Breki sina
Member
- Jun 3, 2013
- 96
- 32
Naibu katibu mkuu wa CCM bara Mwingulu Nchemba akiuliza swali la nyongeza kwa waziri ofisi ya rais utawala bora Mkuchika amesema ni kwa nini viongozi ambao wamesababisha vifo vya watu huko Singida, Arusha akiwataja viongozi wakuu wa CHADEMA; Mheshimiwa Mbowe na Slaa kuwa wafungwe ndio wamesababisha vifo hivyo.
Kama kweli huyu ndio kiongozi wa CCM basi wamekosea kumpatia hiyo nafasi kubwa na adimu ni hivi karibuni tu mahakama ya mkoa wa Singida imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa Chadema mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar Kitila Mkumbo na Mwita Waitara kuwa hawana kesi ya kujibu kutokana na huyo nchemba kushindwa kufika mahakamani.
Na pia huku Arusha tume ya haki za binadamu na utawala bora wamekwisha toa taarifa yao na kuituhumu serikali kuwa ilitumia nguvu kubwa na polisi walituhumiwa kuua.