Mwigulu achafua hewa bungeni na kuzua miguno

Mwigulu achafua hewa bungeni na kuzua miguno

Status
Not open for further replies.

Breki sina

Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
96
Reaction score
32
Naibu katibu mkuu wa CCM bara Mwingulu Nchemba akiuliza swali la nyongeza kwa waziri ofisi ya rais utawala bora Mkuchika amesema ni kwa nini viongozi ambao wamesababisha vifo vya watu huko Singida, Arusha akiwataja viongozi wakuu wa CHADEMA; Mheshimiwa Mbowe na Slaa kuwa wafungwe ndio wamesababisha vifo hivyo.

Kama kweli huyu ndio kiongozi wa CCM basi wamekosea kumpatia hiyo nafasi kubwa na adimu ni hivi karibuni tu mahakama ya mkoa wa Singida imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa Chadema mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar Kitila Mkumbo na Mwita Waitara kuwa hawana kesi ya kujibu kutokana na huyo nchemba kushindwa kufika mahakamani.

Na pia huku Arusha tume ya haki za binadamu na utawala bora wamekwisha toa taarifa yao na kuituhumu serikali kuwa ilitumia nguvu kubwa na polisi walituhumiwa kuua.
 
Kama amesema hivyo basi inawezekana anaumwa ugonjwa ambao haujajulikana. Nilikuwa Ar last week na wengi wanakuambia Mwigulu ni muuaji na baada ya bomu kurushwa alitaka kukimbilia uwanja wa ndege akashindwa kwani walimtafuta sana lakini hatimaye alipanda kama nakumbuka bus. Aache hizo aongee mambo mengine.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
KIMENUKA BUNGENI,MH.MWIGULU NCHEMBA AWALIPUA MBOWE NA DR.SLAA KWA MAUAJI YA NDAGO,IRINGA,ARUSHA NA MOROGORO
9k=

ANAPIGILIA MSUMARI KWA KUSEMA "JELA NDIO WANAKOSTAHILI MBOWE NA DR.SLAA "
MBOWE AINAINAMISHA KICHWA CHINI BAADA YA MWIGULU KUMLIPUA,
chadema-mnyika1.jpg
Ni kiongozi jasiri,ni kiongozi mzalendo,nikijana shupavu,amejitolea kuipigania Tanzania ya kweli,amejitolea kupambana na wahujumu wa nchi popote pale Tanzania,Ni Mh.Mwigulu lameck Nchemba leo tena anafanya kile CHADEMA wapata maumivu yasiyonakifani,Mwigulu nchemba amewalipua kisawa sawa Vioongozi wa CHADEMA wa juu wakiongozwa na Freeman aikael Mbowe na Dr.slaa kuhusika na umwagaji damu za Watanzania wasio na hatia.Ni siku leo asubuhi kwenye kipindi cha Maswali na majibu,Mh.Mwigulu Nchemba akitoa swali la nyongeza anasema "Ndani ya miaka miwili CHADEMA wakiongozwa na Freeman Mbowe na Dr.slaa wamesababisha vifo Arusha,Ndago,Morogopro na Iringa.Kwa mauaji haya yaliyotokana na ukatili wao na kutojali maisha ya watu kwa viongozi hawa wa CHADEMA.Mbowe na Slaa wanastahili kuwa JELA na walistahili kuwa jela siku nyingi".Anasema Mbunge wa Iramba Magharibi.Baada ya kauli hiyo Ukumbi wa bunge unalindima kwa makofi mazito.Huku upande wa CHADEMA kila mmoja akiishia kukunja sura.
images


Safi sana Mwigulu Nchemba,mbona watakukoma sana hawa CHADEMA na mwaka 2015 ndio kabisa kwisha habari yao.
images

 

Attachments

  • Green Guard 3.JPG
    Green Guard 3.JPG
    164.8 KB · Views: 1,122
''Ni kiongozi jasiri,ni kiongozi mzalendo,nikijana shupavu,amejitolea kuipigania Tanzania ya kweli,amejitolea kupambana na wahujumu wa nchi popote pale Tanzania,Ni Mh.Mwigulu lameck Nchemba!

Akili uliyonayo inafanana na Avatar yako ikikuonyesha unakula Kucha!
 
Makada watano CHADEMA kortini.

*Ni watuhumiwa wa tindikali Igunga 2011
*Waachiwa na kukamatwa, wapelekwa Tabora

MAKADA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Igunga, wakituhumiwa kummwagia tindikali Musa Tesha mwaka 2002.

Watuhumiwa hao, walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora jana, ambapo upande wa mashitaka uliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili mahakamani hapo, hivyo kuachiwa huru lakini walikamatwa tena hapo hapo na kurudishwa korokoroni.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ajali Milanzi, mwendesha mashitaka wa polisi, Cosmas Mboya aliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili watuhumiwa hao kwa kutumia kifungu cha 98 (A) cha Sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1985, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kuhusu mwendesha mashitaka kufanya hivyo.

Baada ya kuondoa shitaka hilo, Hakimu Milanzi alikubaliana na upande wa mashitaka na kusema kuwa, washitakiwa wako huru.

Baada ya kufutiwa shitaka hilo, watuhumiwa walianza kutoka nje ya mahakama lakini ghafla walizingirwa na askari zaidi ya 40 waliokuwa wamesheheni silaha aina ya mabomu, bunduki na pingu ambao waliwakamata tena.

Walifungwa pingu, kisha wakapakiwa ndani ya magari mawili ya polisi ambayo yaliondoka eneo la mahakama kwa kasi huku yakiwaacha wananchi waliokuwa wamefurika mahakamani hapo katika mshangao.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga (OCD), Abeid Maige aliwaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa wamepelekwa Tabora kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka mengine mapya. Hata hivyo hakuyataja.

Washitakiwa hao ni Evodius Justian (30) mkazi wa Bukoba, Osca Kaijage (36) mkazi wa Ndala mkoani Shinyanga, Rajabu Daniel (24) mkazi wa Singida na Seif Magesa (37) mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza.

Wote walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga Aprili 12 mwaka huu, kwa kosa la kummwagia tindikali Mussa Tesha (26) mkazi wa Igunga Mjini, wakati wa kampeni za Uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba mwaka 2011.

Chanzo: Gazeti la Mtanzania
 
Safi sana Mwigulu. . Hizo ndizo siasa za CHADEMA. . Wao wanauwa wananchi kwania ya kutafuta huruma kwa wananchi. . .

Asante CCM kwa kumleta Mwigulu kuwa mwiba kwa CHADEMA

Wananchi tumeshawajua wauwaji nyinyi
 
Nchi imebakia kuropoka tuu
wananchi wanaangamia ccm imekwapua hela zote ili kuwazibiti CHADEMA
Hatuna hospital hata moja ya maana ccm chama cha majangili wauaji
CCM imebaki kuuza madawa ya kulevya kila ukienda airport unakamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya
ccm imebakia kupayuka tuu hatuoni chochote inachokifanya wamebaki kukwapua hela za walipa kodi kununulia tindikali na mabomu kutoka China we are tired
 
Dawa ya CHADEMA ni kuwaambia ukweli kama afanyavyo Mwigulu Lameck Madelu Nchemba. Big Up sana MWIGULU
 
Makada watano CHADEMA kortini.

MAKADA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Igunga, wakituhumiwa kummwagia tindikali Musa Tesha mwaka 2002.

Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Ulikuwa umezaliwa kweli?
 
Akili ndogo kutawala akili kubwa.......
 
mwigulu -------- hana uwezo wakufikria, mm nina wasiwasi hata kiwango cha elimu yake anaelimu gan mlopokaji huyo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom