Mwigamba: Baada ya Zitto ni Dr. Slaa

Oook asaanteeeniiii!! Wahini Lumumba sasa mkachukue ujira wa siku, kazi nzuri sana vijana wangu
 

Utasema yoke, nasikia hata kwenye mkakati wa MM23 Mwigamba amekatwa pesa
 
Hata chadema ikifa ccm haitakuwa salama watanzania sio kuwa tunaipenda chadema sana ila dhuluma ya ccm ndo inafanya tuangalia chama mbadala.
 
mwigamba ni mwanasiasa mwamba ambaye anainyima raha na usingizi ameweka wazi kuwa dr slaa kwa sasa anafanya siasa za kupelekwa pelekwa tu.

uliyoyaandika yanawiana (relevant) na upeo wako, wala hatuwezi kukushangaa au kuhoji lolote lakini huyo bro ndo kafuitika ivoo kwenye medani za siasa hapa.
 
Naona ameanza kuchanganyikiwa sasa, yeye ndo mwenye mpango wa kuimaliza CDM na hatafanikiwa.

100% Mwigamba kachanganyikiwa!

Hakujua kama mipango yao itagundulika mapema kabla hajalipwa maana ndani ya waraka kuna kipengele wakubwa zake akina Zitto wanasema wamtumie Milion 2 haraka kwani ana njaa sana!

Pole Mwigamba!CHADEMA ni zaidi ya mtu!CHADEMA ni taasisi
 
hawa wanafiki wanasubiri kutimuliwa hicho kirehere kitakwisha labda yeye na wenzake ndo wana mpango wa kumfukuza hawatafanikiwa kamwe hawana cheo chadema
 

mhhhh naanza ku-connect dots.
 
Mnafurahisha Hiki chama ni zaidi ya mtu ndo mlivyomdangaya MM kuwa yeye ni maarufu kuliko chama sio......Mwigamba anatimiza wajibu wake kwani fedha alizopewa zilikuwa kwa kazi gani.......mtahangaika sana chama kipo mioyoni mwa watanzania ninyi endeleeni kufarijiana huku mitandaoni
 
Kwa hiyo hii single ya Mwigamba sio kweli.. Inavyoelekea hukushirikishwa kwenye single hii wewe..

Ninamaana, Mbowe ni bomu zaidi Slaa, wote ni mabomu ila Mbowe kazidi, na Slaa naye anajisahau yuko bize anaimarisha chama cha familia ya wenyewe, ila wakimtimua tu, muziki una fade away! Haya tusubiri!
 
Mpasuko mkubwa unaokuja soon ni wa CCM,Ambao kama ingeleikuwa ni mvua basi tungesema wingu jeusi tayari na matone yashaanza kudondoka na walioanika nguo na unga wanakimbia kwenda kuanua.
 
DR Slaa kama akishinda urais adui wake mkuu atakuwa Mhe. Mbowe, hii imetokea kwa Nyerere na Kambona, Mwinyi na Mrema, Mkapa na Jenerali Ulimwengu au kwa mfano wa hivi Karibuni Kikwete na Lowasa. Hivyo ili ku consolidate power Dr Slaa atapenda kuwa shadowed na Mbowe ambae ametumia nguvu yake kubwa kuiimarisha Chadema
 
Huyu kweli anazidi kurahisisha kazi ya Kamati Kuu, sijui vipi na ile kesi yake waliosema ya uchochezi aliyo ng'ang'aniwa na mapolisi inaendaje... na ukosefu wa ajira nadhani ni vitu vinavyozidi kumchanganya mdogo wangu huyu.
Kwa kweli ni wakati wa kutulia sana kwake aangalie anaenda wapi sasa!
 
unasikitisha sana yaani unataka kugeuza mkakati wenu wa ma mm m1 m2 m3 kuwa ni mkakati wa cdm?nahisi umeanza kuchanganyikiwa waombe mm wenzako wakusaidie ile milioni mbili uendelee kuzungusha hadi mtakapoanzasha chama chenu.
 
Mwigamba naye amehamia rasmi Lumumba (LB7)? Kweli hali imekuwa mbaya sana. Kutoka uenyekiti wa Mkoa mpaka kulipwa buku saba kwa thread? Hii imekaa vibaya sana.
 
Mwigamba naye amehamia rasmi Lumumba (LB7)? Kweli hali imekuwa mbaya sana. Kutoka Uenyekiti wa mkoa mpaka kukumbizana na buku saba za Lumumba!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…