Mwiba wa chuma(Zuki Gadu)

Mwiba wa chuma(Zuki Gadu)

“Ni nani watu hawa? Lakini sauti hii si mgeni masikioni mwangu, ni nani mtu huyo?” Alijiuliza huku akirejea kuitazama simu yake ambayo haikuacha rekodi yoyote ya mtu aliyepiga kwa namba fiche.
“Dodii! Aagh!” Aliunguruma kwa ghadhabu huku akishindwa kuelewa kitu gani kilitokea hadi akajikuta matatani.
“Lakini hata kama angelijitahidi asingeliweza kwa yule jamaa.” Alijisemea peke yake huku akipiga hatua kuelekea bafuni, simu aliiacha kitandani. Fikra zake zilimbeba hadi kwenye tukio lililotokea muda mfupi uliopita, tukio la kupigwa kama mtoto. Kichwani mwake aliamini ni kumbukumbu mbaya kuwahi kumtokea, lakini hakutaka awe kushindwa, alitaka siku moja alipe kisasi kwa namna ambayo aliyempiga ajutie maisha yake yote. Alijiapiza akiwa ametulia chini ya bomba la mvua maji yakitiririka kuanzia kichwani hadi miguu kabla ya kutafuta sehemu ya kutokea na kuelekea shimoni, utulivu huo uliambatana na kufumba macho huku akiomba kwa lugha alioijua yeye na hakuwa akimuomba Mungu wala miungu, aliomba kukutana na yule mtu kwa mara nyingine hata kwa bahati mbaya ili amfundishe namna ya kupigana bila kuacha uhai wenye kugharimu maisha yake huko mbeleni.
“Naitwa Zuki Gadu....!” Alisema huku akipiga ukuta wa bafu kwa ngumi, macho yake akiwa ameyaelekeza chini na asione hata tone la maji lililokuwa likidondoka kutoka mwilini mwake. Hasira zilizidi uwezo wake wa kufikiri lakini hakuwa na namna wala njia halisi ya kufanya lolote ili kuzipunguza. Alimaliza kuoga na kurejea chumbani, akazivaa nguo alizokuwa amewaza kuzivaa kwa usiku huo kisha akatoka, akafunga vema chumba chake na milango mingine, akatoka na kuelekea barabarani. Muda mfupi baadae alikuwa anaenda kwenye moja ya baa kubwa ambayo ilisifika kwa ufuska nyakati za jioni. Alifika salama na kufanikiwa kuingia ndani, hakuwa mnywa pombe wala lile si eneo ambalo alipendelea kulitembelea, alikuwa na sababu yake kufika hapo. Alienda kukaa viti virefu kando ya kaunta, aliagiza konyagi mzinga na glasi yenye barafu ndani yake, huduma aliipata ndani ya muda aliouhitaji, akamimina na kupiga funda moja alilolimeza kwa taabu sana. Muda wote aliokuwa amekaa hapo macho yake yalikuwa yakiranda huku na huko mithili ya kware aliyepoteana na wanae, aliona kila mtu aliyetaka lakini asilimia kubwa wote walikuwa ni walevi ambao walikuwa wakihangaika na kuidhoofisha miili yao kwa vinywaji vikali. Alikaa kwa zaidi ya saa moja na dakika kadhaa kabla ya kukiona kile alichokisubiria. Mwanamke mwenye weusi wa kung’aa alikuwa kwenye vazi la kimitego huku mkoba wake mdogo ukipepea chini ya kwapa, miwani ya bei ghali ilikuwa kivuti kingine kwenye uso wake, viatu virefu vilimfanya atembee huku akitetemesha milima miwili isiyo na vilele zaidi ya msitari mwembamba uliosabisha mpishano wa milima hiyo miwili iliyokuwa ikishindana kutetemeka bila kujali kama iliacha mtindio wa ubongo kwenye vichwa vya wanaume waliokuwa wakimtazama. Mwanamke yule alighairi kukaa kwenye kiti alichokilenga baada ya kumuona mtu mmoja ambae alifanania sawa na mmoja wa watu ambao huonana nao mara chache sana. Akatembea mwendo wa kutesa abiria wa mbagala waliojazana Kariakoo, kila hatua yake moja iliacha mtafaruku mkubwa kwenye via vya kila mwanaume aliyekuwa akimtazama, hata kama hukuwa ukimtazama ungelilazimika kugeuka ili kumshuhudia kiumbe aliyekuwa akipepea na manukato ghali mwilini mwake katikati ya harufu ya pombe na jasho la wanaume na wanawake waliokuwa wakiishughulisha miili yao kwa muziki mzuri uliokuwa ukiburudisha nafasi zao.
Baadhi ya watu walishindwa kuvumilia na walijikuta wakiangusha miluzi ya shangwe kwa namna ambavyo mwanamke mrembo alivyokuwa akiyashindanisha matuta mawili yaliyojitenga na mwili na kusababisha aonekane kama kabeba vyungu chini ya mgongo wake, mwanamke yule hakujali wala hakuwa na muda huo kwa sababu alijua wale ni walevi na alishazoea shangwe kama hizo hata alipokuwa akikatiza mtaani hasa kwenye vijiwe vya bodaboda na vijiwe vya kahawa na mikusanyiko mingine iliyohusisha wanaume hasa vijana rijali. Alitembea huku akijiuliza maswali mengi kuhusu mgeni aliyemuona kaunta, alijipa maswali kwa sababu mtu huyo hakuwa mtu wa kuonekana hapo kirahisi na pia si mtu wa kuhangaika na ulabu kwa namna yoyote.
“Naomba Savannah ya baridi...”Aliagiza huku akikaa kando ya kiti alichokuwa amekalia mgeni aliyeamini alikuwa pale kwa sababu yake.
“Huwa napenda wepesi wako wa kuinusa harufu yangu...” Zuki alisema huku akichukua glasi na kuvuta funda dogo la kileo na kuacha kipite kwa taabu kwenye koromelo.
“Bila shaka umekabwa kooni, tema nikusaidie kupooza.” Mwanamke alisema huku akipokea chupa ya pombe alioagiza, akafakamia funda kadhaa.
“Nitafutie pikipiki namba 456 DLD, mnyonye hadi ubongo, nitatoka kwa siku sita pekee, siku ya nane nitakuwa hapa mjini na nitahitaji kukuona ili unipunguzie shibe.”Zuki alimwambia.
“Nile chakula cha shilingi ngapi?” Aliulizwa.
