Nakuomba uniruhusu nikupende

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Mara kadhaa nimepata wasaa wa kutazama sura yako kwa ukaribu zaidi. Hatua chache toka ulipo hiyo imenipa wasaa wa kuutazama uziri wako nikiwa karibu.

Sio mtaalamu katika kuyaeleza maneno yanayo husisha mapenzi. Ila leo nimeona ni busara zaidi kukueleza haya. Inanilazimu kukueleza kwa kuwa kutokukueleza ni kutotumia haki yangu ya kimsingi pia nitakuwa nimejikosea sana. Kwani hatujui nini kinakuja mbele yetu baadae.

Japo sijawa na wasaa mzuri katika mapenzi hiyo aijaniondolea hamu ya kupenda kama mwanaume. Leo nimeona ni busara kukueleza haya ambayo toka mara ya kwanza nakuona pale nilitamani kukueleza. Sielewi nini maana ya mapenzi ila moyo wangu una hisia nzito za mapenzi dhidi yako. Nakupenda sana Brenda na nakupenda kimapenzi. Nahitaji uwe mpenzi wangu na mama wa wanangu kama tukijaaliwa.

Kwa mda sasa nimekuwa nikiubeba mzigo huu wa kukwambia haya moyoni mwangu. Sasa mzigo huu umekuwa mkubwa kiasi unanishinda kuhimili na kuamua nikwambie.

Safari yangu ya kimahusiano ya kimapenzi ifungwe nawe. Tuwe pamoja mpaka kiama. Nipe jukumu la kukusimamia kama mme nami nikupe jukumu la kunilea kama mke. Sitamani kuongea mengi ila nachukia kunyamaza hii inasababishwa na mengi niliyonayo ambayo nahitaji uyasikie.

Sio mzuri katika kujielezea ila yote yanitokayo kinywani mwangu ni kweli. Brenda naweza nisiwe mwanaume unayemhitaji kwani nawe una machaguo ila naweza kuwa mwanaume wa ndoto yako. Maneno haya hayatakuwa tupu tu bali nipe nafasi ili niyathibitishe.

Napenda nisimame upande wako kwa nyakati za furaha na huzuni, napenda niwe kwenye nyakati zote za maisha yako yaliyobaki hapa ulimwenguni. Napenda kuendelea kuongea yale yaliyojificha ndani ya kifua changu. Ambayo wakati wote yalikuwa siri kuu kwangu lakini natamani kusikia neno lolote kutoka kwako pia.

Natamani kukusikia ukisema lolote ila kabla ya hilo nakuomba pia. Tafadhali usiseme lolote ambalo litafanya nijihisi sina thamani katika ulimwengu huu. Nakuomba sana hili na hata magoti nitapiga mbele yako ili kuonesha ni kiasi gani nakuomba jambo hili. Kwani siwezi kuhimili kukukosa na sifahamu itakuwaje ikiwa hauta kuwa wangu wa maisha.

Unaweza kusema kuwa mpo wengi na nitampata mwingine. Lakini kati ya wengi hao wewe pekee ndio jicho langu limekuona. Wewe pekee ndio moyo wangu umekuchagua. Wewe pekee ndio akali yangu inakuwaza. Najiona nikiwa bora zaidi pale ambapo utakubali kuungana na mimi katika safari hii ya mapendo ambayo leo nataka tuianzishe. Nakuomba uniruhusu nikupende
 
FB_IMG_16466379533385663.jpg
 
Shida inaanzia baada ya kuchovya mara mbili tatu, hayo maneno unayaona hayana maana tena kwa Brenda.

Unamtafuta mwingine halafu unamwambia maneno hayohayo uliyomwambia brenda.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom