Mwenyezi Mungu tujaalie tupate Magufuli Mwingine

Wakuu wasalaaam,
Namshukuru Mungu muweza wa yote ningali hai hata muda huu na type.
Kwa kweli niseme kweli, Magufuli ndiye rais bora wa wakati wote kwa mujibu wangu, simaanishi wengine hawafai ila katika wawili au watatu hatuna budi kuchagua.
Kwangu mimi kila ninapoona shida ya maji najisemea kimoyomoyo maybe mzee angekuwepo hizi mambo zisingekuwepo, ninapoona umeme unakatika katika pia namkumbuka mzee,
Wadau sina maana mbaya ila namkumbuka Magufuli.
Povu ruksa. Na kazi iendelee mama kasema.
 
Huna haja ya kujitetea! Ata mimi mwenye umri wa miaka 31 kwangu Nyerere sijamuona wala Mwinyi sijamuona akiwa madarakani! Lakini Che Mkapa kioindi hicho bado akili haijakomaa kuhusu masuala ya kijamii.

Niwekee Kikwete, Magu na Samia kama kura yangu sitopepesa macho inaenda kwa Magufuli.
 
Wakuu wasalaaam,
Namshukuru Mungu muweza wa yote ningali hai hata muda huu na type.
Kwa kweli niseme kweli, Magufuli ndiye rais bora wa wakati wote kwa mujibu wangu, simaanishi wengine hawafai ila katika wawili au watatu hatuna budi kuchagua.
Kwangu mimi kila ninapoona shida ya maji najisemea kimoyomoyo maybe mzee angekuwepo hizi mambo zisingekuwepo, ninapoona umeme unakatika katika pia namkumbuka mzee,
Wadau sina maana mbaya ila namkumbuka Magufuli.
Povu ruksa. Na kazi iendelee mama kasema.

IMG_20211212_185614_232.jpg
 
Yaani we wacha tu,tumerudi kulekule tulikotoka, rushwa imeanza kuota tena mizizi, tuseme ukweli sasa huduma zimekuwa ghali na kama huna kitu mkononi hakuna atakuita na kukuuliza shida yako, utaangaliwa tu pengine uambiwe nenda kule na huku.

Na ukitaka kujua angalia kwenye mambo ya passport hapa utaweza kuona ni kwa kiasi gani tumerudi tulikotoka.

Unahitaji pasi ndani ya siku basi weka laki tano unaletewa nyumbani, huna utaambiwe ulete viapo na makaburasha ya bibi yako babu yako na hata wale usio wakumbuka na kama haitoshi lete hati ya kiapo na hapo unapigwa kalenda, migration wamecharuka, Kitu ambacho wakati wa Magu ni jambo la siku mbili tu, jaza fomu weka picha kitambulisho cha Utaifa umemaliza kazi siku ya piili unapokea pasi yako.

Mwenyezi Mungu ametupa somo ambalo inafaa turudi nyuma na kumtaka msamaha,hakuna kama magufuli na dalili sizioni ,ni lazima tuombe tena atupatie kama yey,ye. Vyombo vilivyopo sasa ni vya kusukumana ni vile vya ukimwaga mboga namwaga ugali, wanaogopana, wanalindana , wakati wake akipata fununu tu anafuatilia kiaina siku ya pili unasikia jamaa hana kazi tena mbele za watu na kama haitoshi anakupa data zote ni jinsi gani umehusika katika kuvuruga.

yapo mambo alikuwa na kasoro ila sio yeye ni wale vitimba kwiri wanaotaka sifa na kujipitisha na alikuwa hata hao akiwapatia nafasi huwalipuwa tumeona akina makonda na wengine walikuwa wapo kwenye line zake, tuseme Nchi ilikaa sawa katika utowaji haki kwa kila raia haswa wale aliowaita wanyonge. Na wanaovuruga bado wapo na ndio hawa wanaopandikiza kesi za uongo, kubambikiza ndio wanazidi kuichafua nchi wakiamini wanalinda maslahi yao.

Naamini dua itaitikiwa na kupata mshika gongo mwengine.
Ewe Mwenyezi Mungu tuepushie mbali na kiumbe dhalim kama Meko kisije kupata nafasi ya uongozi tena katika Taifa letu

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Wakuu wasalaaam,
Namshukuru Mungu muweza wa yote ningali hai hata muda huu na type.
Kwa kweli niseme kweli, Magufuli ndiye rais bora wa wakati wote kwa mujibu wangu, simaanishi wengine hawafai ila katika wawili au watatu hatuna budi kuchagua.
Kwangu mimi kila ninapoona shida ya maji najisemea kimoyomoyo maybe mzee angekuwepo hizi mambo zisingekuwepo, ninapoona umeme unakatika katika pia namkumbuka mzee,
Wadau sina maana mbaya ila namkumbuka Magufuli.
Povu ruksa. Na kazi iendelee mama kasema.
Misukule ya Mwendazake imekosa mtu wa kuwalisha unga baada ya mmiliki kuzikwa Chato mwezi Machi
 
Back
Top Bottom