<br />Mnamkaribisha kwenu, kwani munajua chanzo cha mgogoro? Hebu shughulisheni akili kidogo kugundua tatizo nini kabla ya kumkaribisha? Mbona Mh. Rostamu hamjamkaribisha au yeye alijivua gamba na huyu mwenyekiti amejivua shati?
nadhani we nae ni gamba! kwa jinsi mi nianvymfahamu msukuma, alikuwa ni mtu wa kuhoji matumizi ya fedha za wananchi-umma. nimemuona mara nyingi akizungumzia madaraja yaliyojengwa chini ya kiwango ilihali mihela kibao imetumia...actually huyu jamaa alikuwa na approach zote za chadema sema tu ailiingilia mlango mbaya.....taarifa yako iwasilishe vizuri bila kuichakachua. fafanua ni wapi kajiuzulu na wapi kavuliwa uenyekiti wa halimashauri.
Ni kweli kabisa alikuwa na migogoro na madiwani wenzake, ndipo jana ukumbi wa halimashauri ulizingirwa na polisi kwa kuwa kikao kilichokuwa kinaendelea kililenga kumvua uenyekiti wa halimashauri.
madiwani wa geita walifanikiwa kumvua uenyekiti wa halimashauri ambo aliupata kwa kununu kupitia makusanyo yake katika magari yake ya kusafirishia abiria.
Musukuma hakujiuzulu uenyekiti wa halimashauri, alivuliwa na madiwani wenzake. baada ya kuhisi heshima yake imeshushwa, ndipo alipotangaza kuachia na nafasi zake zote zilizotokana na yeye kuwa diwani pamoja na udiwani wenyewe. hakujiuzulu kwa kupenda bali alitimuliwa, ndo akaachia nafasi zake zote.
kinachomusumbua Msukuma, ni kiburi cha mali alizonazo, akadhani halimashauri itaongozwa na kiburi cha pesa zake. darasa han, ndharia za uongozi hana ili mradi ana hela kila kitu alinunua.
<br />HUYU mwenyekiti sijamuelewa..,nimemsikiliza jana kwa umakini mkubwa lakini nikashangaa anaposema Anajiuzulu na UDIWANI.sasa yeye tumemchagua kura diwani hiyo ya uenyekiti ni mikakati yake,sasa inakuaje anataka kutusaliti tuliompigia kura mwaka 2010,kwa ajili ya wachache ambao kipindi hicho nao walikuwa wakiomba kura kwa watu wa kata zao....SASA hapa tufikirie ALIKUWA anafuata nini? tumwache aende CCM ina watu wengi wenye uwezo zaidi zake yeye.POLENI wapigAKURA WA NKOME
Habari za kutoka Geita zinadai kuwa mwenyekiti alikuwa anahoji matumizi ya pesa ambazo zinatolewa GGM (Mgodi wa geita) kusaidia maendeleo ya wilaya ya geita.
Pamoja na fedha lukuki zitolewazo hakuna maendeleo ambayo mtu anaweza kuonyesha wapi hizo fedha zimefanya kazi. Maana nasikia alienda kuonana na uongozi wa mgodi kuhoji nivipi wanasaidia maendeleo ya wilaya wakampa takwimu zote za fweza, ndo alitaka kujua pesa ziliko enda. Basi wale wanao tafuna na wanasomeshea watoto wao ulaya wakaona huyo si mwenzao, kwa kutumia pesa zao wamewahonga madiwani na leo wakapiga kura ya kutokuwa na imani naye na kikao kilihudhuliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza " KANDORO"
CCM hawawataki kabisa watu ambao wapo kwa maendeleo ya UMMA
Kanyasu upo sawa ninachojua mimi juu ya msukuma ni mtu anaependa umaarufu huku akisema uongo wa wazi, wengi wanajua ni mtetezi wa wanyonge ukweli yule ni mfanyabiashara ambaye kila anachogusa anataka apate faida, walivyomkatalia akaanzisha majungu, ni msukuma huyhuyu aliyesema eti eneo la hospital limeuzwa na akasema anao ushahidi alipoulizwa eneo gani atoe ushahidi akashindwa. Amekua kero kwa makandarasi wilayani humu kila kukicha anadai mpaka ashibe ndo watapata kazi.Habari za uhakika kutoka kata za nkome,katoma,nzera na lwezera zinasema wananchi wapambe wa msukuma wamefanya vurugu kubwa hadi mtu mmoja kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya kwa kutaka kumnyang'anya siraha polisi.vurugu hizo zimesababisha askari wa ffu kutoka geita kwenda huko umbali wa km 65 kutoka geita mjini.
Source katibu wa ccm kata ya nkome.
Karibu kwetu,peoplez power[/QUOTE
TATIZO ni kuwa mafiisadi wa vidole viwili huwa hawaachi kukaribisha pia mafisadi wenzao toka CCM
ujumbe murua.99.9ni heri kuchelewa ufukweni ukisubiri chombo kingine kuliko kupanda jahazi lililotoboka. bg up mwenyekiti!