Mwigulu ana Hali mbaya Iramba

Mwigulu ana Hali mbaya Iramba

Hapa ndipo ninapo elewa kwa nini katika ule muswada wa sheria kwa vyama siasa ulisema ," mwanasiasa atakaye hama chama chake haruhusuwi kugombea nafasi ya ubunge mpaka atimize mwaka mmoja ndani ya chama".

Hivyo Mwigulu ikitokea amepigwa chini kugombea katika hilo jimbo hatokuwa na nafasi ya kurudi tena Bungeni mpaka uchaguzi unaofuata iwapo tu atakubaliwa na chama chake.

This is not fair , Msajili ndio Mwenyekiti wa vyama vyote vya siasa while atakuwa remoted from Magogoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonekana kuna maelekezo maalum ya kumsadia Kitila Mkumbo kuwa Mbunge la Iramba Magharibi jimbo linaloshikiliwa hivi sasa na Mwigulu Nchemba.

Kwenye mizunguko yangu jimboni humo, jimbo mojawapo kati ya majimbo machache yaliyobakia kutumia fedha za vijiji kufanyia siasa za CCM, Mwigulu amebaki kupiganiwa na watu wachache dhidi ya kundi kubwa linaloonekana linapokea maelekezo toka ngazi za juu ndani ya chama hicho.

Kitila Mkumbo inaonekana anazidi kukaza kitanzi kitakachomuua kisiasa Mwigulu Nchemba kwenye jimbo analoliongoza hivi sasa
Anavuna alichopanda
Acha arudi mtaani tuumie pamoja
 
Nimetembea maeneo mengi sana lakini Iramba wanajitahidi sana kwenye kujiletea maendeleo. Kwa mfano kwenye ujenzi wa nyumba na upangaji wa mji wa Kiomboi na baadhi ya vijiji. Ingawa kuna tatizo kubwa sana la maji na madaraja kwenye yale maeneo yenye mito ya msimu. Ila Mkalama wana Hali mbaya kwa kweli.

Tatizo la Iramba bado fedha za vijiji zinatumiwa kwa kazi za kisiasa za CCM.
Ndio maana nasema historia na geography ya miaka Ile kuhusu Iramba ni batili. Kuna wahuni tu walikuwa na nia ovu wakaandika uongo. Hivi sasa hata chakula Kuna mikoa inahemea toka Iramba. Ukienda kwenye makazi yameonekana ni Bora mpaka ndani vijijini wakati Kuna wilaya nchi hii hata msosi bado hawapati wa kutosheleza familia zao na hata makazi bado duni mno sema Tu wako vizuri kwenye media hasa wanaokaa mijini
Issue kubwa hapa ni matumizi mabaya ya pesa za maendeleo kuwekwa kwenye mambo ya chama ccm
 
Issue kubwa hapa ni matumizi mabaya ya pesa za maendeleo kuwekwa kwenye mambo ya chama ccm
Ni kweli kabisa. CCM inawatesa sana watendaji wa vijiji wa Iramba kwa kulazimisha fedha za vijiji kugharamia shughuli za chama chao kama vile safari za kutoka kwenye kata kwenda Kiomboi ama viongozi wa wilaya wanapotembelea vijijini fedha za vijiji hutumiwa kuwakirimu.
 
Binafsi bado sijashawishika kama prof. Kitila atafit katika ubunge wa Iramba. Sijaona bidii yake ya kutaka kuona wananchi wa iramba wanajikwamua angalau Kwa issue hata ya maji tu.
Naona itakuwa bonge ya setback kama atapitishwa.
 
Kwa issue hata ya maji tu.
Nadhani mbali na maji ya Ardhini lakini maji yanayopita kama kule Kidaru yakitegwa na kujengewa bwawa yanaweza kusaidia. Pale Iguguno kuna kila dalili kwamba pakichimbwa kisima kinaweza kupeleka maji sehemu kubwa sana ya Iramba.

Maji ndiyo ingetakiwa iwe ajenda kwa wanaotaka Udiwani na Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
 
Nadhani mbali na maji ya Ardhini lakini maji yanayopita kama kule Kidaru yakitegwa na kujengewa bwawa yanaweza kusaidia. Pale Iguguno kuna kila dalili kwamba pakichimbwa kisima kinawezekana kupeleka maji sehemu kubwa sana ya Iramba.

