Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,122
- Thread starter
- #41
Daudi Nyuso alikuwa kwenye vazi lake la suti ya bei ghali kutoka Uturuki, sigara mkononi na kikombe cha kawaha mezani. Miguu yake aliibebanisha na mgongo wake aliuegemeza kwenye sofa la sufi, macho yake yakilitazama dari. Alikuwa anatafakari jambo kuhusu mgeni aliyekuwa kwenye moja ya vyumba vya nyumba yake, mgeni ambae kwa taarifa alizokuwa nazo ni kwamba alikuwa Entebe kwa sababu yake na alitakiwa kuondolewa uhai wake na huyo mgeni ambae alitambulika kwa jina la Zuki Gadu, raia wa Tanzania. Mbali na yeye kuwa sebuleni, walinzi wake aliowaamini na wao walikuwa wamegewana kona za sebule kuhakikisha ulinzi madhubuti kwa bosi wao. Alimtazama mmoja kati yao, akamuita kwa ishara.
“Ondoa vitu vyote hapa mezani.” Alimwambia huku akizima sigara yake na kuitupia kwenye kitezo, kabla mlinzi hajaanza kufanya alichoalekezwa tayari yeye alishainuka na kuiweka suti yake, akapiga hatua kuelekea kwenye chumba kilichomhifadhi mgeni wake wa ajabu.
“Bakini hapa sebuleni.” Aliwaamuru walinzi wake waliotaka kumfuata. Agizo lake ni sheria na hakukuwa na wa kulipinga. Alikifikia chumba alichokikusudia, akafungua mlango ambao ulifungwa kwa nywila. Akaingia ndani ya chumba kilichokuwa na giza, akawasha taa na mwanga ukatamalaki. Chini ya sakafu iliyomwagiwa maji kulikuwa na kiumbe aliyelala usingizi mzito na asijue amelala kwenye maji. Alimtazama kwa zaidi ya dakika mbili pasipo na kufanya lolote, mawazo yake yalikuwa juu ya mgeni wake huyo ambae alikuwa bado hajarejewa na fahamu zake.
“Una sura ya upole isiyoendana na harakati zako. Sifa zako na wewe ulivyo ni vitu viwili tofauti.” Daudi aliongea kwa sauti ya chini huku akichuchumaa na kumgusa Zuki Gadu ambae bado alikuwa kwenye usingizi wa kifo.
“Una roho ngumu sana sijapata kuona, unaweza kumuua mtu kwa meno yako licha ya kuwa hukuwa na nguvu. Mmh! Ona ulivyojipakaza damu za mwanaume mwenzako mdomoni mwako.” Aliendelea kuongea huku akiwa anayachota maji kwa mkono wake na kuyamwaga kichwani kwa Zuki Gadu ambae alionesha mguso wa maji ulikuwa ukimpa hisia kwa kuwa alikuwa akitikisika kila matone ya maji yalipokuwa yakimgusa.
“Amka basi tuzungumze! Amka nikuoneshe mi nae ni mwanaume kama wewe.” Daudi alisema huku akiwa bado anaendelea na zoezi lake ambalo lilianza kuonesha kufanikiwa, mtu wake alikuwa akihangaika kuyafumbua macho yake.
“Utanichelewesha!” Alisema huku akiinuka, akatazama kwenye kona ya chumba kile kulipokuwa na meza iliyokuwa imebeba sanduku kubwa la chuma, akapiga hatua na kuifikia na moja kwa moja akalifungua sanduku. Macho yake yakakutana na vifaa mbalimbali vya kutesea, akavutiwa na nyaya za umeme, akazichukua na kulifunga sanduku kisha akaenda kuzichomeka sehemu maalumu ukutani,kisha akazichuna kidogo na kuzitupa chini kabla ya kuwasha ili kuruhusu umeme kuzitembelea. Hakuwa na wasiwasi kuhusu yeye kwa sababu alikuwa na viatu ambavyo havikuwa rafiki wa kupitisha umeme, alikuwa na raba zenye ufito mzito wa mpira. Kitendo cha nyaya za umeme kugusana na maji, umeme mkali ukasambaa haraka hadi alipokuwa Zuki Gadu na kumshitua kwa nguvu kubwa kiasi akazinduka haraka huku akiwa hana cha kufanya zaidi ya kuzisilikizia nguvu za umeme zilivyoutesa mwili wake.
