Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi nchini asema kuporomoka kwa bei ya Samaki kutasabisha uvuvi haramu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Mwenyekiti wa Chama Cha Wavuvi Nchini, Bakari Kadabi amesema Kuporomoka bei ya samaki kutapelekea kufilisi mitaji yao na kuchochea uvuvi haramu kwasababu italazimika wavuvi wahakikishe wanapata samaki wengi ili wapate kipato kikubwa

Aidha, ameiomba Serikali kuingilia kati mabadiliko ya bei za uuzaji wa mazao ya samaki viwandani pamoja na kusimamia sheria ya ununuzi wa mabondo yanayotokana na sangara kufuatia kutokuwepo utaratibu maalumu wa uuzwaji hivi sasa

Bei ya kilo moja ya Samaki inadaiwa kuporomoka kutoka Tsh. 11000 hadi Tsh. 7000

Source: Dar Mpya
 
Yeye hataki wananchi wapate unafuu wa bei anaita kuporomoka kwa bei.
Anasahau kama hizo bei zimepanda haraka haraka juzi kati tu? Akiona zinashuka ajue supply imezidi demand bila shaka au kuna cost flan imeshuka hivyo bei itashuka kama ilivyo kwa bidhaa zingine.

Alafu hiki kitu kinaitwa chama cha wavuvi ni porojo tu, Tanzania ina maeneo mengi sana ya maji na uvuvi wake haufanani, kuwa na chama chenye mtazamo mmoja ni jambo gumu aache porojo na siasa za bei rahisi
 
Back
Top Bottom