HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,569
Mzinga wa nyuki ni hatari sana!
Miezi minne iliyopita nilichokonoa mzinga wa nyuki,kilichotokea ni nyuki mmoja dume aliyeshiba akanidunga mwiba wake halafu akatema sumu ..kilichotokea ni maumivu kiasi na uvimbe ambao unakua taratibu.nimeuliza kwa wataalamu wameniambia uvimbe utaendelea kukua mpaka wiki 40,waswahili wanasema miezi tisa!
Napata kichefuchefu hasa wakati wa asubuhi,
chonde chonde,mwenzenu nimekoma kuchezea mzinga wa nyuki!
Nimejikuta najiuuliza KIPUUZI ...
Ulidungwa kwa matakwa yako au kwa kulazimishwa? Kwa nini wakati anakudunga mwiba hukutumia kinga? Au ulipenda mwenyewe kuvimba? Una uhakika sumu aliyoacha ni moja tu ya kukusababishia uvimbe tumbo kwa miezi 9 na hakuacha ile ya kukusababishia uanze kutumia ARVs? Je, hili ni jambo ambalo umelifurahia na kutaka kutupa taarifa au limekuhuzunisha na unatoa tahadhali kwa wengine kuwa makini na kuchezea mizinga ya nyuki?