Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,056
Nimeyasikiliza na kuyasoma maelezo ya CDF juu ya dakika za mwisho za Hayati John Magufuli.
Kwa imani ya kikatoliki, na nadhani ya wakristo wote:
1) Dakika za mwisho huamua mwanadamu aende wapi, yaani aipokee huruma ya Mungu au aende jehanamu.
2) Hakuna dhambi isiyosamehewa na Mungu.
"Njooni kwangu ninyi nyote mnaoelemewa na mizigo ya dhambi, nami nitawapumzisha"
"Dhambi zenu hata ziwe nyekundu kama damu, nami nitaziosha"
"Tabibu hayupo kwaajili ya walip wazima bali wagonjwa"
"Nakuahidi,leo hii itakuwa pamoja nami peponi", aliambiwa jambazi aliyeomba msamaha dakika yake ya mwisho.
Pia kuna ule mfano wa wafanyakazi waliopewa kazi, mwingine asubuhi, mwingine mchana, mwingine alasiri, na mwingine jioni kabisa, lakini wote wakiahidiwa mshahara mmoja. Akimaanisha wapo wanaoishi maisha mema maisha yao yote, wapo wanaoanzia katikati, wengine dakika ile ya mwisho kabisa, lakini wote thawabu yao ni mbingu/ahera.
Mabeho anasema kuwa marehemu alimwomba wampeleke nyumbani kwake Chato, ili akafariki akiwa nyumbani kwake. Anasema pia kuwa marehemu alisema kuwa ugonjwa ule usingepona. Na yeye mwenyewe marehemu, akiwa na fahamu zake aliomba aitiwe kiongozi wa kiroho, akapewa mpako mtakatifu, na baada ya hapo akakata kauli, na jioni, akaaga Dunia.
Kwa wale wakatoliki, kuoneshwa kifo chako ni neema, kulindwa milango yako ya fahamu ni neema, kupokea mpako mtakatifu wa wagonjwa ni neema.
Bila ya kujali marehemu alikuwa na maisha gani kabla yake, lakini mwisho wa safari yake, kiimani marehemu, aliimaliza safari yake ya Duniani kwa neema ya huruma ya Mungu.
Wakati tukimkumbuka hayati Magufuli siku hii ya leo, zaidi tuyatafakari maisha yetu, tuyatafakari matendo yetu tukijua kuna siku maisha yetu yatakoma hapa Duniani, tujiulize tutaacha nini kwa watu wengine, tukitambua kuwa hekima ya Mungu siyo ya mwanadamu. Kuna wakati matendo yetu mazuri mengi au machache, huyatakasa makosa yetu mengi au machache, na hivyo kuipokea neema na msamaha kamili wa Mungu wetu. Apumzike kwa amani mwenzetu aliyetutangulia.