahaaaaaa.... Afu mkutano wakaenda kuufanyia kwenye shamba la mahindi ili picha ikichukuliwa waonekane wengi hahaaaaaaa!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hahaha safi sana! Naomba ajw kukanusha tumzomee tena hapa jf kama jana.maana yeye anakanusha hata visivyo faa kukanusha.atasema atatoa ushahidi mbinguni kuwa hajazomewa..asizomewe yeye amekuwa nani? Kikwete mbona huzomewa sembuse yeye ugh!
 
Back
Top Bottom