Habari wanajamvi,
Kutokana na hali ya uwepo wa watoto wengi wa nje ya ndoa hivi karibuni, nimeona niulize maswali yafuatayo humu jamvini ili tupate maoni, ushauri na uzoefu juu ya suala hili.
Kutokana na hali ya uwepo wa watoto wengi wa nje ya ndoa hivi karibuni, nimeona niulize maswali yafuatayo humu jamvini ili tupate maoni, ushauri na uzoefu juu ya suala hili.
- Je, ni busara kwa mtu kuoa au kuolewa na mtu aliyezaa na mtu mwingine?
- Je, ukioa au kuolewa naye mawasiliano ya hao wazazi juu ya mtoto wao yanatakiwa kuwaje?
- Je, ni sahihi mtoto kuchukuliwa ili akalelewe na baba/mama wa kambo?
- Kama atachukuliwa kulelewa na baba/mama wa kambo, je mama/baba mtoto aruhusiwe kuja kumuona mtoto?
- Na vipi mwezi ambaye anakuja kuzaa nje baada ya ndoa kufungwa? Je mtoto aletwe na kulelewa na watoto wengine au aachwe kwa huyo hawara?
- Je, kama mwenzi amezaa nje ya ndoa kuna haja ya kuendelea kufanya mipango ya maendeleo pamoja au ni bora kila mtu ajijenge ki mpango wake?
- Ni mazingira yapi mazuri yatawezesha ndoa iendelee kustawi ili hali kuna mtoto wa nje ya ndoa?