Mwenzenu nifanyeje!??

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,329
23,873
Mpenzi wangu wa moyo, uzurio nauenzi,
nachunguza wangu moyo, nipate japo utenzi,
niseme bila uchoyo, jinsi gani nafa ganzi,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Si kwa umbo wala sura, uzurio wavutia,
kwa lugha iso na zira, kiswahili natumia,
kuonesha pasi hijra, jinsi gani mekufia,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Pendo la kweli hungoja, ulisema wewe hani,
nami ni tayari ngoja, kukuweka wewe ndani,
tena bila ya vioja, tueleke kanisani,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Naahidi kuwa nawe, milimani na bondeni,
furahani niwe nawe, nikupende na shidani,
Mola pia awe nawe, sikuachi asilani,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Penzi langu sibadili, kwani moyo tauchoma,
shikilia kwa manjali, pwani tutafika mama,
nakupenda kama wali, sivunje wangu mtima,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Sipendi kusema mengi, na kupiga tararira,
kwa beti ziso nyingi, nimemaliza ziara,
kwa vazi la udhurungi, ninajitoa kafara,
Nami naomba uliza, "WILL YOU MARRY ME?"
 
Is this for Jukwaa la lugha, na si kwamba unaumizwa moyoni na huyu naniliu?...Sema usaidiwe kaka..! --By ze way, this is GOOD FOR NEW LOVERS!....Its almost a decade since i exchanged the vows with my sweetheart, and since then, the taste hasnt changed!...Love, sweet love!
 
Mpenzi wangu wa moyo, uzurio nauenzi,
nachunguza wangu moyo, nipate japo utenzi,
niseme bila uchoyo, jinsi gani nafa ganzi,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Si kwa umbo wala sura, uzurio wavutia,
kwa lugha iso na zira, kiswahili natumia,
kuonesha pasi hijra, jinsi gani mekufia,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Pendo la kweli hungoja, ulisema wewe hani,
nami ni tayari ngoja, kukuweka wewe ndani,
tena bila ya vioja, tueleke kanisani,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Naahidi kuwa nawe, milimani na bondeni,
furahani niwe nawe, nikupende na shidani,
Mola pia awe nawe, sikuachi asilani,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Penzi langu sibadili, kwani moyo tauchoma,
shikilia kwa manjali, pwani tutafika mama,
nakupenda kama wali, sivunje wangu mtima,
kutoka ndani ya moyo, nakupenda ua ridi.

Sipendi kusema mengi, na kupiga tararira,
kwa beti ziso nyingi, nimemaliza ziara,
kwa vazi la udhurungi, ninajitoa kafara,
Nami naomba uliza, "WILL YOU MARRY ME?"

hongera ebby asili, kwa kuionja asali
naliona penzi kweli, kama hutolibadili
na ulile kiukweli, ikiwa na huyo mwali
sasa hilo la ndoa, huoni hiyo papara?

huoni hiyo papara, hasa hilo la ndoa?
umeshapita mabara, ndipo ukaopoa?
umeshakuja na bara, uone tulivyo poa?
haya nakuachia, kusuka au kunyoa

....itaendelea
 
Wandugu nisameheni, taaluma linishinda,
binti kweli nampenda, kubadili menishinda,
nyuma siwezi kwenda, msaada sitopenda,
nilitaka edit title, ikabaki mejikita!

Kwa kifupi nataraji, ujumbe umemfika,
kwangu yeye kama maji, sipokunywa nitapika,
wajua nakuhitaji, kila saa na dakika,
nilitaka edit title, ikabaki mejikita!

Pakajimy nakwambia, penzi langu kwake kweli,
majungu tanitupia, sitomfanya wa pili,
utamuwe twaujua, japo miaka miwili,
nilitaka edit title, ikabaki mejikita!

MTM shukurani, kweli umenielewa,
kwani we ulitakani, muda binti kumuowa,
kusubiri siwezani, ni afadhali kunyowa,
meenda kote barani, jaona mwingine poa!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom