josephdeo
Member
- Nov 23, 2015
- 96
- 208
Mtoko wa chakula cha usiku ambacho nilikuwa na wiki mbili nimeuomba kutoka kwa Brenda ulikuwa umekubaliwa. Tulikuwa kwenye moja ya mgahawa katikati ya jiji la Mwanza. Tuliagiza chakula na kula kwanza hii ilikuwa kanuni niliyokuwa nimesoma kwenye moja ya majalida ya mahusiano. Kanuni hiyo ilielezea kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kukubaliwa maombi yako kwa mwanamke ikiwa tu atakuwa kashiba.
Tulipomaliza kula chakula kile cha usiku majira ya saa nne. Nikaomba usikivu wa mwanamke aliyekuwa mbele ya macho yangu. Aliponipatia kile nilichokiomba nami nikaanza kuongea. Maneno haya huyakumbuka hata sasa na sidhani kama nitaweza kusahau kwa sababu pia yeye uniambia nilitumia njia bora zaidi kumtongoza.
Nilimtizama kwa mda kiasi kisha nikamwambia. "Mimi ni mzuri lakini sio malaika, pia ninayo mabaya yangu lakini kamwe sijawahi kuwa shetani. Bali kijana mdogo kwenye dunia kubwa iliyojawa na mengi ila kati ya yote ninajiona mapenzini kwako". Nikavuta pumzi za wastani huku woga uliokuwa ukinitafuana awali ukiniondoka.
"Mara kadhaa nimepata wasaa wa kutazama sura yako kwa ukaribu zaidi. Kama nifanyavyo hivi sasa... Hatua chache toka ulipo hiyo imenipa wasaa wa kuutazama uzuri wako nikiwa karibu. Sio mtaalamu katika kuyaeleza maneno yanayo husisha mapenzi. Ila leo nimeona ni busara zaidi kukueleza haya. Inanilazimu kukueleza kwa kuwa kutokukueleza ni kutotumia haki yangu ya kimsingi pia nitakuwa nimejikosea sana. Kwani hatujui nini kinakuja mbele yetu baadae". Nikacheka kicheko hafifu kisha nikamwambia. "Nadhani unaona hali tunayokutana nayo kila iitwapo leo". Naye akatabasamu..jambo ambalo nikanipa moyo kuendelea kuyasema niliyoyakusudia.
"Japo sijawa na wasaa mzuri katika mapenzi hiyo aijaniondolea hamu ya kupenda kama mwanaume. Leo nimeona ni busara kukueleza haya ambayo toka mara ya kwanza nakuona nikiwa hoi kitandani nilitamani kukueleza. Nilikuwa sifahamu ni nini nahijati kwa mwanamke mpaka pale macho yangu yalipo hifadhi kumbukumbu hizo kichwani mwangu. Toka hapo nimekuwa nikipata msukumo ndani yangu. Ya kuwa wewe ndie aina ya mwanamke ninaye kuhitaji. Sidhani kama unajisikia namna kama mimi ninavyo jihisi. Lakini tunaweza kujihisi hivi wote ikiwa tu utaruhusu nikupende na kunikabidhi majukumu ya kuuhifadhi moyo wako".
"Sielewi nini maana ya mapenzi ila moyo wangu una hisia nzito za mapenzi dhidi yako. Nakupenda sana Brenda na nakupenda kimapenzi. Nahitaji uwe mpenzi wangu na mama wa wanangu kama tukijaaliwa. Ninatumaini kuzifunga breki zangu kwako. Kwani kila nikikutazama najiona nikiwa mme huku wewe ukiwa mke. Sio mkamilifu au mtiifu ila angalau naweza kuwa bora nikiwa kando yako". Haiba za kike zikamvagaa na akaangalia chini. Hii ilikuwa mara ya kwanza kuliona jambo hili likitokea kwa Brenda kushindwa kunitazama uso kwa uso angalau kwa sekunde tatu tu.
Nikaendela. "Safari yangu ya kimahusiano ya kimapenzi ifungwe nawe. Tuwe pamoja mpaka kiama. Nipe jukumu la kukusimamia kama mme nami nikupe jukumu la kunilea kama mke. Sitamani kuongea mengi ila nachukia kunyamaza hii inasababishwa na mengi niliyonayo ambayo nahitaji uyasikie. Napenda nisimame upande wako kwa nyakati za furaha na huzuni, napenda niwe kwenye nyakati zote za maisha yako yaliyobaki hapa ulimwenguni. Napenda kuendelea kuongea yale yaliyojificha ndani ya kifua changu. Ambayo wakati wote yalikuwa siri kuu kwangu lakini natamani kusikia neno lolote kutoka kwako pia". Ukimya ukawepo kidogo ambao waswahili usema ukimya wa kumpisha shetani.
Lakini kabla ya kufungua kinywa chake kuzungumza nikamkatisha kwa kumwambia. "Natamani kukusikia ukisema lolote ila kabla ya hilo nakuomba pia. Tafadhali usiseme lolote ambalo litafanya nijihisi sina thamani katika ulimwengu huu. Nakuomba sana hili na hata magoti nitapiga mbele yako ili kuonesha ni kiasi gani nakuomba jambo hili. Kwani siwezi kuhimili kukukosa na sifahamu itakuwaje ikiwa hauta kuwa wangu wa maisha. Unaweza kusema kuwa mpo wengi na nitampata mwingine. Lakini kati ya wengi hao wewe pekee ndio jicho langu limekuona. Wewe pekee ndio moyo wangu umekuchagua. Wewe pekee ndio akali yangu inakuwaza. Najiona nikiwa bora zaidi pale ambapo utakubali kuungana na mimi katika safari hii ya mapendo ambayo leo nataka tuianzishe. Nakuomba uniruhusu nikupende". Nikanyamaza sasa kumsubiri kuniambia chochote kati ya yote niliyoyasema.
"Tunaweza kurudi base". Hili ndilo lilikuwa jibu lake ambalo sio tu nilijihisi kudharauliwa bali nilijiondolea thamani yangu kama binadamu.
Ila nikajikaza tu kama mwanaume huku nikiuambia moyo ufanye shughuli uliyopewa ya kusukuma damu. "Ndio tunaweza kurudi". Nilijibu.
Vipi tuendelee au tukaushe...