Mwigamba: Baada ya Zitto ni Dr. Slaa

Mtifuano utakua zaidi 2015 hapo ndipo chama kitakaposambaratika kabisa

Imekuwaje tena 2015 badala ya CDM kufa 2013? Mlidhani CDM ni nccr? mtaweweseka sana huku chama cha mizigo kikiwafia.WANANCHI BADO WANAYASUBIRI MAISHA BORA MLIYOWAAHIDI NA SIKU NAZO ZINAYOYOMA,OCT 2014 SIO MBALI!
 
Mtifuano utakua zaidi 2015 hapo ndipo chama kitakaposambaratika kabisa

Magamba inatakiwa mupelekwe kwa TB Joshua mukafanyiwe maombi ili pepo wachafu waliojaa vichwani mwenu wawatoke.Ni CHADEMA gani ambayo unasema ifikapo mwaka 2015 itasambaratika kabisa?mbona mumesha sema kuwa CHADEMA haitafika mwaka 2015 itakuwa imesha kufa?au kuna CHADEMA nyingine zaidi ya hii.
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Samson Mwigamba amesema kuwa mpango unaofuata kwa sasa ni kumuondoa Dr slaa ndani ya chadema.
amesema baada ya zitto kuondolewa ndani ya chama mtu atayefuata katika kushughulikiwa ni Dr Slaa ambaye kwa sasa amekuwa amekuwa akifanya shughuli za chama kwa kupelekwa pelekwa bila yeye mwenyewe kujua.

Mwigamba amesema kuwa upo mkakati kabambe unaendeshwa na baadhi ya watu kwa kushirikiana na watu walio nje ya chama ili kukimaliza chama kabla ya kufika kwenye uchaguzi mkuu 2015.
Amesema kuwa Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambaye yupo karibu sana na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ndio vinara wa mkakati wa kukiangamiza chama, huku John mnyika na Tundu Lissu wakijiweka mbele bila kujua hatima yao.

View attachment 127642 View attachment 127643
source; Rai Jumatano.desemba 18,2013.
ukiwa mfuasi wa chakavu hata akili inachakaa
 
Mfa maji bwana haachi kutapa mwigaba hao watu wawili slaa na mbowe ndio dira ya chama na slaa kakwepa mikuki mingi haiwezi tokea kitu ya kipuuzi kama hiyo umelikoroga lako ulinywe mwenyewe.
 
Kabla hamjaanza kumshambulia Mwigamba jiulizeni hivi M2 ameshapatikana?Isijekuwa kuwa M2 anayezungumziwa na kina Tundu Lissu ndio Dr Slaa?...I am just connecting the dots here.Huenda hawataki kuitumia njia ile waliyoitumia kwa akina Zitto kwa kuhofia mipango yao kubuma,Nahisi njia watakayoitumia kwa Dr Slaa itafanana na ile iliyotumika kwa yule Rasta wa Mara.Afterall kitambo tu tumeshajua kuwa Billicanas Boy yupo katika pay-roll ya Mzee wa Monduli anayeusaka Urais kwa udi na uvumba.
 
Maskini Mwigamba anasema chochote ili mradi asisahaulike kwenye vyombo vya habari'
pole yake ndo tumeshamsahau tayari
 
Siamimi kwa sababu nakumbuka Mbowe alipogombea urais, aligombea tuu ili kujifurahisha na kuvuta ule mkwanja wa King maker!. Dr Alipogombea aligombea kiukweli kweli na 2015 japo naujua msimamo wake, sitaki kuamini kuwa Mbowe anataka kujaribu tena mchezo ule ule huku anaelewa fika stutus ya makabila fulani fulani na urais urais wa JMT unless ile siri ya partenity iwekwe wazi ili achagulike! vinginevyo ni kujifurahisha tena!. As of now Chadema haina mtu wa 2015 ila msijekushangaa yule yule jamaa yangu ndio mgombea wao!. Hili mbona lilikuwa simple tuu kwa kumweleza Zitto all the plans ili asiwatibulie na sio kumzushia hadi kumfukuza!.

Pasco

Alipofukuzwa na kuvuliwa uanachama ndugu Himid wa Zanzibar wala hamkusema wala hamkumtetea namna hiyo?Nadhani mipango yenu imekwama na ndio maana mnalia sana juu ya Zitto.Kama Zitto ni kifaa kwanini nyie kina Pasco Msimchukue na kumpa uenyekiti kwenye chama chenu?Lazima iwe Chadema?Mbona ni furaha sana hiyo kwenu kumpata Jembe?Kwanini Uenyekiti uwe kwa Chadema tu?
 
Mkuu, Dr Slaa uwezo alionao ni wa kupora wake za watu tu. mengine hayajui

Wewe mbona maisha ya wakazi wengi wa hapo Lizaboni ni choka mbaya na wewe upo tu hutaki kushughulika nao uwakomboe?Pale kijiwe cha Petrol Station Lizaboni wanamama wanauza maandazi tangu asubuhi hadi jioni, na wewe huoni tatizo kwa nini?
 
siasa za maji taka hao kama wanajiona vinara kwanini wasianzishe chama chao?mpira wa miguu una taratibu zake na sheria zake hata ZIZOU alishawahi pewa kadi nyekundu kwa kukiuka sheria za mpira kwani ZZK ni nani mpaka aachwe tu acheze rafu?ccm tatueni migogoro ya ardhi mliyo asisi sio mnaimba ngonjera na chama chenu cha mizigo
 
mwigamba ni mhaini,anazidi kufanya kazi ya kamati kuu nyepesi,bora mwenzao kitila aliyeamua kukaa kimya.
Aaaaaaghhhhhh ndio najiamkia zangu nakutana na hii habari,hivi ya Kitila na UDSM imeishia wapi au walishajiridhisha kuwa hakuwa kiongozi wa chama? kama alivyodai.
 
Back
Top Bottom