Maji ndiyo ingetakiwa iwe ajenda kwa wanaotaka Udiwani na Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
Sasa MTU kama kitila anataka ubunge lakini sijawahi hata kusikia akizungumza issue za maendeleo Iramba.
Jesca kishoa naye kapata ubunge wa viti maalum sijui hakufurahishwa?? Kapotea forever. Watu kama hawa mi napata shida kuwaamini kama watakuwa wa mswada Kwa Iramba.
Kila MTU ana kile kinachomuumiza, kinachomuumiza asilale kwa kuwa bibi zake hawama maji na kinamfanya hata kile kidogo alichonacho awaze kwenda kutoa msaada hata kama sio mbunge au hata ainfluence mabadiliko. Hawa wamekimbia na hawaendi hata jimboni. Mpaka wapate ubunge??
Mwigulu ana kitu kinamkereketa moyoni kuhusu Iramba na najitahidi sana. Bado namuona MTU potential Kwa Iramba kuliko hao wasaka vyeo wapya.
 
Kama unafanya ulinganisho kati ya Mwigulu na hawa wengine upo sahihi.
Ukiangalia jesca kwa mfano na hata kitila, wamekuwa kwenye nyendo za kutaka ubunge lakini ni miaka mitatu sasa hata kupeleka vikitabu tu vikasaidia vijana katika shule za kata au hata bundle ya bati katika ujenzi wa shule za kata hawajawahi kuonekana.
Mfano pale kisana wanajenga mabweni japo hata madarasa bado hayajatimia, lakini hakuna aliyeona angalau ashiriki Kwa namna yeyote Ile. Ni kama vile ni kazi ya mwigulu so mwachiieni japo hapa hata mwigulu ameshindwa kuwaleta pamoja wadau Kwa nia ya kusukuma Kasi ya maendeleo
 
Mfano pale kisana wanajenga mabweni japo hata madarasa bado hayajatimia, lakini hakuna aliyeona angalau ashiriki Kwa namna yeyote Ile.
Lakini Kisana wana matatizo mawili makubwa.Kwanza wana viongozi wasio na mpangilio kwenye kufanya kazi zao. Wanapenda kuanzisha miradi mipya kabla ya zamani haijakamilika. Mimi mpita njia waliniambia nichangie 5000 kwa ajili ya madawati, nilipowahoji wao wanahitaji kiasi gani kukamilisha madawati wanayohitaji wakawa hawana jibu.

La pili maisha ya pale mpangilio wake siuelewi kabisa. Yaani inakuwaje mtu mmoja anawafumania wake zake na watu tofautitofauti na kulipwa fedha? Yaani inakuwaje watu wanafumaniani zaidi ya mara moja halafu wanaendelea kuishi pamoja kama si mradi wa kupora fedha za watu wengine?

Lakini pia Kisana wana Imani sana za kishirikana. Huwezi kuamini jinsi wanavyolima na kupata mazao ya kutosha lakini ni miongoni mwa maeneo yalilyo nyuma kimaendeleo. Waache mambo yao ya kishirikina la sivyo maeneo mapya yatawaacha mbali sana!!

Zaidi ya hapo ni kweli watu wengine hawaonekani kuchangia maendeleo ya Iramba kwa ujumla wake!!
 
Unabishana na mtu anayetumia account fake?
Alitaka kuonesha kwamba nilichoandika nimetunga, ningemkalia kimya kuna watu wangehisi labda kweli nimetunga. Lakini MAPUMA MIYOGA anajua ninachoongea kwa kuwa kweli yeye ni wa Iramba Magharibi siyo kama DrLove69 aliyeleta ushabiki wa kisiasa.
 
Alitaka kuonesha kwamba nilichoandika nimetunga, ningemkalia kimya kuna watu wangehisi labda kweli nimetunga. Lakini MAPUMA MIYOGA anajua ninachoongea kwa kuwa kweli yeye ni wa Iramba Magharibi siyo kama DrLove69 aliyeleta ushabiki wa kisiasa.
Mkiambiwa ukweli ili mauche tabia zenu za kupotosha Umma inakuwa "Ushabiki wa Kisiasa"!? Ama kweli makamanda mmeishiwa hoja.
 
Fuatilia mjadala uone ni kwa nini mwenzio alikimbia!
Ni nani amekimbia!? Nina majukumu ya kutekeleza ili watoto wangu wapate Elimu na malezi bora kamanda. Huwa sishindi JF 24/7.
Mwisho wa Uongo na Uzandiki ni AIBU kamanda. 2020 sio mbali.
 
Back
Top Bottom