“Kama kawaida.. milioni 30” Zuki alijibu na kujiandaa kushuka kiti kirefu, lakini akasita baada ya kumuona binti mrembo Montana akiwa amezubaa akitazama mita chache nyuma ya mgongo wa Zuki na wakati huohuo kelele za fadhaiko zikisikika kutoka kwa watu waliokuwa karibu nae, hakuhitaji kujulishwa kulikuwa na hatari nyuma yake nae akafanya kitendo ambacho kiliwaacha midomo wazi waliokuwa wakimtazama. Akaruka juu kwa sarakasi ambayo ni ngumu kuilezea, akazunguka mara tatu hewani kabla ya kutua kwenye kiti akiwa ametanguliza mikono huku uso wake ukiwa sambamba na jamaa mmoja aliyekuwa kashiba kifua kwa mazoezi ya mitaani, hakumkawiza, akajikunja kwa namna ya kushangaza na kuachia teke kali lilitua vema mgongoni mwa kijeba, kabla kijeba hakijajua kinapigwaje na mtu aliyejuu ya kiti tena akiwa mikono chini, miguu juu, Zuki Gadu alinesa na kutua chini kwa madoido huku lile donge lake la hasira likiwa limepata pa kutokea na hakutaka kufanya makosa katika hilo. Kwa wepesi wa hali ya juu, aliudaka ukosi wa shati la kitenge alilokuwa kavaa asusa wake kisha akaanza kumcharaza makofi mengi yasiyo na idadi halisi, hayakuwa makofi pekee hata ngumi na vifuti vilikuwa ni sehemu ya adhabu yake kwa jamaa ambae alikuwa amemwinda na chupa ilioshia kupasukia kwenye madirisha ya kaunta. Walevi walipiga kelele za shangwe huku wengine wakiomba dozi iongezwe kwa mtu ambae hakuonekana kuwa na nia njema na usalama wao na hakika dozi ilitolewa sawa na kipimo cha tabibu aliyemdanganya kijana avae mashati ya vitenge mithili ya wale wapiga kampeni za uchaguzi wakati wa mchuano wa Jakaya na Dr. Slaa. Tena si kuvaa tu bali alivaa na kukatiza nalo kibabe katikati ya kundi kubwa la walevi wasiojua ustaarabu wa nguo za vitenge.
“Basi... Basi...! Utaniulia msugua nyamnole wangu baba we...”Montana aliingilia ugomvi ambao mshindi alishapatikana kwenye sekunde ya kwanza tu ya mzunguko wa kwanza wa pambano na ilikuwa inatafutwa KO ili mshindi kujihakikishia. Zuki Gadu alimgeukia Montana na kumkata jicho kali ambalo lilisema kila kitu kilichokuwa moyoni mwake, mkono wake wa kulia ukielea juu huku wa kushoto ukiwa bado umeung’ang’ania ukosi wa kitenge cha baunsa uchwara.
“Huo moto tafadhali usiumalizie kwa huyu mwanafunzi wa vidudu anaejua kulamba unene wa kidole kilichoota katikati ya upaja wangu pekee, ufundi wake bado nauhitaji bwana.” Montana aliendelea kusihi huku akijaribu kuushusha mkono wa Zuki uliokuwa umeganda hewani huku ukitetemeka kwa ghadhabu. Miguu ya kuku alielewa kilichomaamishwa na mwanamke mrembo Montana lakini, hakutaka mkono wake ulioelea hewani kwa zaidi ya nusu dakika ushuke bila kugusa kijana mvaa vitenge kama mhubiri wa kisipika Kariakoo, akaushusha kwa nguvu zake zote na ukatua vema utosini kwa jamaa yule ambae aliishia kuanguka chini huku akiwa mzito wa kila kiungo mwilini mwake, mdomoni na puani akimwaga michuzi iliyotia kinyaa kuitazama.
“Mpunguzie dozi ya feni lako ili apunguze wivu wa kibwege, atakufa kwa kudandia vya bure.” Zuki alisema kwa utulivu wa kutisha kisha hakungoja majibu ya Montana, akapiga hatua na kutoka nje ya baa na kuacha watu wakimshangilia kwa namna alivyotoa sinema ya bure yenye ladha ya sahihi ya mapigano licha ya kuwa mbali kiujuzi na mpinzani wake, hakuzijali hizo kelele na wala hakuijali sauti ya mhudumu iliyomtaka alipie kinywaji chake kabla hajaondoka. Wakati huo ilikuwa yapata saa tatu kuelekea saa nne kasoro usiku, alipata usafiri wa bei rahisi uliomrejesha nyumbani kwake. Alipofika kwake hakutaka kupoteza muda, alichukua begi lake dogo la kusafiria na kuweka nguo zake mbili pekee, ukiwa ni utaratibu wake wa kila mara pindi awapo na safari ya aina ile, safari ya hatari. Hakusahau kubeba kiasi kidogo cha pesa na kadihela ambayo huitumia kila awapo nje ya nchi. Alipokwisha kujiandaa hakutaka kukawia, aliingia mtandaoni na kuweka oda ya ndege binafsi ambayo ingelimfikisha hadi mjini Bukoba kwa usiku huo, alitaka kutumia njia ya Mtukula kuingilia Uganda na ndivyo ilivyokuwa.
 
Mimi pia nilimtumia pesa hajawahi kutuma nikaamua kumuachia kifupi Ana tamaa za kijinga
Hao watatu tayari tatizo Lao limetatuliwa na limejitokeza kwa bahati mbaya kwa siku sita baada ya wao kulipia. Wewe unachuki binafsi ambazo sijui umezitolea wapi. Kila Uzi nikipandisha lazima ujitokeze. Hiyo zamani unadai riwaya gani? Ulilipia shilingi ngapi., Ulihitaji riwaya gani ukaikosa?
Ardhi ya Wegero haina matepete kama wewe.. usiibaki ardhi hiyo iliyobarikiwa.
 
Umesahau eeeee kwenye mdunguaji wa goma(kama sijakosea jina) Sina chuki na ww ila napenda kukwambia ukweli tatizo hutaki kuupokea riwaya zako hazieleweki ww pia hujibu sms za watu inbox huoni huo ni utapeli?
Kuhusu wegero ni Sehemu ambayo nilienda nikaipenda wala siyo kwetu
 
Hata uhakika huna. Punguza porojo aisee... RIWAYA zangu hazieleweki unafungua Uzi wa Riwaya zangu ili ufaidike kitu gani ndugu. Punguza utoto. Yaani riwaya ya miaka mitatu nyuma ambayo hakuna aliyewahi kuinunua akaikosa Leo uibuke na hoja mufilisi? Lete uthibitisho wa jumbe nisizojibu. Punguza mihemuko na pengine anaekupaga simu uchezee anastahili bakora.
 
2.
Jua la utosi lilimkuta akiingia ndani ya jiji la Entebe, kilomita nyingi kutoka mpakani mwa Tanzania na Uganda. Alikuwa ametumia usafiri wa aina tofauti tofauti kabla ya kuingia Entebe huku mara nyingi akiwa ametumia gari binafsi zenye kasi na ambazo mara chache hukutana na vizuizi vya askari. Mji mzuri ulimpokea kwa hekaheka za watu waliokuwa wakijitafutia riziki halali na zisizo halali, hilo hakujali wala halikumhusu na hakutaka liwe kipaumbele chake kwa lolote. Miguu ya kuku akiwa na noti za dola kadhaa za kimarekani alifanikiwa kupata hoteli ya daraja la kati, alikodi chumba alichohitaji na kisha akajipa muda wa kupumzika huku akiwa na zoezi moja la kutalii ndani ya mji Entebe ifikapo jioni, alitarajia kufanya hivyo ili kuitambua mitaa na nyumba zake huku lengo lake likiwa ni kuiona nyumba namba 607 ambayo hakujua ilikuwa mtaa gani ndani ya jiji lililojengwa na kujengeka. Alilala bila kutia chochote tumboni mwake akiwa amefanya hivyo kwa lengo la kuwahi kuamka.
Wakati yeye akilala mchana ili aanze mizunguko yake jioni, mahali fulani ndani ya mji wa Entebe kulikuwa na taarifa iliyokuwa ikifika mahali na kujadiliwa.
“Kuna jipya gani huko mtaani?” Jamaa mmoja aliyekuwa amevaa kaptura kubwa yenye mifuko mingi aliuliza huku akivuta sigara na kuuachia moshi mwingi uliosambaa ndani ya sebule kubwa iliyopambwa kwa samani za kisasa.
“Jipya ni kuhusu huyu jamaa hapa. Ameingia leo mchana akitokea Tanzania.” Mnyetishaji wake alimjibu huku akimuonesha picha kupitia simu yake. Jamaa akaitazama ile picha kwa umakini mkubwa huku akiwa ameisahau sigara iliyokuwa ikiteketea katikati ya vidole vyake.
“Ni nani huyu jamaa?” Aliuliza na kuirejea sigara yake.
“Ni muuaji wa kulipwa na si muuaji wa kawaida, anasifa lukuki za mafanikio ya kazi zake, ni mtu hatari sana, akikanyaga kwenye ardhi yako basi kuna jambo anapanga kulifanya.” Mlinzi alijibu huku akirejesha simu yake mfukoni.
“Unahisi yupo hapa kwa sababu gani?” Jamaa aliuliza huku akizima sigara yake na kuitupia kwenye kitezo.
“Kuua!” Mlinzi alijibu.
“Mimi au mwingine?”
“Bado hatuwezi kusahau kelele za Zibuabanda.. anaweza kufanya hivi.”
“Lakini Zibuabanda sidhani kama anaweza hata kutoa kauli, hali yake ni mbaya sana tangu aliponusurika kuuawa miaka mitatu nyuma, ana enawezaje?”
“Kila kitu kinawezekana, kumbuka tulisafisha kila kitu na kama atapata ahueni ni lazima atakuweka kwenye kikaango ili kurejesha vilivyo vyake.”
“Mwanajeshi mpumbavu yule... Mfuatilieni huyo mgeni na msimuue kabla sijaonana nae.” Jamaa alisema na kuinuka, akaelekea chumbani na walinzi wake watatu waliokuwa sebuleni wakihakikisha ulinzi wake walimfuata na kuishia mlangoni wakati yeye akiingia chumbani.
Mnyetishaji ambae alikuwa ni mlinzi akusanyae taarifa za aina mbalimbali ndani na nje ya Entebe, aliondoka baada ya kuagana na bosi wake na alienda kutoa maelekezo yaliyomhusu mgeni wa ajabu aliyeingia Entebe akitokea Tanzania.
Saa kumi na mbili jioni ilimkuta Zuki Gadu akiwa umbali wa kilomita nane kutoka kwenye hoteli aliyokuwa amefikia. Alikuwa kwenye taxi aliyoikodi umbali mfupi kutoka kwenye hoteli aliyokuwa amefikia.
“Kutoka hapa hadi huko unakodhani nitaipata hiyo nyumba ni umbali gani umesalia?” Zuki alimuuliza dereva.
“haiwezi kuwa umbali wa dakika kumi kuanzia sasa, ni mtaa wa tatu ama wa pili hivi ambao una nyumba zinazoanza na namba 600+” Dereva alijibu kisha ukimya ukachukua hatamu huku kila mmoja akiwa na lake kichwani. Dakika nane baadae dereva alikuwa anaegesha gari kando ya barabara.
“Hapa tulipo ni mtaa wa Bagadano, mtaa ambao unaidadi kubwa za nyumba zenye namba 600 na hivi, hivyo naamini nyumba unayoihitaji inaweza kuwa miongoni mwazo. Nakushauri utembee kwa miguu ili uwe na nafasi nzuri ya kuipata nyumba unayoitafuta.”Dereva alimwambia.
“Sawa.”Zuki alijibu kwa ufupi huku akilipa kiasi walichokubaliana, akashuka kwenye gari na kumruhusu dereva aendelee na safari yake ili kujitafutia kipato kwa watu wengine. Aliendelea kusimama kando ya barabara hata baada ya gari kuondoka, alikuwa akikagua namba za nyumba zote zilizokuwa kando ya barabara iliyotumiwa na wakaazi wa mtaa huo, haikuwa barabara kubwa. Macho yake yaliendelea kuukagua mtaa huo wenye nyumba nzuri na za kisasa huku nyingi kati ya hizo zikiwa zimezungushiwa kuta ili kuficha yaendeleayo kwa wamiliki.
“Mtaa wa wazito bila shaka.” Aliwaza huku akijaribu kuufananisha huo mtaa na mtaa masaki, Dar es laam. Alivuka barabara na kuhamia upande ambao aliona nyumba zake zikiwa na namba alizohitaji, akachagua njia ya kawaida ambayo ilitumiwa na watembea kwa miguu kuzikfikia nyumba zao. Macho yake yakiwa makini aliendelea kukagua nyumba moja baada ya nyingine. Ukimya wa mtaa na wenyewe uliendelea kumfanya awe makini zaidi ili asije kushitukiwa na wenyeji. Haikumchukua muda mrefu kabla ya kuipata nyumba namba 607, aliitazama akiwa umbali mfupi na kuiona namna ilivyomezwa na ukuta mrefu uliokuwa umezungushiwa nyaya za umeme, kamera za ulinzi na zenyewe zikiwa zimefungwa kwenye nyaya hizo kwa namna ambayo ilionesha kila aliyekuwa akiikaribia nyumba ile alikuwa akionekana.
