Nina kiwanja changu kama nusu eka nilichonunua 2012 maeneo ya Chanika. Nilikizungushia fence ya waya na mara moja moja nilikuwa natuma mtu apasafishe.
Takriban miaka 6 nilikuwa nje ya Dar kikazi. Nimerudi mwisho wa mwezi wa 9 ila ilikuwa sijapata fursa ya kwenda kwenye kiwanja changu.
Jana nilikutana na jamaa yangu ambae ni dalali. Katika kupiga story akaniambia kuna kiwanja kikubwa kinauzwa Chanika. Baada ya kutaja eneo nikamwambia hata mimi nina eneo langu huko. Tukakubaliana leo tuende kuangalia kiwanja chake anachouza na mimi nipitie kwangu.
Tulianzia kwa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa maana kwa mujibu wa dalali ndiye muhusika mkuu.
Kupelekwa kwenye kiwanja ni eneo langu. Sijataka kusema chochote nikamuacha aongee tu. Anadai kiwanja ni cha baba wa mkewe kampa mwanae hivyo wameamua kuuza.
Kumuhoji kuhusu nyaraka akadai anao mkataba wa mauziano wa serikali za mitaa. Nimeona copy una tarehe ya 2014. Mimi nina leseni ya makazi na tayari hati ipo katika process. Zoezi la hati lilifanywa shirikishi kwa wakazi wa eneo lote hilo.
Nilichoamua, kesho naamkia polisi kumshitaki jamaa kwa utapeli maana nina rekodi ya sauti ya maongezi yake yote. Nitahakikisha mpaka wamtie ndani.
Angalizo kwa walimwengu, wekeni mazoea ya kutembelea viwanja vyenu, msitelekeze kwa muda mrefu bila kwenda. Hakikisheni kila document ipo up to date na la muhimu zaidi epukeni sana kununua viwanja kiholela bila kujiridhisha ardhi kwanza.