“Hapo sawa.” Daudi alisema huku akizima umeme na kutulia akimtazama mgeni wake ambae alikuwa akihema kwa nguvu kubwa mithili ya mwenda mbio za masafa marefu.
“Naitwa Daudi Nyuso!” Alijitambulisha huku akichuchumaa kando ya uso wa Zuki ambae alianza kurejewa na nguvu zake baada ya hekaheka za kuamshwa na nguvu ya umeme. Mwili wake bado ulikuwa unatetemeka lakini aliweza kuinua macho yake na kumtazama mtu aliyejitambulisha kwake.
“Najua unaitwa Zuki Gadu au tuseme unaitwa Miguu ya kuku.. nitapenda kukuita hivyo.” Daudi alisema huku akiyarusha macho yake kwenye miguu ya Zuki, akaachia tabasamu la dharau.
“Inawezekanaje wembamba wa vimiguu vyako hivyo uwe tishio kwa maisha ya watu? Yaani hata kuku wangu wa kisasa wanasupu miguuni kuliko wewe... Hahaaaa. Au mpo wawili?” Aliuliza swali akimalizia kwa kucheka kicheko cha kinafiki.
“Miguu ya kuku.. hebu nambie umetumwa na nani kuniua.” Alisema huku akimgusagusa.
“Simjui.” Zuki akaiapata sauti yake.
“Humjui? Unawezaje kufanya kazi ya mtu usiyemjua?” Daudi alimuuliza.
“Si kanuni yangu kumjua anaenituma ila ni kanuni yangu kumjua niliyetumwa.” Zuki alijibu huku akifanya jitihada za kuinuka na kukaa kitako bila kujali alikuwa akikaa kwenye dimbwi la maji.
“Basi nipo hapa. Unaweza kuniua.” Daudi alisema huku akijipiga kifuani na macho yake makali yakitua usoni mwa Zuki ambae bado alikuwa anatazama chini pasipo na kumtazama mwenyeji wake.
“kama umepata nafasi kama hii, hakikisha umeniua. Usiponiua sasa hakika litakuwa kosa lako ambalo hutawahi kulijutia.” Zuki alisema huku akiinua uso wake na kumtazama Daudi Nyuso.
“Umelipwa shilingi ngapi? Nitakulipa mara saba zaidi ili umuue aliyekutuma.” Daudi alirusha ndoano yenye mnofu. Zuki Gadu alitabasamu kwa dhihaka kisha akamalizia kwa cheko kubwa.
“Nina kanuni zangu chache zenye manufaa. Nikishapokea pesa huwa sigeuki. Hata ungenipa utawala wa Uganda bado sitaweza kubadili maamuzi yangu. Kama unayonafasi ya kuniua, hakikisha umefanya hivyo na si janjajanja unayotaka kuifanya.” Zuki alimuonya.
“Basi sawa. Ngoja nikuoneshe mimi ni nani.” Daudi alisema huku akiinuka, akapiga miguu chini mara mbili na likatokea kitu ambacho Zuki Gadu hajawahi kufikiria kukutana nacho maishani mwake, wala hakuwahi kudhani zile soga za zamani enzi ya sungura na fisi zitakuwa na uhalisia kwenye maisha ya kidijitali.
“Ni nini hiki!!” Zuki alisema huku akiinuka haraka pale alipokuwa amejibweteka, ule uchovu na maumivu yote hakujua viliishia wapi, alichosikia kwa wakati huo ni mapigo ya moyo wake yalivyokuwa yakipiga kwa kasi kubwa mithili ya mdundo wa ngoma kwenye tamthilia za Ottoman.
Daudi Nyuso alikuwa amepotea kimaajabu mbele ya uso wake na hakujua alielekea wapi.