“Nani anaishi kwenye nyumba hii?” Alijiuliza huku akiipita kama vile hakuwa na habari na nyumba hiyo. Wakati alipokuwa akilipita geti la kuingilia ndipo alipogundua nyuma yake kulikuwa na mtu akimtazama kwa tuo, hakujali bali aliendelea na safari yake kama wapita njia wengine.
“Nyumba inalindwa kuanzia nje, bila shaka kuna ulinzi mkali zaidi huko ndani.” Aliwaza. Kwa mazingira aliyoyaona alibashiri kutakuwa na mtu mzito anaeishi ndani ya nyumba hiyo, mtu ambae si rahisi kuingilika. Alihitaji kumjua mtu huyo kabla giza halijakolea na sehemu pekee ya kuvuna taarifa za mmliki wa nyumba hiyo aliijua. Safari yake iliulenga mtaa wa Gagajuro, mtaa uliochangamka sana na ni mtaa ambao kila biashara hufanyika hasa biashara za magendo na uhalifu mwingine wa rejereja. Kwenye mitaa hiyo kulikuwa na mtu mmoja maarufu aliyefahamika kwa jina la Gachuma. Kwake kila kitu kilikuwa na thamani, iwe maneno ama bidhaa alichohitaji ni pesa. Taarifa za kila kona ya Entebe alikuwa anazijua na hata kama ungelitaji kinyesi cha mtu yeyote aliyeishi ndani ya Entebe ni lazima angelikuletea kwa gharama mliyokubaliana. Huyo ndiye Gachuma Itaro mzaliwa wa Bunazi, Bukoba na kulowea Uganda na maisha yake kwa asilimia kubwa yalitegemea pesa ya Kiganda. Mbali na kuwa mjanja wa mjini pia alikuwa ni mnyetishaji mzuri kwa askari polisi wa Entebe na maeneo ya jirani na kwa askari alikuwa hatozi fedha kuwapa taarifa bali alihakikishiwa usalama wa kazi zake haramu.
Siku hiyo Gachuma alikuwa kwenye moja ya ofisi yake iliyokuwa pembezoni kidogo ya mtaa wa Gagajuro, ofisi hiyo huitembelea kila siku inapofika kuanzia saa tatu usiku hadi saa nne na nusu, hukaa kwa saa moja na nusu pekee na kuondoka kuendelea na ziara kwenye ofisi zingine za aina ile. Ofisi yake hiyo ilikuwa maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji ambazo huuzwa kinyume cha sheria, mbali na hivyo pia ilikuwa ni sehemu ya kuwahifadhi wahamiaji haramu watokao sehemu mbalimbali ndani ya Afrika, wakati mwingine ilikuwa ni sehemu ya kuwahifadhi wahalifu sugu wanaotafutwa kwa udi na uvumba na serikali za nchi mbalimbali. Kitu kimoja ambacho wahalifu hao hawakujua ni kwamba, kuna nyakati Gachuma aliuza taarifa zao na mwisho hujikuta wakiangukia mikononi mwa polisi siku chache baada ya kutoka mafichoni. Gachuma kupitia biashara hiyo alijikuta akiingiza kiasi kikubwa cha pesa licha ya kiasi kingine kuwagawia polisi waliokuwa wakilinda uhalifu wake. Moja ya sifa kubwa aliyojenga kwa watu waliokuwa wakifanya kazi zake ni yeye kutokuwa nje ya muda, ikiwa alitakiwa kufika saa moja ni kweli hufika ndani ya muda huo. Kilichowachanganya wengi ni pale walipoona hakuwa na usafiri mwingine zaidi ya baiskeli yake ya kizamani chapa Avon ambayo aliifunga muziki mkubwa na urembo mwingine mithili ya msukuma wa Bariadi.
Miongoni mwa wateja waliokuwa wakinywa ulabu wa kienyeji alikuwa ni Zuki Gadu ambae wakati wote alikuwa makini kutazama mwenendo wa mshale wa saa yake. Alimfahamu vema sana Gachuma na aliifahamu ratiba yake ya matembezi. Saa tatu kamili muziki ulisikika hatua chache kutoka kwenye mabanda ya walevi, wimbo wa Saida Karoli, Maria Salome. Wimbo pendwa kwa Gachuma. Kila mtu alijua ni nani aliyekuwa anawasili, walevi waliomzoea walipiga kelele za shangwe kwa kuona unafuu wa pombe za bure umekaribia, ulikuwa ni utaratibu wake kuwanunulia pombe walevi wote kila alipofika hapo na waliruhusiwa kunywa wale ambao tayari wamelewa. Alifanya hivyo ili kuwakwepa wacheza na fursa. Uchangamfu ulikuwa ni moja ya sifa yake, aliizima radio yake na kuwasabahi watu wote waliokuwa hapo kisha akachukua kombe kubwa lililokuwa na mataputapu na kunywa funda moja kisha akarejesha kombe kwa waliokuwa wamenunua, akafurahi nao kisha akaelekea kwenye moja ya kijumba chakavu ambacho kilikuwa ni kama ofisi yake. Kijumba hicho ni yeye pekee alikuwa na funguo zake licha ya kwamba mlango wake hata kwa pigo moja ungeliweza kufunguka lakini ni nani wa kufanya hivyo? Nani asiyejitaka hadi awaze kuuvunja mlango wa ofisi ya Gachuma Itaro? Si walevi, si wageni wala wafanyakazi wake waliowaza kuhusu mlango wa ofisi hiyo iliyojengwa kwa udongo na kuezekwa kwa bati tatu pekee na zilitosha. Baada ya kuingia ofisini kwake aliwasha taa na kuanza kufuta vumbi la kiti kilichokuwa mle ndani, alipomaliza alikaa na kusubiri makusanyo ya siku nzima kutoka kwa wasaidizi wake waliokuwa wakifanya kazi kwa mgawanyo wa majukumu bila kuingiliana. Mfanyakazi wake wa kwanza aliingia akiwa na kibunda cha pesa zilizotokana na mauzo ya pombe, mfanyakazi wa pili nae aliingia baada ya mfanyakazi wa kwanza kutoka, huyu yeye alikuwa anahusika na taarifa za wahalifu waliojificha mashambani pamoja na wahamiaji haramu, mfanyakazi wa tatu aliingia na kibunda cha pesa za makusanyo ya pesa za waomba taarifa mbalimbali na mawasiliano yao. Mfanyakazi wa nne alikuwa na taarifa za usalama wa shamba lote. Kila mfanyakazi alikaa kwa wastani wa dakika kumi na sekunde kadhaa kabla ya kumuachia nafasi mwingine aonane na bosi wao.
