GE2025 Mwenyekiti wa UVCCM Kagera, Buruhan amegoma kusaini matokeo ya kura za maoni Bukoba vijijini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,608
Bukoba Vijijini | CCM Kura za Maoni Falis Athumani Buruhan amegoma kusaini matokeo ya kura za maoni baada ya kutoridhika na matokeo hayo yaliompa ushindi Dk. Jasson Samson Rweikiza, aliyeibuka mshindi baada ya kupata kura 6,485 kati ya kura halali 11,582 Falis Athumani Buruhan, alipata kura 4,619, huku wagombea wengine wakifuata nyuma kama ifuatavyo: 3. Fahami Mastawily Juma – 239 4. Asted William Mpita– 124 5. Edimund Emmanuel Rutaraka – 89 6. Philibert Francis Bagenda – 44

Buruhan aligonga vichwa vya habari zaidi Aprili 2024 baada ya kuibua mjadala alipotoa kauli hadharani akilitaka Jeshi la Polisi kutojihusisha na utafutaji wa watu wanaomkosoa Rais Samia na viongozi wengine mitandaoni endapo watapotea.

Your browser is not able to display this video.
 
Falis Athumani Buruhan amegoma kusaini matokeo ya kura za maoni baada ya kutoridhika na matokeo hayo yaliompa ushindi Dk. Jasson Samson Rweikiza, aliyeibuka mshindi baada ya kupata kura 6,485 kati ya kura halali 11,582
Falis Athumani Buruhan, alipata kura 4,619, huku wagombea wengine wakifuata nyuma kama ifuatavyo:


3. Fahami Mastawily Juma – 239
4. Asted William Mpita– 124
5. Edimund Emmanuel Rutaraka – 89
6. Philibert Francis Bagenda – 44

Chanzo : NipasheDigital

Pia soma
~
Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute
~ Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali
 
Huyu jamaa hana sifa ya kuwa kiongozi, ndo alisema tukiona watu wanapotezwa tusishangae
 
siku nyingine hakikisha taarifa yako ndio uandike
 
Huyu dogo bado sanaa kisiasa kuna vitu anakosa
 
Alikuwa na matumaini makubwa kupita kiasi, sasa matokeo yamemshangaza.
Bahati mbaya sana Kwenye kura za maoni hata usiposaini haisaidii chochote, imeisha hiyo.
 
Akashughulike na mpinzani wake na polisi wasiingilie. 😅

Menyewe kwa menyewe!
 
Alikuwa na matumaini makubwa kupita kiasi, sasa matokeo yamemshangaza.
Bahati mbaya sana Kwenye kura za maoni hata usiposaini haisaidii chochote, imeisha hiyo.
Kiburi cha kutumika kama chui wa karatasi au kinyago cha mpapule akimwakilisha Karamagi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera. Hakujua kama hata mchonga kinyago (Karamagi) amemshindwa Rweikiza mara mbili.

Lililobaki akavae kanzu na baraghashia akasubirie mpango wa Sa100 na Karamagi
 
Classmate Rutaraka ,jina la mshua wake halijambeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…