Mwigulu ataka taratibu za uhamiaji zirahisishwe AFCON 2027

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani na Tamisemi kukamilisha maandalizi ya mipakani kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2027 (AFCON 2027) zitakazoandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza Namanga, Arusha Februari 23, 2026, amesema kutokana na muingiliano mkubwa wa watu kuvuka mipaka kufuatilia michezo, ni lazima kuwe na maandalizi madhubuti ili kuepusha changamoto.

Amesisitiza kuwa Tanzania kwa sasa ina mpira mkubwa Afrika Mashariki baada ya kufika hatua ya 16 bora, hivyo mashabiki wengi wanatarajiwa kusafiri kuvuka mipaka kushuhudia mechi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amesema ushirikiano wa Tanzania na Kenya ni mzuri na mipaka iko salama.
 
Mimi nirahisishiwe niende Burundi
 
Back
Top Bottom