Mwigulu atoa maagizo mawili Uwanja wa AFCON Arusha

Mwigulu atoa maagizo mawili Uwanja wa AFCON Arusha

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,185
Reaction score
17,706
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba leo, Ijumaa, Aprili 17, 2026, ametoa maagizo mawili kwa wanaosimamia mradi wa ujenzi wa Uwanja wa soka wa Arusha utakaotumika kwa Fainali za AFCON 2027.

1776430230100.png

Maagizo hayo ni uharakishwaji wa mradi huo pamoja na matumizi stahiki ya fedha za ujenzi wa uwanja huo.

Amesema uwanja huo unatakiwa kukamilika mapema ili kuendana na muda wa maandalizi waliopewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

“Kaguzi zitakuja mapema zaidi ya hapa. Fanyeni kazi usiku na mchana. Tusiweke dosari ambazo hazihusiani na maandalizi ya viwanja. Ongezeni vitendea kazi, ongezeni nguvu kazi ili tutekeleze mapema huo muda ambao tumeuweka.

“La pili tuendelee kuzingatia thamani na viwango vya fedha. Tutimize mahitaji na matakwa ya waendesha shughuli wa AFCON lakini lazima tuwape thamani ya viwango Watanzania ambao ndio watoa fedha ya ujenzi,” amesema Mwigulu.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Uwanja huo jijini Arusha.
 
Back
Top Bottom