Mwenza Kupotea kwa Miaka 5 Kunatosha Kuvunja Ndoa?

Mwenza Kupotea kwa Miaka 5 Kunatosha Kuvunja Ndoa?

RALC255

New Member
Joined
May 11, 2025
Posts
4
Reaction score
4
EDECA1FC-E4F9-4F6A-9A1A-4D6206D4FBE4.png

Presumption of Death katika Sheria ya Ndoa na Mirathi
➡️ Je, mtu anapotea bila mawasiliano kwa miaka mitano mfululizo… je, bado ni mume/mke wako halali?
➡️ Je, bado atahesabika yupo hai? unaweza kufungua mirathi bila cheti cha kifo chake?
➡️ Au kuolewa tena bila talaka?

Hili si swali la kufikirika pekee. Ni tatizo halisi linalowakumba watu wengi nchini, hasa wake au waume waliotelekezwa kwa ukimya bila talaka, bila maelezo, bila msiba. Sheria ya Tanzania inalizungumzia vipi jambo hili?

🔍 Presumption of Death: Nini Maana Yake?
Presumption of death ni tamko la kisheria linalomruhusu mtu kutangazwa kuwa amefariki ikiwa hajasikika kabisa kwa miaka mitano mfululizo, na hakuna aliye na mawasiliano naye ambaye angetarajiwa kuwa nayo kama angekuwa hai.

Sheria inayotumika ni:
Kifungu cha 161(1) cha Sheria ya Ndoa (Law of Marriage Act, Cap 29 RE 2019)
A person shall be presumed dead if he has not been heard of for a period of five years by those who might be expected to have heard of him if he were alive.”

Kwa kifupi, kimya cha miaka 5 kinaweza kuwa kifo cha kisheria.

🧾 Kesi ya Msingi (Temeke, 2022): Salum Omary Hamad
Katika kesi ya Misc. Civil Application No. 36 of 2022, Mahakama Kuu Temeke ilimsikiliza Fatma Kitwana Ally ambaye mume wake alipotea mwaka 2017, hakusikika tena, na hakuacha ujumbe. Aliishi naye kwa ndoa halali na walikuwa na watoto wanne.

Alitaka kutangazwa kuwa mume wake amefariki ili aweze kufungua mirathi na kutumia mali alizoziacha kama:​
  • Viwanja vya makazi
  • Akaunti za benki
  • Mashamba
Mahakama ilikubaliana naye, na ikamtangaza mumewe kuwa amefariki kisheria.

Lakini pia katika shauri hilo, Mahakama Kuu Temeke ilieleza wazi kuwa:
Disappearance for a minimum of five years is sufficient for a court to make such a declaration (presumption of death).” — Mugeta, J.​

Mahakama ilisema pia:
It is time we enact a law akin to the Presumption of Death Act, 2013 of the United Kingdom to take care of the affair of missing persons.”

Hii inaonyesha ukubwa wa tatizo na umuhimu wa kufuatilia haki yako kisheria.

Lakini si kila mtu aliyepotea kwa miaka 5+ atahesabika amefariki. Mahakama huangalia mambo kama:
✅ Alikuwa akipatikana kirahisi awali?
✅ Familia ilichukua juhudi gani kumtafuta?
✅ Imetolewa taarifa polisi au magazetini?

Kwa wanawake waliotelekezwa na waume waliopotea, hii ni njia pekee ya kuendelea na maisha kwa heshima ya kisheria:​
  • Kuolewa tena kihalali
  • Kurithi mali
  • Kuwasomesha watoto kwa kutumia mali ya baba yao​

❓Je, Wewe Upo Kwenye Hali Hii?
Unaishi kwenye ndoa ambayo mume au mke alitoweka miaka mingi iliyopita?
Umeshindwa kuendelea na maisha kwa sababu huna cheti cha kifo?
Umeshindwa kugusa na kutumia mali zilizokuwa kwa jina lake?

Basi huenda Presumption of Death ni njia yako ya kisheria ya kupata suluhisho.​
7BD23175-1833-420D-8D1F-EAD2083848E6.jpeg

IMEANDALIWA NA
Robik Attorneys & Legal Consultants (RALC)
Near Ubungo Plaza, Dar Es Salaam
🌐 www.ralc.co.tz | Instagram ralc255
Email.
info@ralc.co.tz | Phone. +255 683 505 715
Angalizo Muhimu (Disclaimer):
Maelezo yaliyomo kwenye uzi huu yametolewa kwa madhumuni ya elimu ya jumla tu na hayawezi kuchukuliwa kama ushauri wa kisheria wa moja kwa moja. Robik Attorneys & Legal Consultants haitawajibika kwa matumizi yoyote ya taarifa hizi bila kupata ushauri rasmi wa kisheria.​
 
Je, hii ni kwenye masuala ya ndoa tu au hata mtu akipotea tu kama yule Ben Saasaba kwa sasa anakuwa anahesabika kama alishafariki?

Na vipi kama mahakama ishagawa mali zake ila baadaye akatudi baada ya labda miaka 7?
 
Ndoa inavunjwa na pande zote mbili, tofauti na hapo oa kwa mara ya pili ila yule wa kwanza akipatikana haki zake zinaendelea kuwepo
 
Je,hii ni kwenye masuala ya ndoa tu au hata mtu akipotea tu kama yule Ben Saasaba kwa sasa anakuwa anahesabika kama alishafariki?
Na vipi kama mahakama ishagawa mali zake ila baadaye akatudi baada ya labda miaka 7?
Habari ndugu hamada umelewa asante kwa swali zuri.

Kwanza kabisa sheria zetu za Tanzania ambazo zipo kimaandishi katika suala hili mtambuka ni sheria ya ndoa Tu, lakini bado hata kwa mtu ambaye hakuonekana kwa kipindi kirefu kama ulivyotoa mfano wa bwan. Ben bado mtu anaweza kwenda mahakamani na kuiomba mahakama kutangaza mtu huyo ameshafariki chini ya Kanuni za Kisheria za Kimapokeo (Common Law Principle) yaani sheria ambayo chanzo chake si bunge bali ni maamuzi ya mahakama na desturi zilizoidhinishwa na mahakama, ushuhuda mzuri katika hili ni case ya Salum Omary Hamad.

Kwahiyo, Mtu yeyote mzima anapopotea bila kusikika kwa miaka mitano mfululizo, wale waliokuwa karibu naye kisheria (wake/waume, watoto, wazazi, au wadhamini) wanaweza kuomba mahakama itoe tamko la kwamba mtu huyo amefariki kisheria (presumed dead). Hii inaweza kuwa kwa ajili ya:​
  • Kufungua mirathi
  • Kusitisha au kusuluhisha ndoa
  • Kushughulikia mikopo au mali zilizobaki
  • Kurekebisha kumbukumbu rasmi (kama ID, uraia, nk.)
Na Ikitokea mtu amerudi baada ya kutangazwa kuwa amefariki kisheria bado ananafasi ya kulinda maslahi yake kwani tamko la presumption of death linaweza kufutwa (revoked) mara tu itakapothibitika kuwa mtu huyo yupo hai.

Mali zilizogawiwa kisheria hazirudishwi moja kwa moja, isipokuwa kwa kufungua shauri lingine mahakamani (kwa mfano, kudai mali kupitia case ya madai).

Iwapo mtu huyo alikuwa na mke/mume, ndoa mpya aliyooa/olewa mpendwa aliyebaki huweza kuwa halali ikiwa ilifanyika baada ya presumption of death, ila inaweza kuleta changamoto za kihisia na kisheria.

Karibu kwa msaada zaidi
 
Ndoa inavunjwa na pande zote mbili, tofauti na hapo oa kwa mara ya pili ila yule wa kwanza akipatikana haki zake zinaendelea kuwepo
Habari ndugu Auto-Marvelt Ulichosema kina mashiko kihisia, lakini kisheria tuna mifumo inayoweka utaratibu maalum pale ambapo mume au mke anapopotea bila mawasiliano kwa muda mrefu, na haijulikani kama yuko hai au la.

⚖️ Kisheria, Ndoa Haiwezi Kusubiri Kimya cha Milele Bila Hatua Rasmi
Sheria ya Ndoa Tanzania kupitia Kifungu cha 161(1) inasema wazi kuwa:​
Mtu anaweza kutangazwa kuwa amefariki ikiwa hajasikika kwa muda wa miaka mitano mfululizo na wale wanaotarajiwa kusikia kutoka kwake hawajasikia.”

Hii inampa aliyeachwa uhuru wa kisheria kuchukua hatua:​
  • Kuomba Mahakama itangaze ndoa hiyo kuwa imekoma kwa msingi wa “presumption of death”.​
  • Kuendelea na maisha (ikiwemo kuolewa/kuoa tena) bila hofu ya kuwa kwenye ndoa mbili kinyume cha sheria.​
🔁 Lakini swali la msingi linabaki pale pale. Je, Mwenza Akipatikana Baada ya Tamko?

Kama mtu aliyepotea akirudi baada ya kutangazwa amefariki:​
  • Hana haki ya moja kwa moja kudai “ndoa irudi”. Hali ya kisheria huanza upya, na inaweza kuhitaji maamuzi mapya ya Mahakama ikiwa kuna mgogoro.​
  • Tamko la Mahakama linaweza kufutwa kwa ushahidi mpya, lakini haliwezi kubatilisha kiotomatiki ndoa mpya au mgawanyo wa mali uliokwisha fanyika kihalali.​
Karibu kwa Msaada zaidi
 
Habari ndugu hamada umelewa asante kwa swali zuri.

Kwanza kabisa sheria zetu za Tanzania ambazo zipo kimaandishi katika suala hili mtambuka ni sheria ya ndoa Tu, lakini bado hata kwa mtu ambaye hakuonekana kwa kipindi kirefu kama ulivyotoa mfano wa bwan. Ben bado mtu anaweza kwenda mahakamani na kuiomba mahakama kutangaza mtu huyo ameshafariki chini ya Kanuni za Kisheria za Kimapokeo (Common Law Principle) yaani sheria ambayo chanzo chake si bunge bali ni maamuzi ya mahakama na desturi zilizoidhinishwa na mahakama, ushuhuda mzuri katika hili ni case ya Salum Omary Hamad.

Kwahiyo, Mtu yeyote mzima anapopotea bila kusikika kwa miaka mitano mfululizo, wale waliokuwa karibu naye kisheria (wake/waume, watoto, wazazi, au wadhamini) wanaweza kuomba mahakama itoe tamko la kwamba mtu huyo amefariki kisheria (presumed dead). Hii inaweza kuwa kwa ajili ya:​
  • Kufungua mirathi
  • Kusitisha au kusuluhisha ndoa
  • Kushughulikia mikopo au mali zilizobaki
  • Kurekebisha kumbukumbu rasmi (kama ID, uraia, nk.)
Na Ikitokea mtu amerudi baada ya kutangazwa kuwa amefariki kisheria bado ananafasi ya kulinda maslahi yake kwani tamko la presumption of death linaweza kufutwa (revoked) mara tu itakapothibitika kuwa mtu huyo yupo hai.

Mali zilizogawiwa kisheria hazirudishwi moja kwa moja, isipokuwa kwa kufungua shauri lingine mahakamani (kwa mfano, kudai mali kupitia case ya madai).

Iwapo mtu huyo alikuwa na mke/mume, ndoa mpya aliyooa/olewa mpendwa aliyebaki huweza kuwa halali ikiwa ilifanyika baada ya presumption of death, ila inaweza kuleta changamoto za kihisia na kisheria.

Karibu kwa msaada zaidi
Nashukuru kwa maelezo yako sasa nimeelewa.
 
Back
Top Bottom