“Amewezaje? Huyu ni mtu ama jini?” Alijiuliza huku akikimbilia ukutani na kuegemea, macho yakapata nafasi nzuri ya kukitazama chumba kizima na asimuone.
“Mimi ni zaidi ya jini bwana mdogo. Utajisumbua bure kupambana na mimi.” Sauti ilisikika lakini mzungumzaji asionekane, hata upande sauti ilipotokea haikubashirika ni kama mzungumzaji alikuwa ameondoa mwangwi kwenye sauti yake kiasi kwamba usingeliweza kujua alikuwa akizungumza akiwa upande gani.
“Jito...” Zuki Gadu alitaka kusema kitu lakini haikuwezekana kabla ya pigo moja zito kutua kifuani kwake, aliyempiga hakumuona. Wakati akijiuliza mpigaji alikuwa upande gani, akashangaa akivutwa kwa nguvu na kutupwa chini kirahisi mithili ya gunia la mchicha. Akiwa anataka kuwahi kusimama akashangaa anakula konde lingine safi lililoyatikisa meno yake ya mbele na kumuacha akichuruzikwa na mchuzi wa damu.
“Leo ni siku ya furaha kwangu, sitaki nikuue. Endelea kukaa humu ndani hadi usiku wa leo nikuoneshe kwa nini niliwahi kuwa IGP wa muda mfupi zaidi kwenye historia ya Dunia. Jiandae pia kunambia aliyekutuma.” Sauti ilisikika na kufuatiwa na vishindo vya mtu aliyekuwa akitembea kwenye maji, muda mfupi baadae mlango ulikuwa unabamizwa kwa hasira. Na kwa sababu ya kubamizwa huko ukashindwa kujifunga vema na ukabaki wazi.
“Hii ni nafasi yangu pekee ya kutoka humu ndani, la sivyo huyu mchawi ataniua leo.” Aliwaza huku akiharakisha kukimbilia mlangoni, alifanikiwa kutoka na kuanza kutembea kwa tahadhari kuifuata korido ndefu iliyopambwa kwa mwanga mkali wa taa zenye kutumia kiasi kikubwa cha umeme. Hatua zake sita zilitosha kumfanya afurahie wazo lake la kujikomboa kabla hatua yake ya saba haijatowesha furaha hiyo. Zuki Gadu alibaki akiwa amekodoa macho na asielewe ni kitu gani kilichokuwa kimetokea kwenye maisha yake. Alijikuta akiwa amerudi kwenye chumba cha mateso na asijue alirudije. Ni kama alikuwa akitembea ndani ya chumba na si kutoka nje kama alivyodhani.
“Haiwezekani!” Zuki aliwaza kwa sauti huku akiruka hatua ndefu na kuufikia mlango ambao bado ulikuwa wazi, akaugusa na kuutikisa, ukatikisika kama alivyotaka. Akatoka nje na kugeuka kuutazama kama kweli ulikuwa nyuma yake na yeye alikuwa akitazamana na korido ndefu yenye mwanga wa kutosha. Ni kweli mlango ulikuwa nyuma yake kumaanisha alishatoka ndani ya chumba. Akapiga hatua moja ndefu, hatua ya pili kikatokea kitu kingine ambacho hakuwa akimedhania wala kukifikiria zaidi ya kukiona runingani kwenye sinema za Sultani Tamba. Mbele yake kulikuwa na bwawa la maji na hakuona mwisho wake.
“Nitakuwa naota!” Aliwaza huku akigeuka na kutazama nyuma yake, mlango ulikuwepo na chumba alichotaka kilikuwepo lakini rent vilikuwa zimezungukwa na maji, ni kama alikuwa katikati ya kisiwa.
“Ni nini hiki kinanitokea?” Alijiuliza huku akipiga hatua na kurejea ndani ya chumba cha mateso, akaurudishia mlango lakini hakutaka ujifunge. Akasimama katikati ya chumba na kufikiria cha kufanya lakini kila alichojaribu kuwaza hakuona kama kutakuwa na msaada kwake, kila kitu kilikuwa kigumu kwake kukabiliana nacho kwa wakati huo.