Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,122
RIWAYA; MWIBA WA CHUMA.
Na; Bahati Kisarwa Mwamba.
Simu; WhatsApp 0658564341
1.
Siku kwake ilikuwa inaelekea kuisha vema. Jioni ya siku hiyo aliamua kuimalizia kwa kufanya mazoezi ya kukimbia kilomita nane. Alikimbia bila kujali waliomfahamu walikuwa wakimshangaa kwa namna ipi kwa sababu, hawakuwahi kumuona akikimbia zaidi ya kumuona akishinda mtaani kwa kujichanganya na watu mbalimbali huku akiwa amevaa kanzu, vazi ambalo liliwafanya majirani zake kumkariri hata kama alikuwa akitembea usiku mnene. Wapo waliompigia mluzi wa shangwe kwa kumuona akiwa amependeza kwenye vazi la trakisuti yenye bendera ya Tanzania.
“Leo Sheikh umeamua kupunguza mafuta?” Alisikika mama mmoja akimpazia sauti kutoka umbali mfupi na eneo alilokuwa akipita, akamjibu kwa kutabasamu na kumpungia mkono. Safari yake iliendelea kwa umbali aliohitaji, aligeuka na kuanza kurejea nyumbani kwake ambapo alipanga kuingia kwenye chumba cha mazoezi na kuzikata dakika mia moja na ishirini kama alivyokwisha zoea. Njiani alipishana na watembea kwa miguu, waendesha pikipiki, baiskeli na gari chache sana. Kuna wakati alipishana na wapasha misuli wenzake ambao kwao ilikuwa ni kawaida kukimbia kila inapofika jioni. Akiwa katikati ya safari yake kuna pikipiki moja ilimpita kwa kasi kubwa huku akiwa ameikwepa kwa sentimita chache sana, laiti kama asingelikuwa si mtu mwenye kuhisi hatari mapema pengine angeliishia kugongwa vibaya.
“Jamaa kalewa bangi tayari....” Aliwaza huku akitikisa kichwa kwa masikitiko na kuendelea kunyakua miguu kama kawaida, aliamua kumsamehe mwendesha hovyo huku akimuombea afike salama aendako.Alipokaribia njia ya kuelekea nyumbani kwake umbali wa mita mia moja kutoka barabarani, alipunguza mwendo na kuanza kukimbia taratibu ili kupooza viungo vyake kabla hajaanza kutembea kuifuata njia nyembamba iliyokuwa ikikatiza nyuma ya kuta za nyumba za majirani zake. Giza nalo lilizidi kukolea licha ya kwamba taa za majirani ziliwashwa na kuangaza kwa kiasi kikubwa kwenye njia aliyokuwa akikimbia na nusu kutembea huku akibana pumzi kidogo na kuiachia kwa namna ya kuyaandaa mapafu yake kupitisha hewa kwa kiasi kidogo baada ya kutoka kuyatumikisha kwa mbio za kasi. Hakuwa na wasiwasi kwenye njia aliyoizoea kwa zaidi ya miaka mitano tangu alipohamia kwenye nyumba yake mpya baada ya kuhama kutoka sehemu aliyokuwa akiishi zamani. Angelihofu nini ikiwa mitaa ilikuwa tulivu na hakuwahi kusikia kuna kibaka ama mwizi kaiba? Angelihofu nini ikiwa vijana wa mtaani walimfahamu na kumheshimu kuliko kawaida, ni nani ambae angeliweza kuinua hata mdomo wake kumtisha ingali kila mtu alimfahamu, kila mtu alimpenda na kulitaja jina lake la utani kwa furaha? Hakika wasiwasi wa kukatiza kwenye uchochoro wa kumfikisha kwake akili yake haikuwahi kuuwaza. Licha ya kutembea kwa kujiamini lakini kuna hali fulani ilianza kujijenga kichwani kwake, alianza kuhisi kuna hatari siku chache zijazo. Mwili na akili yake vilishirikiana kujenga picha ya matukio machache ya kubashiri ambayo hakutarajia kama yangelikuwa na matokeo mazuri.
“Na ni muda mrefu sana sijapata kazi wala kashikashi yoyote... Maisha yakiendelea hivi nina imani nitaanza kwenda msikitini au kanisani kwa kadri imani itakavyonielekeza.” Aliwaza huku akisimama katikati ya njia na kugeuka nyuma alikotoka, hakuona mtu wala kuhisi dalili ya uwepo wa mtu. Kwake wasiwasi ni akili na kila mara hutembea kwa tahadhari hata kama atakuwa hatazami nyuma lakini huyaacha masikio yake yanase kila tukio kama antena. Akaanza kuishusha zipu ya sweta lake huku akiumaliza ukuta wa nyumba ya tatu kabla ya kufika kwake. Vitendo vyote hakufanikiwa kuvimaliza, hakumaliza kona ya nyumba wala kumaliza kuishusha zipu ya sweta la trakisuti aliyovaa kabla ya macho yake hayajaona kivuli cha mtu mbele yake. Mtu yule alikuwa amekaa juu ya pikipiki yake na kuifumbata mikono yake kifuani, kichwa chake akiwa amekiziba kwa kofia ngumu ya kuendeshea pikipiki.
Alisimama ghafla huku mkono ukiganda na zipu na mguu mmoja ukishindwa kuinuka chini kuufuata mguu mwingine uliokwisha tangulia, macho hayakupepesa na ngozi yake ikajikunja kwa baridi ya ghafla iliyotowesha jasho lote alilotumikia kwa zaidi ya nusu saa. Sekunde chache baadae akili yake ilianza kufanya kazi na kumbukumbu zikarejea; mavazi na aina ya pikipiki ya yule mtu ni sawasawa na ile ambayo ilimpita dakika chache wakati akikaribia kumaliza mbio zake za ucheshimwili.
“Haiwezi kuwa bahati mbaya..” Aliwaza huku akisimama mguu pande na mikono akiishusha chini kwa namna ya kujiweka tayari kwa lolote mbele yake. Hakusogea mbele wale kurudi nyuma, alibaki akiwa amesimama na macho yake yakiwa mbele sawasawa na mwili wa mtu aliyekuwa amekaa tulivu kwenye kwenye pikipiki yake. Masikio yake nayo yalikuwa tayari kupokea mjongeo wowote kando yake.
“Safi sana...”Alijisemea mara baada ya kumuona mtu aliyekuwa kwenye pikipiki akishuka kwa namna yake, alishuhudia sarakasi safi isiyoacha kishindo wakati wa kutua chini. Macho yake yakiwa kodo kwa kiumbe aliyekuwa amesimama kando ya pikipiki yake, mwili wake ukajivunja kwa kwenda chini na mkono wake wa kulia ukazihesabu punje nne za changarawe na kuzitupia mdomoni kisha akasimama wima akiwa tayari kupokea barua ya mwaliko wa makonde. Hakutaka kuwa wa kwanza kupiga hatua kumfuata mtu ambae hakujua dhamira yake halisi ni ipi, akatulia huku umakini ukiwa juu zaidi kuliko kawaida, hakupepesa.
Alichokuwa akikisubiri ndicho na mwenzake alikuwa anasubiri lakini mwendesha pikipiki alipoona anategewa, akafanya kile ambacho alihitaji kufanya bila kupoteza muda. Kwanza akapiga hatua moja ndefu na kuiweka nyuma pikipiki yake kisha akayatazama mabega yake kwa namna ya kutaka kuona kuta mbili zilizomweka katikati, akachanua tabasamu lake kwa namna ya kudhihaki kisha akafanya kitendo ambacho mtu aliyekuwa mbele yake hakukiona vema. Alinesa na kwenda juu kisha akakanyaga ukuta uliokuwa kushoto kwake na kuutembea kwa kasi kumfuata Zuki Gadu ambae bado alikuwa anashangaa kitendo cha mwendesha pikipiki kukimbia ukutani mithili ya mjusi, alipomkaribia akajiachia na kutua chini kisha akanesa tena na kuruka juu kisha akajipinda na kuukanyaga ukuta wa upande wake wa kulia, kwa kasi ileile akapiga hatua tatu na kutua chini akiwa uso kwa uso na mbaya wake ambae alikuwa anatema punje moja ya changarawe na kubakiza tatu, akamchekea kwa dharau kisha akamtisha kama anataka kupaa tena lakini kabla hajafanya hivyo akaachia makonde matatu ya haraka haraka na yote yakajaa vema kifuani mwa Zuki Gadu ambae hakuelewa alipigwaje. Mpigaji hakuridhika na hakutaka kumpa mwanya wa kufanya lolote, akanesa na kuukanyaga ukuta kisha akafyatua teke kali lililotua vema kwenye mkono wa Zuki ambae alikuwa anajaribu kuukinga mkono wake ili kupunguza uzito wa teke hilo, lakini aliishia kuteguka mkono kwa namna teke alilopokea lilivyokuwa na ujazo mkubwa.
“Huyu jamaa mbona kama anavyuma mwilini?” Alijiuliza huku akitema kipande kingine cha changarawe na kusaliwa na vipande viwili mdomoni. Akanesa na kurudi nyuma lakini hilo likawa ni kosa ambalo hakupata muda mzuri wa kulijutia kabla ya kukutana na mateke mawili yaliyotua vema kifuani mwake kwa kupishana kwa sekunde chache, mateke hayo yalikuwa na uzito uliotosha na kumsukuma nyuma kisha kumbwaga chini kwa kishindo mithili ya mlevi aliyeanguka juu ya kaburi.
“Anapiga na haongei...!” Zuki alijisemea taratibu huku akijaribu kukabiliana na maumivu makali yaliyokuwa yaliyoanzia kifuani na kusambaa sehemu zingine za mwili. Licha ya maumivu hayo lakini alifanikiwa kujizoazoa na kusimama huku akitema punje nyingine ya changarawe na kusaliwa na punje moja pekee, macho yake yakiendelea kumshuhudia jamaa akiwa amesimama wima mbele yake bila kutaka kufanya lolote lile la ziada. Zuki Gadu aliingiwa na hofu kwa namna ambavyo adui yake alijipa utulivu mkubwa kiasi kwamba hakueleweka anakusudia kufanya nini na kwa mara ya kwanza alikiri kukutana na adui mwenye nguvu,kasi na ujuzi wa mapigano. Lakini hiyo haikuwa sababu ya yeye kushindwa kujipanga upya ili kutokuingia kwenye aibu ya kupigwa kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake na hakutaka hilo litokee, lakini alishindwa kuelewa jambo moja muhimu kwenye maisha; siku hazifanani na hazina kurasa za kufanana kwenye maisha ya binaadamu.
Lakini angelijuaje ikiwa mara zote amekuwa mshindi kwa kila pambano aliloshiriki? Angelijua vipi ikiwa maisha yake yaliyojaa hekaheka za kila namna hayajawahi kumwingiza kwenye aibu ya kupigwa ama kushindwa kumudu jambo liloingia kwenye anga zake? Lakini hakujua... hakujua..
Zuki Gadu p.a.k Miguu ya kuku alijiweka vema tayari kwa mpambano, akatega mtego wake ambao aliamini ni lazima adui auvae kwa namna yoyote. Akakaa mguu pande kisha akawa kama anachuchumaa na kuutanguliza mguu mmoja mbele huku akiiandaa mikono yake kufanya kile alichokusudia, akatega. Hila yake ilikuja kumshangaza hata yeye mwenyewe pale ambapo aliyemtegea alipofanya kitu ambacho hakukitarajia, jamaa alirudi nyuma hatua tatu kisha akaanza kukimbia kwa kasi ya duma, alipomkaribia aliteleza mithili ya mchezaji ashangiliae ushindi kisha akaachia mapigo matatu kwa namna ya kuvigawanya viungo vyake, ngumi ilitua vema chini ya kidevu cha Zuki Gadu huku miguu yake ikifanya kazi ya kuitengua miguu yake iliyokuwa imewekwa mkao wa mrukochura. Miguu ya kuku alipiga ukelele wa maumivu makali yalitokea sehemu tatu tofauti mwilini mwake na wakati huohuo jamaa yeye alikuwa akasimama wima nyuma yake huku akinesanesa tayari kwa kuachia pigo lingine ambalo alikuwa kalidhamiria. Akampiga kwa namna aliyoitaka yeye na taratibu Zuki Gadu akaenda chini mzimazima huku maumivu ya nyuma ya kichwa yakiwa ni makali kuliko kawaida, macho yake nayo yakaingiwa na ukungu na akashindwa kuona vema licha ya kujitahidi kadri ya uwezo wake kuona adui yake alitaka kumfanya nini. Licha ya maumivu na akili yake kuanza kushindwa kufanya kazi vema, lakini alijitahidi kujigeuza ili amuone vema.
“Hatimae leo nimepatikana!”Aliwaza huku akifanikiwa kumuona jamaa kama kivuli kilichokuwa kikimwinamia, akajaribu kurusha mikono lakini ikawa mizito, akatupa mguu lakini akagundua imekuwa mizito maradufu kwa sababu adui yake alikuwa ameikanyaga na kusimama juu yake huku akinesanesa kama vile amekosa mhimili sahihi.
“Aaggh!” Zuki aliunguruma kwa jaziba na wakati huohuo guu zito likatua kifuani na kumnyima hata pumzi ya kutatarika, akatulia huku akihema kwa taabu, alimuomba Mungu ampe angalau dakika chache za uhai ili aweze kujitetea kutoka kwenye mikono ya mtu ambae hakuwahi kudhani kama atakutana nae kwenye maisha yake, maisha ambayo amezoea kushinda kila mara. Maombi yake yalisikilizwa lakini hayakusikilizwa kwa namna aliyoitaka, akazidi kuishia nguvu na pigo la kichwa alilopigwa awali lilizidi kumchanganya kwa maumivu ambayo bado yalikuwa yakizidi kuharibu utimamu wa mwili wake, nguvu zikzidi kumkimbia na giza likazidi kufunika mboni za macho yake, hakujua kilichoendelea wala hakujua alichofanyiwa tena na adui yake ambae alikuwa akimwadhibu kwa nyodo na majivuno.
Tukutane jioni....