 
Acha hizo wewe msichana,mimi nimenunua riwaya nyingi za huyu jamaa kwa mfumo wa kulipia halafu unatumiwa WhatsApp na hakujawahi kutokea utata
 
Acha hizo wewe msichana,mimi nimenunua riwaya nyingi za huyu jamaa kwa mfumo wa kulipia halafu unatumiwa WhatsApp na hakujawahi kutokea utata
Siwezi kukujibu maana siyo tabia zangu kujibu watu wenye ID nyingi kwa mtu mmoja
 
Gachuma baada ya wafanyakazi wake wote kuripoti kwake, alibaki peke yake na maburungutu ya fedha zilizopatikana kwa njia mbalimbali, alizihesabu kwa umakini ili kuzihakiki. Alipohakikisha hesabu ziko sawa alichukua kiswaswadu chake na kuzitafuta namba za afisa mmoja ambae kituo chake cha Polisi hakikuwa mbali na shamba, alitaka kumpa mgao wake ili aendelee na ratiba zingine. Wakati akiendelea kufanya mawasiliano macho yake yaliona mlango wake ukisukumwa na kisha mtu asiyemtarajia akasimama wima katikati ya mlango akiwa amemkazia macho. Alizubaa kidogo na asielewe kama alikuwa ndotoni au alikuwa kwenye uhalisia wake.
“Chu..Chu..chuma kingali moto!” Alisema kwa kukwamakwama huku akikata simu iliyokuwa imeunganishwa upande wa pili.
“Chuma hakiwashi moto.” Zuki alisema huku aliusukuma mlango nyuma yake na kuufunga, akapiga hatua na kusogea karibu na uso wa Gachuma.
“Unakumbukumbu kali sana. Imepita miaka mingi na bado unakumbuka utambulisho wetu.” Alisema na kuangusha tabasamu adimu kuonekana usoni mwake hasa awapo kwenye harakati zake zenye mashaka na uhai wake.
“Siwezi kusahau kamwe. Vipo vingi vya kusahau ila siyo harakati za Oparesheni Duma na namna tulivyoteseka mithili ya vikinda vya tai. Nakumbuka sana.” Gachuma alisema na kusimama kumpisha kiti mgeni wake ambae hajapata kuonana nae kwa zaidi ya miaka kumi na tano.
“Umewazeje kunifikia kirahisi namna hii?” Alimuuliza.
“Kwani siku hizi una ulinzi wa Al shabaab? Nitashindwa vipi kumfikia mwendesha baiskeli maarufu hapa Entebe? Hilo ni swali kweli? Halafu umesahau sisi ni wana wa Duma? Umesahau kwamba harufu ya duma waliokulia pamoja haiwatoki hadi kifo? Aah Gachuma!” Zuki alishangaa.
“Najua huna habari njema, nipashe nione namna ya kuzibeba habari zako.” Gachuma aliamua kufupisha maongezi kwa kuwa muda ulizidi kumtupa mkono na hakutaka kuchelewa aendako.
“Kweli Gachuma ni yuleyule wa jana na leo, hapotezi muda kizembe. Anyway, nahitaji taarifa za Plot nambari 607.” Zuki alisema kilichompeleka pale huku akiwa anahangaika kuisachi mifuko yake iliyohifadhi dola kadhaa.
“No! Wewe ni ndugu yangu wa mapito ya hekaya za kweli.” Gachuma alimzuia kuendelea na zoezi lake la kutaka kuzinunua taarifa.
“Unaongelea ule mtaa wa vigogo?” Aliuliza huku akifikiria kidogo, akarejesha macho yake kwa Zuki na kutikisa kichwa.
“Inawezekana nisiwe sahihi lakini hapo anaishi mtu mmoja anaitwa Daudi Nyuso. Huyo jamaa aliwahi kuwa mkuu wa jeshi la polisi hapa nchini, cheo ambacho hakukihudumu sana kabla ya kuondolewa kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake. Haikuishia kuvuliwa madaraka bali na jeshini aliondolewa kabisa. Kilichokuwa nyuma yake ni tuhuma za kushirikiana na waasi wa Uganda wanaopigana vita nchini Congo DR. Alikuwa akishirikiana na wanajeshi ambao hawakuwa waaminifu wa jeshi la Congo. Baada ya kuachishwa kazi aliendelea na maisha yake na biashara zake nyingi zinahusu madini. Sasa hivi anajiingiza taratibu kwenye siasa za Uganda na tayari kwa kutumia pesa zake ameanza kupata ushawishi na kiasi fulani ni mtu asiyegusika. Anaulinzi angalau unaelekea kukaribia wa makamu wa rais. Hafikiki kizembe.” Gachuma alitua.
“Unaweza kupata angalau ratiba zake za hivi karibuni?” Zuki aliuliza.
“Hakuna gumu lakini itabidi nipate angalau saa chache za kufuatilia. Mawasiliano yangu ya siri ni yale yale ya miaka nenda rudi, nistue ikifika saa saba ya usiku.” Gachuma alisema huku akimpa nafasi Zuki ya kuinuka kwenye kiti na kuondoka, hakutaka kuendelea kupoteza muda ikiwa ameshatoa taarifa ziliuliziwa. Zuki aliondoka kama mzimu shambani kwa Gachuma Itaro, Gachuma nae akaondoka kuendelea na ratiba zake akiwa na kazi moja ya kufanya kwa saa chache zilizosalia.
