Mwigamba: Baada ya Zitto ni Dr. Slaa

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Aliyekuwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Samson Mwigamba amesema kuwa mpango unaofuata kwa sasa ni kumuondoa Dr slaa ndani ya chadema.

amesema baada ya zitto kuondolewa ndani ya chama mtu atayefuata katika kushughulikiwa ni Dr Slaa ambaye kwa sasa amekuwa amekuwa akifanya shughuli za chama kwa kupelekwa pelekwa bila yeye mwenyewe kujua.

Mwigamba amesema kuwa upo mkakati kabambe unaendeshwa na baadhi ya watu kwa kushirikiana na watu walio nje ya chama ili kukimaliza chama kabla ya kufika kwenye uchaguzi mkuu 2015.

Amesema kuwa Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambaye yupo karibu sana na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ndio vinara wa mkakati wa kukiangamiza chama, huku John mnyika na Tundu Lissu wakijiweka mbele bila kujua hatima yao.

attachment.php
attachment.php

source; Rai Jumatano.desemba 18,2013.
 

Attachments

  • mwigamba.jpg
    mwigamba.jpg
    285.4 KB · Views: 12,395
  • mwigamba1.jpg
    mwigamba1.jpg
    323.6 KB · Views: 9,516
Mtifuano utakua zaidi 2015 hapo ndipo chama kitakaposambaratika kabisa
 
ANAYEKULA NYAMA ZA WATU HAACHI... HIYO NDIO DHAMBI ya UBAGUZI AMBAYO MWAL NYERERE ALIIKEMEA, UKIMALIZA KUWATENGA MAJIRANI, LAZIMA UWARUDIE NDUGU ZAKO.
 
mzee slaa akifukuzwa chadema ataishije jamani wamvumilie tu ili aendelee kupata huo mshahara kuweza kuendesha maisha yake.
 
mwigamba ni mhaini,anazidi kufanya kazi ya kamati kuu nyepesi,bora mwenzao kitila aliyeamua kukaa kimya.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom