Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 962
- 1,909
Akisoma Bajeti Kuu ya Mwaka wa Fedha 2026/27 Bungeni, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar amesema Katika Bajeti ya 2026/27, Serikali imefanya matumizi mahsusi kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi na huduma mbalimbali ikiwemo:
(i) Shilingi trilioni 2.86 kwa ujenzi wa barabara, madaraja, na viwanja vya ndege.
(ii) Shilingi trilioni 1.59 kwa miradi ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme ikiwemo mradi wa Gridi ya Taifa. Serikali imekamilisha na kuzindua mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere lenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 na hivyo kusababisha uwezo wetu wa kuzalisha umeme kufikia megawati 4,522.54. Aidha, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Serikali imetumia shilingi bilioni 521.3 na hivyo kufanya jumla ya vitongoji vilivyofikiwa na umeme kuwa 39,003; 11
(iii) Shilingi trilioni 1.58 kwa uimarishaji wa vyuo vya VETA, kukuza ujuzi kwa vijana na ujenzi wa miundombinu ya elimu pamoja na mikopo ya wanafunzi 284,487 wa elimu ya juu, na ugharamiaji wa elimumsingi bila ada iliyonufaisha wanafunzi 16,838,013;
(iv) Shilingi trilioni 1.27 kwa ujenzi na ukarabati wa reli ikiwemo shilingi trilioni 1.12 kwa ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa (SGR), katika kipindi hiki ujenzi wa reli ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma ulikamilika na huduma za usafiri na usafirishaji zilizinduliwa rasmi;
(v) Shilingi bilioni 870.4 kwa utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini ikiwemo uendelezaji wa mradi wa Gridi ya Taifa ya Maji na ujenzi wa mabwawa, likiwemo la Kidunda litakalonufaisha mikoa mitatu ya Morogoro, Pwani na Dar-es-Salaam;
(vi) Shilingi bilioni 681.7 kwa ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya afya;
(vii) Shilingi bilioni 667.3 kwa ulipaji wa 12 madeni yaliyohakikiwa ya wazabuni na watoa huduma, wakandarasi na washauri elekezi hususan wa ndani ya nchi;
Soma Pia: Prof. Shemdoe: Mkandarasi anayejenga barabara kuelekea Uwanja wa AFCON 2027 Arusha hataongezewa muda
(viii) Shilingi bilioni 302.0 kwa ujenzi wa miundombinu na viwanja vya michezo na ushiriki kwa ajili ya mashindano ya AFCON 2027.