********
Wakati Zuki Gadu akihangaika na kupata taarifa za Daudi Nyuso, nchini Tanzania harakati nyingine zilikuwa zinaendelea kama kawaida. Montana alikuwa kwenye kazi aliyoachiwa na Zuki Gadu, kazi ambayo alitakiwa kuikamilisha ndani ya siku sita pekee na taarifa za awali alizopewa ziliishia kwenye namba ya pikipiki na hakukuwa na taarifa za ziada. Dar es laam ni jiji kubwa na lenye idadi kubwa ya watu, vyombo vingi vya Moto hivyo ni ngumu kuitafuta pikipiki moja na kuipata kirahisi. Kwa wengine ingelikuwa ngumu lakini kwa Montana ugumu unapungua kwa kiasi kikubwa, kwa nini? Kwa sababu ni mwanamke anaejuana na kila mtu anaetakiwa kumjua huku silaha yake kubwa ikiwa ni uzuri wake ambao huwachanganya watu wengi bila kujali hadhi zao. Nani alisema kichwa kidogo kikisimama hadhi ya mtu unazingatia? Thubutu yako, kila kizuri kilimezewa mate na kila mtu na hapo ndipo wenye mabavu ya madaraka na fedha hutumia madaraka yao kumega wavitakavyo. Montana alimegwa na kila mwenye pesa jijini Dar es laam, alimegwa na kila mwenye madaraka ili mradi aive kwa tamaa juu yake. Watu wengi hawakuwahi kujua sababu ya Montana kuugeuza uzuri wake kama chambo ya kumnasa amtakae na kingine ambacho hawakujua ni kwamba, hakuwa mwepesi wa kuvua nguo kwa kila aliyemtaka bali alikuwa hodari wa kuvuna taarifa kwa kila aliyeingia kwenye hamsini zake. Mbali na kufanya kazi na Zuki Gadu lakini mwanamke huyo alikuwa ni mtego wa kitengo nyeti sana nchini Tanzania na alifunzwa kwa sababu hiyo. Taarifa nzuri na mbaya za watu mashuhuri zilipitia kwake na kuchujwa kabla ya kufika dawatini. Kitu kimoja alichofundishwa na akafundishika ni kutokurejea alikoiba taarifa na kabla ya kuvua nguo alihakikisha anakufyonza kila alichotaka kusikia na endapo akipata kila kitu unaweza usione maumbile yake na ukaishia kujilaumu huku yeye akiwa mbali na uso wako, ukifanikiwa kumgusa utakavyo ina maana kuna kitu amekwama kukipata bila kukuonesha utupu wake na akikuonesha atakikisha anakufanyia yote ambayo si kahaba wala kungwi amewahi kuyafanya kitandani, baada ya hapo anakumega taratiibu na utampa atakacho kisha anatokomea na usijue alipoelekea. Licha ya utaalamu wake huo uliogharimu pesa nyingi wakati wa mafunzo yake, lakini hakuwahi kuvuna chochote kutoka kwa Zuki Gadu na badala yake alijikuta akitumika yeye kuvuna taarifa alizohitaji Zuki. Alifanya kila jihadi kuhakikisha anajua njia zote za Zuki lakini aliambulia patupu na akaishia kuisubiri siku ambayo hajui itatokea lini ili amjue vema mtu huyo ambae kumuona huwa ni kama kumuona Kakakuona, itokee bahati tu. Montana alikuwa na mitego yake kwa Zuki lakini kitu kimoja ambacho hakujua ni kwamba, Zuki alishazihesabu hatua zake siku nyingi sana na alijua uhatari wa kuweka ukaribu nae, hiyo ni moja ya sababu iliyomfanya Zuki awe anajitokeza kwake mara chache sana na hujitokeza awapo na ishu ya maana ambayo ni lazima Montana ahusike na baada ya hapo hupotea kama vile hakuwahi kuonana nae maisha yake yote. Montana alitaka uaminifu kwa Zuki hivyo kila kazi aliyokuwa akiifanya alikuwa anataka kuwa karibu zaidi yake na aliifanya kwa juhudi kubwa. Baada ya kupewa namba za pikipiki hakulaza damu, alimtembelea kwa kushitukiza mtu wake wa zamani ambae alikuwa ni kigogo mmoja ndani ya ofisi za TRA. Aliyetembelewa aliona ni bahati ya mtende kuota jangwani, kupita muda mrefu bila kumuona Montana kisha ghafla tu anajitokeza akiwa na uzuri ulioongezeka maradufu, hiyo ilikuwa ni bahati ambayo hajawahi kuiota. Kutokea kwa Montana kulisimamisha kazi za kibosile kwa dakika kadhaa, walipiga soga nyingi hadi pale kibosilea aliponasa kwenye mtego, akaombwa kuitambua pikipiki hiyo ambayo ilisadikika mmiliki alihusika kumwibia Montana. Kibosile akafanya alichoombwa na ndani ya muda mfupi jina la mmiliki wa pikipiki likapatikana, makazi yake nayo yakapatikana. Montana alipopata alichotaka akaaga, akasindikizwa na noti nyingi za elfu kumi huku yeye akiacha namba ambayo aliizima dakika tatu baada ya kutoka ofisini. Malima Bilali lilikuwa jina la kwanza kukaa kichwani mwake punde alipoziacha ofisi za mamlaka ya mapato. Kwa taarifa za haraka haraka alitambua jamaa alikuwa ni mmliki wa kituo cha kuoshea magari maeneo ya Mkwajuni, Kinondoni.
Saa tatu baadae gari aina ya Toyota Crown ilikuwa inaingia kwenye maegesho ya kituo cha kuoshea magari kilichokuwa Mkwajuni. Kabla hata gari haijasimama tayari vijana wawili walikuwa wameizunguka wakiomba kumsikiliza mteja wao. Gari ikazimwa na aliyekuwa ndani ya gari hakushuka wala kushusha vioo kuwasikiliza wenyeji wake, alitulia kwa zaidi ya dakika tatu akiwa anayasoma mazingira ya eneo lile,mbali na wale vijana wawili waliokuwa wakigombea kutoa huduma, kulikuwa na mabarobaro wengine watatu ambao walikuwa wameliegemea gari moja huku wakionekana kuwa katikati ya kikao cha kusimuliana yaliyokuwa yakiendelea mjini. Kwa namna walivyokuwa wanajiamiani kusimama eneo walilokuwepo moja kwa moja alihisi watakuwa wanahusika na kituo kile. Akashuka kuijaribu bahati yake. Montana alikuwa kwenye vazi fupi lililoacha maungo yake wazi, nywele zake ndefu aliziachia ziufunike mgongo wake, macho yake aliyafunika kwa miwani ya bei kubwa na mwilini alipulizia uturi wa bei ghari. Kwa namna alivyoshuka aliacha watu wote na mshangao wa sekunde kadhaa, nae akaamua kuwamaliza kabisa kwa kuzungusha kichwa chake na kuzifanya nywele zake nyeusi zitawanyike huku na huko kwa namna ya kuvutia.
“Mtatumia muda gani kulisafisha gari langu?” Aliwauliza vijana waliokuwa kando ya gari lake.
“aah..ahh.. dakika ishirini tu..” Mmoja alijibu kwa mashaka kama vile hakuwa na uhakika na kile alichokuwa amekijibu, lakini kigugumizi chake ni kwa sababu ya kiumbe aliyekuwa mbele yake, alimtamani lakini alijiua hataweza kumpata hata kwa dawa. Hadhi yake hakuona kama inaendana hadhi ya mwanamke aliyekuwa akitazamana nae. Si vijana hao pekee waliokuwa wakijitenga na daraja la mwanamke aliyekuwa mbele yao, hata wale vijana wengine waliokuwa bize na maongezi walikuwa wameacha kila walichokuwa wanafanya, macho yao yakahamia kwa malaika mweusi aliyekuwa mbele yao, walikuwa wakijipima daraja lao kwa kiumbe aliyependelewa na Mungu uzuri wa ajabu na siyo uzuri tu, hata nyota alikuwa ya kupendwa alikuwa nayo.
Wakati gari ikiendelea kuhudumiwa, Montana aliomba kukaa kando ili asubiri gari lake, hiyo ikawa nafasi nzuri kwa vijana wakware kupanga vema karata zao na hatimae wakaamua kumwacha mmoja kati yao ajaribu bahati yake huku wengine wakisubiri kuona kama watapata ushemeji au watatoswa. Vijana waliosalia waliamua kumuacha mwenzao Kwa sababu waliamini anafaa kuhangaika na binti mzuri na aliyeonekana kuwa na kipato, walimsusia kwa sababu alikuwa na kipato kikubwa kuliko wao. Aliyesusiwa alikuwa ni Malima Bilali.
Montana alizihesabu vema hatua za kijana mjivuni mwenye kuonekana kuwa na pesa za kurungishia warembo, alitembea kwa kujiamini na mikogo ya hapa na pale. Alitabasamu kwa kuwa alijua ni kitu gani kingelifuata kwenye maongezi yao.
“Habari yako mrembo..” Jamaa alisabahi.
“Nzuri.” Montana alijibu kwa ufupi na kuendelea na kuperuzi kwenye simu yake.
“Naitwa Bilali ni mmiliki wa hiki kituo cha kuoshea magari.” Alijitambulisha.
“Ahsante kwa kunifahamisha.”Montana alijibu na kuinua uso wake kumtazama Malima, aligundua jambo ambalo alishalitilia shaka tangu alipoisikia lafudhi ya Malima. Uso wa Malima ulikuwa na matokeo ya utumiaji wa vipodozi vikali, lafudhi yake pia haikuwa ya Mtanzania halisi wala jamii ya jina alilojiita. Malima hutoka ukanda wa kanda ya ziwa hasa mkoani Mara kwenye jamii za wavuvi pamoja na visiwa vya Ukerewe. Bilali pia halikuwa jina la ukanda huo bali ni jina linalotumiwa na watu wenye asili ya bara Hindi ni nadra majina yenye asili mbili kuchangamana ijapokuwa inawezekana. Lakini ni ngumu zaidi mtu anaeonekana kuwa na asili ya nchi ya Congo kuwa na vinasaba na jina la Malima na ubini wa Bilali kisha akawa anaejichubua. Hilo lilimtia shaka Montana na likamfanya avutiwe zaidi na kutaka kumjua Malima ni nani.
“Gari inaweza kuchukua muda mrefu kuoshwa, hapa hapakufai kusubiri.” Jamaa alisema kwa mikogo huku akiligeukia eneo la jirani ambalo lilitunza mgahawa na watu wachache walikaa wakiburudika na mlo.
“Naomba tukae pale angalau upate maji wakati gari lako likiendelea kuhudumiwa, ahsante kwa kuchagua ofisi yangu.” Malima alisema.
Montana hakutaka kuongeza neno kwa sababu moja ya silaha yake kubwa ya kumsoma mtu ni kumpotezea wakati akibwabwaja, alitaka amuelewe vema mtu huyo na tabia zake. Aliinuka bila kusema lolote kisha akaanza kupiga hatua kuelekea mgahawani, nyuma yake alifuata Malima ambae aliwageukia wenzake na kuwanyooshea alama ya dole la ushindi kwa kumuinua mwanamke mrembo.
“Agiza chochote nitalipa.” Malima alisema baada ya kufika mgahawani.
“Niitakunywa maji tu.” Montana alijibu na kuendelea kuperuzi simu.
“Ningependa kulijua jina lako mrembo.” Malima alianza kurusha ndoano bila kujua alishatupiwa yeye na alikaribia kunasa.
“Naitwa Marry Mariam.” Montana alidanganya.
“Kwa hiyo nikuite Marry au Mariamu?” Aliulizwa.
“Niite hivyohivyo, Marry Mariam.” Alisema na kuiweka simu kwenye mkoba, akamtazama kwa macho malegevu yaliyoenda kuvuruga mfumo wa akili wa mtazamwaji. Baada ya macho yaho kutua kwenye fikra za Malima, kilichofuata ni raha za muda mfupi na karaha ya muda mrefu. Lakini nani angelijua yajayo? Ninge hubaki kauli ya kila kiumbe hai mwenye kauli na hutamkwa yakishatokea. Ninge ni kauli ya majuto. Nani alijuta kati yao? Mi sijui.
 
3.
Zuki Gadu alirejea kwenye hoteli aliyofika ikiwa ni saa sita na dakika kadhaa usiku. Aliingia chumbani kwake kwa tahadhari kwa kuwa hakutaka kujiamini ikiwa alikuwa kwenye mawindo na asingelishangaa hata yeye akiwa anawindwa. Alikikagua chumba chake kwa umakini mkubwa hadi alipojihakikishia hakukuwa na tatizo lolote. Akaingia bafuni na kujimwagia maji kisha akahakikisha amelala akiwa amevaa nguo zake na viatu, hakujiamini na alitaka lolote likitokea limkute akiwa kamili bila kujisumbua kuhangaika na jambo lingine ambalo lingilimpotezea muda wake. Kabla ya kulala alitaka alitaka kuruhusu kiyoyozi kipooze joto la kiangazi, lakini ilishindikana na ni kama mfumo ulikuwa na hitilafu.
“Lakini mchana kulikuwa shwari.” Aliwaza huku akipuuza na kwenda kujitupa kitandani na kuanza kuutafuta usingizi huku akiwa amesahau kutuma ujumbe kwa Gachuma kama walivyokuwa wamekubaliana. Akapitia na usingizi haraka zaidi kuliko alivyokuwa amedhania, ni kama usingizi uliomsomba haukutoka kwenye utimamu wa mwili wake, kulikuwa na msukumo wa lazima uliomlazimisha kulala fofofo. Licha ya kulala usingizi mzito lakini haikumchukua saa moja kuamka, aliamka huku akihisi akili inauzito ambao hajawahi kuupata, mwili nao ulikuwa mzito kiasi kwamba alishindwa kugeuka kirahisi. Wakati akiwa bado anajiuliza ni kitu gani kilichomkuta, akahisi mwili wake ni wa baridi sana na akiwa bado anajiuliza kuhusu ubaridi huo, masikio yake yalinasa sauti ya mvumo uliotoka kwenye kiyoyozi.
