Kwa raia mwema na wa kawaida haijalishi ni nani anaongoza nchi, iwe cdm, ccm, cuf nccr nk bali ni kuona watu wenye uwezo wa kukabiliana na matatizo yanayoikabili nchi kama usalama wa mipaka yetu na mahusiano mema na majirani zetu kabla ya kwenda kutafuta majirani wa mbali kama Ulaya, Amerika, China, Uarabuni nk.
Lakini pale unapogundua kuwa tuna viongozi wa aina hii na mtu kama huyu anashika miongoni mwa nafasi za juu kabisa za chama tawala ndio unapata jibu ni kwa nini tuna matatizo yote tuliyo nayo huku wasiwasi wa hatima ya taifa letu ukiongezeka. Kauli/swali kama hii ni matusi makubwa kwa Bcom na MBA holders hasa kutoka chuo kinachoheshimika kama UDSM.