BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Hamisi na mwenzake Juma Kapilima, mkazi wa Liwale, walitenda kosa la kuharibu na kuuza miundombinu ya Kingo za Mabomba ya Gesi, Juni 2022 na kulisababishia hasara hiyo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Pamoja na hukumu hiyo, Washtakiwa wote wawili wametakiwa kulipa kiasi cha Tsh. 54,710,000 kama fidia kwa TPDC kutona na uharibifu uliofanywa.
============
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Lindi imemhukumu kifungo cha miaka 20 aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji cha Mahumbika wilayani humo Hamis Bandari (46) kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka.
Hamisi amepata hukumu hiyo Pamoja na mwenzake Juma kapilima (38) ambaye ni mkazi wa wilaya ya Liwale aliyehukumiwa miaka 20 pia kwa kosa la kuharibu miundombinu ya gesi na kuisababishia hasara shirika la maendeleo ya Pertoli Tanzania (TPDC) na serikali kiasi cha shilingi milioni 119.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, watu hao walitenda makosa hayo mwezi Juni 2022 baada ya kuharibu miundombinu ya mabomba ambayo yanayotumika kuweka kingo katika sehemu linapopita bomba la gesi na kisha kwenda kuyauza.
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Lindi Maria Batulaine ambapo pia amewataka wawili hao kulipa shirika la TPDC fidia ya Shilingi Milioni 54,710,000