“Kimejitengeneza chenyewe?” Alijiuliza huku akijaribu kuinuka lakini mwili ulikuwa mzito kupindukia na hapo aligundua hakuwa kwenye hali ya kawaida, wakati huohuo pua zake zilianza kunusa harufu nzuri ambayo hakuwa mgeni wa harufu ya aina ile.
“Dadeki!” Alijisemea huku akipambana kuziba pua zake ili kukwepa harufu ambayo aliamini inatoka na hewa ya kiyoyozi, harufu ambayo kama angeliivuta kwa kiasi kikubwa ingelimsababishia uchovu wa kila kiungo chake. Wakati huo alikuwa akijaribu kuinuka kitandani, ijapokuwa mwili wake ulikuwa mzito lakini bado alipambana na kufanikiwa kusimama, mkono mmoja ukiwa umeziba pua zake na mkono mwingine akihangaika kupapasa chochote ambacho kungelikuwa karibu kisimkwamishe kuufikia mlango.
“Nimenasa kizembe sana.” Aliwaza huku akiendelea kuusogelea mlango, lakini kabla hajaufikia masikio yake yalinasa sauti ya mkimbio ww kiumbe hai hatua moja nyuma yake.
“Ooh shiiit! Ameingiaje humu? Ameingia saa ngapi?” Alijiuliza huku akiachia pua zake na kushusha pumzi nyingi ili kuruhusu mapafu yake yaweze kupunguza mrundikano wa hewa aliyoizuia kwa zaidi ya dakika moja, akageuka taratibu huku akiwa ameuandaa mwili wake kukabiliana na lolote kutoka kwa adui aliyekuwa nyuma yake. Macho yake yaliyoanza kuwa mazito yalimuona kiumbe aliyevaa nguo maalumu za kuzuia hewa chafu akiwa amesimama wima na kipande cha fimbo mkononi mwake.
“Mjinga amenichezea kizembe...” Zuki aliwaza huku akiwa makini kuhakikisha haingii mikononi mwa mtu ambae hakuonekana kuwa wema wowote kwake.
“We..we.. ni na ni?” Alipambana kupaza sauti yake lakini haikutoka kama alivyotarajia ijapokuwa aliyemkusudia alisikia.
“Mimi ni kifo chako...” Jamaa alijibu huku akijiandaa kutumia fimbo yake kumuadhibu Zuki. Kitendo hicho kilionwa vema na Miguu ya kuku ambae hakutaka kufa kizembe wala hakutaka kupoteza pambano lingine akiwa nje ya nchi yake, lile pambano alilopoteza akiwa hatua chache kufika nyumbani kwake bado lilizitesa fikra zake na hakuwa tayari kuona anadhalilika tena, lakini angelifanya nini ikiwa akili inataka na mwili hautaki? Kila kiungo chake kilikuwa kizito kufanya kile alichotaka kufanya, macho yake nayo yalikuwa yameanza kuusaliti uoni thabiti. Licha ya yote lakini alifanikiwa kulikwepa pigo la kwanza la mtu aliyekuwa mbele yake, akajiweka mbali kidogo huku hesabu zake akizipeleka haraka ili angalau afanikiwe kumdhibiti adui yake. Umbali aliojiweka alimsaidia kupiga hatua tatu mbele kisha akajiachia mzimazima na kumkumba adui yake ambae nae alikuwa anajiandaa kutupia pigo alilodhani lisisingewezakanika kukwepwa. Wote wawili wakapiga mweleka chini lakini madhara yakawa kwa mvamizi ambae alitanguliza mgongo chini. Zuki Gadu hakutaka adui yake apate nguvu, haraka akawahi kuinuka na kumlalia juu yake kwa lengo la kumshushia makonde kadhaa lakini nguvu za mwili zilimsaliti, ila haikuwa sababu ya yeye kushindwa kufanya jambo ambalo lingempa heshima ya pambano ambalo hata mwenyewe hakuwa na uhakika kama atashinda, kwa nguvu zake zote alizosalia nazo mwilini mwake, akakita meno shingoni mwa adui yake na kung’ata kwa nguvu kisha akavuta sehemu iliyoingia meno na kunyofoa nyama na kuitema. Damu nyingi zilimfikia usoni, kelele nyingi zilipigwa na adui yake ambae alikuwa anajaribu kukuruka mithili ya kuku aliyekatwa shingo na kuachwa. Wakati akihisi ameshauchukua ushindi ili atoke nje kabla ya ile hewa ya kiyoyozi haijamzimisha kabisa, alishangaa akiinuliwa kwa nguvu na mtu aliyekuwa amesimama nyuma yake, akatupwa chini kwa kishindo na kuiashia kupiga ukelele wa maumivu na hamaniko, alipotaka kuinuka ili apambane tena na mtu huyo ambae alioneka kuwa jabari la miraba minne, nguvu za mwili wake zilimsaliti, kila kiungo cha mwili wake kilikuwa dhaifu na pumzi nazo alianza kuzivuta kwa taabu kubwa. Hakutaka kufa kizembe, alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake na kusimama huku akipepesuka mithili ya mlevi wa chibuku, lakini hata kumuona aliyekuwa mbele yake ikawa taabu, giza la chumbani lilizidi mara dufu na hata ule mwanga uliokuwa ukitokea dirishani nao haukuweza kupepesua mboni zake. Wakati huohuo alishangaa akipaa juu huku maumivu makali yakisambaa kuanzia kidevuni na kuelekea sehemu zingine za kichwa chake, alikuwa amepigwa ngumi ya chembe kidevu na alikubali kukaa. Pigo lingine lililofuatia lilitua vema upande wa sikio lake la kushoto, kwa pigo lile kila kitu kikazima kwenye mfumo wake wa fahamu, hakusikia wala kuona chochote. Zuki Gadu kwa mara nyingine alipoteza pambano kirahisi kuliko alivyodhania na alipoteza kwa mara ya pili kwa tofauti ya siku moja pekee. Je, Zuki kazeeka kiasi cha kushindwa kutambua hatari? Zuki kazidiwa uwezo wa kupambana kwenye hali ngumu au Zuki kawaje? Sijui! Sijui!.
 
Kwa kipande kimoja kimoja hivi tutafika kweli hata kwenye hamasa ya kuhamia whatsapp hivi karibuni kweli?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom