Mwenyekiti Wa Ukombozi Na Ufahari!

Mwenyekiti Wa Ukombozi Na Ufahari!

MATOLA SIGNATURE WAFU: Hawa ni maiti wako Hai ila ni mazoba, hata wakiambiwa na CCM walipie PUMZI na USINGIZI watalipia ingawa hawana kitu. Wanakubaliana na kila hali hawajui kupinga wala kukataa, hawana tofauti na mabehewa ya treni kinakokwenda kichwa ndiko wanakokwenda wao.
 
Hatuwezi kukubali mabadiliko kisha tukapinga kile kiletacho mabadiliko hayo, na pindi tutakavyofanya hivyo tutajiingiza katika utata wa kimantiki. Utata ambao utapelekea watu kuhoji juu ya dhamira yetu na misimamo tuliyonayo.

Ndio ni utata, kukubali umuhimu wa kitu na kupinga kutumika kwake..,nasema Mbowe atueleze matumizi ya VX-standard kwenye ziara yake kusini na hata hapa dar hakupingani na sera yake ya kupunguza gharama??? au gharama za VX standard ni pindi tu ikitumika na viongozi wa serikali na akina Nape???

Lazima tuweke bayana ni kipi tunapinga na kipi tunakikubali na kwanini tunapinga ama kukubali.,ama sivyo ni UTATA MTUPU..!!!
 
Hii thread si ipo unaanzisha ili iweje? watanganyika bana!
 
Haya ni mitumba ndugu....wale AURORA wameyaweka kwenye patrol zao kuonyesha hayana thamani kubwa
 
Hatuwezi kukubali mabadiliko kisha tukapinga kile kiletacho mabadiliko hayo, na pindi tutakavyofanya hivyo tutajiingiza katika utata wa kimantiki. Utata ambao utapelekea watu kuhoji juu ya dhamira yetu na misimamo tuliyonayo.

Ndio ni utata, kukubali umuhimu wa kitu na kupinga kutumika kwake..,nasema Mbowe atueleze matumizi ya VX-standard kwenye ziara yake kusini na hata hapa dar hakupingani na sera yake ya kupunguza gharama??? au gharama za VX standard ni pindi tu ikitumika na viongozi wa serikali na akina Nape???

Lazima tuweke bayana ni kipi tunapinga na kipi tunakikubali na kwanini tunapinga ama kukubali.,ama sivyo ni UTATA MTUPU..!!!
sema hukubali wewe na NYINYIEMU,USITUSEMEE ALAAAAAAA!
 
The Horse big up kwa uzi huu naunga mkono hoja, naona baadhi ya wenzetu hapa CDM nao wanasumbuliwa na ugonjwa wa viongozi wengi wa CCM ambao mara nyingi wanasema ambacho hawamaanishi. Mbowe na CDM tumekuwa mstari wa mbele kupinga matumizi mabaya ya fedha za umma ikiwemo viongozi kutumia MASHANGINGI. Ajabu hata yeyey sasa anaona burdani kuranda na hayo MASHANGIGI. Kwa fikra zangu uhenda hata hapa CDM nako sio shwari kivile, wasi wasi wangu uko mbele ya safari. Tusilewe sifa na kujifanya hatuoni, kama kiongozi/wamanachama wa CDM akipotoka tuambiane ukweli tuache unafiki wa MAGAMBA sote tunajua unafiki wao ulipowafikisha. Sitaki silly excuses katika hili. Kuna Kiongozi mmoja wa dhehebu flani aliwahi kuuliza kuhusu UFISADI kama watu wote tunauchukua kwa DHATI na DHAMIRA ZETU au ni ukosefu wa FURSA. CDM tunaanza kuthibitisha hili kuwa KELELE zetu nyingi nyuma ya pazia kuna mengi yamejificha. Siasa za Bongo ni ngumu kumpata Kiongozi mwenye machungu na nchi hii, wengi tunasukumwa na njaa zetu zikiambatana na malengo binafsi. Sina ushabiki wala unafiki wa siasa.
 
wakubwa!.....Huyu gamba lake limekaa pabaya,lipo kwenye......
 
Kwani haya ni ya umma au ya chama?
 
hoja haina mashiko kwa sasa
hilo ni vx moja tu je ukihesaabu hayo ya mawaziri, wakuu wa vitengo, wakuu wa mikoa na wilaya ni mangapi?
haiingii akilini mkuu wa wilaya anatembelea vx la millioni 150 wkt vijiji vyake havina maji,barabara,hospoitali wala madawati.
ukitaka kumtoa mvuta bangi kuacha bangi nawe vuta bangi afu mweleze madhara yake ndicho anachofanya mbowe
gari magamba si wamempa? amerudisha akaambiwa lazima atumie sasa afanyeje
?auze? uwezo wa kuliuza hana bora alitumie kukiimarisha chama ili kuinyonga vema CCM
KAMUA BABA CCM WAMEKUPA BOMU LA KUWALAIPUWA WAO WENYEWE
 
wakubwa!.....Huyu gamba lake limekaa pabaya,lipo kwenye......

Enyi ndugu waTaifa hili hii hoja inaenda na inarudu kila kukicha si kwamba watu ni machizi au laa.....ni kwamba watu siku hizi si wakuburuza tuu kama misukule....Hii hoja ya mashangingi chama kama kweli ni cha watu then ajitokeze kiongozi na kutolea maelezo ya kina ikiwa ni pamoja na kutoa comparative advantages and disadvantages za magari mengine.

Lakini majibu kama vile
Hilo lake binafsi
Au hili ni la mtumba......sijui Aurora wameyafanya ni road patrol
Na majibu kama haya......yataturudisha kwa mada hii kila uchao......shime wahusika.....sio wafuasi wa chama mje hapa muwape wanachama wenu maelezo
 
Hatuwezi kukubali mabadiliko kisha tukapinga kile kiletacho mabadiliko hayo, na pindi tutakavyofanya hivyo tutajiingiza katika utata wa kimantiki. Utata ambao utapelekea watu kuhoji juu ya dhamira yetu na misimamo tuliyonayo.

Ndio ni utata, kukubali umuhimu wa kitu na kupinga kutumika kwake..,nasema Mbowe atueleze matumizi ya VX-standard kwenye ziara yake kusini na hata hapa dar hakupingani na sera yake ya kupunguza gharama??? au gharama za VX standard ni pindi tu ikitumika na viongozi wa serikali na akina Nape???

Lazima tuweke bayana ni kipi tunapinga na kipi tunakikubali na kwanini tunapinga ama kukubali.,ama sivyo ni UTATA MTUPU..!!!

magamba kweli tumeishiwa sela daaa! watu walishaijadili sana hii!
 
Mkubwa! OLESAIDEMU ,achieni nchi iongowe na CHADEMA kwanza alafu muhoji.....Gamba litawavuka nyie subirini
 
Enyi ndugu waTaifa hili hii hoja inaenda na inarudu kila kukicha si kwamba watu ni machizi au laa.....ni kwamba watu siku hizi si wakuburuza tuu kama misukule....Hii hoja ya mashangingi chama kama kweli ni cha watu then ajitokeze kiongozi na kutolea maelezo ya kina ikiwa ni pamoja na kutoa comparative advantages and disadvantages za magari mengine.

Lakini majibu kama vile
Hilo lake binafsi
Au hili ni la mtumba......sijui Aurora wameyafanya ni road patrol
Na majibu kama haya......yataturudisha kwa mada hii kila uchao......shime wahusika.....sio wafuasi wa chama mje hapa muwape wanachama wenu maelezo

Sidhani kuwa na kutumia VX ni tatizo. Tatizo ni kuwa unayo mangapi na je yana ulazima kuwa ? tunaambiwa kuwa serikali inamiliki magari haya yenye thamani ya Tshs 5 Trilioni......na ndio hoja yenyewe lakini si kuwa serikali isiwe kabisa na magari haya!!!.......unajua hii pesa ina weza kufanya mangapi? Mbaya zaidi maafisa wa serikalai wanfanya biashara katika manunuzi ya haya magari....mimi nimesisistiza kuwa haya ya CHADEMA siyo kama yale ya serikali kwa kuwa ni ya mtumba na hayana gharama ndio maana AURORA anayatumia katika patrol....
 
By Safari_ni Safari "Kwani haya ni ya umma au ya chama?

Kwa ufahamu wangu umma ndio unazaa Chama nashindwa kuelewa msingi wa swali lako. Hoja yangu ni kwamba CDM kama Chama wanawezaje kuthubutu kutumia Mashangingi kama haya ili hali umma unaotaka kuwaweka madarakani na unaohudhuria mikutano yao ukiwa umepigika kupita kiasi? Pesa hizo cha Chama zingetumika kwa matumizi mbadala yenye kulenga maslahi na ustawi wa walio wengi. Tuache kujiliwaza tuangalie mambo kwa mapana yake. Sisi wananchi ndo huwa tunachangia kuwalevya madaraka Viongozi wetu. Najua wengi hatupendi kujadili mapungufu ya Viongozi wa CDM kwasababu nafsi zetu zimejawa na UNAFIKI ULIOKUBUHU.
 
Tut tut tut..........hatuelewani kumbe? Hebu soma post #16.........halafu ona huyu RIDHIWANI alipokuwa anazungusha fomu za baba mwaka 2010 labda ndio utanielewa

1.JPG
 
Back
Top Bottom