Wizara ya Uvuvi itoe kipaumbele kwa Wavuvi Wadogo na wa kati

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,944
12,506
Mwaka jana wizara ya uvuvi kwenye bajeti ilitenga pesa kwa ajili ya kusaidia uvuvi , na likatoka tangazo la watu wanaotaka mikopo kwa ajili ya uvuvi waandike majina yaende Makao Makuu Dodoma.

Majina yalienda na mpaka leo hakuna mrejesho, wiki iliyopita wizara imeandaa semina na mafunzo kwa ajili ya vijana 500, ufugaji samaki kwenye mabwawa nchi nzima. Kwenye uvuvi changamoto za wavuvi ni zana duni,boti,engine na mitaji ya ununuzi mafuta ya uvuvi.

Wavuvi wakiwezeshwa itainua kuanzia wavuvi wenyewe,wachuuzi wa samaki,wakina mama wanaouza samaki mtaani. Uvunaji wa samaki ni mdogo kuliko uhitaji wa samaki nchini ingawa tuna ukanda mkubwa wa pwani ya Bahari ya Hindi.
20230226_090222.jpg
 
Pesa waliweka kwenye fixed account benki ya wakulima (TADB) ili KUPIGA RIBA kwa miezi 6 kwanza. Sasa hivi wameanza kusikilizia upepo, wakisikia maneno maneno yamezidi wanatupia kapicha kamoja kwenye ukurasa wao wa twitter kisha wanaendelea kusikilizia

Ukisikia miradi inasimamiwa na serikali ya CCM ujue HAMNA KITU HAPO, pesa inaenda kwenye kazi za chama na nyingine wajanja wananunulia MAJUMBA YA KIFAHARI huko Amerika na Paris

Mikopo Vizimba.PNG

Fishing boat.jpg
 
Tanzania imezungukwa na maji kila eneo ila hao Samaki ni ghari kwa kuwa mazingira ya wavuvi sio rafiki...
Urafiki upi? Mbona serikali yako inazidi kujinasibu kumwaga fursa?

BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUWAINUA WAFUGAJI, WAVUVI NCHINI​

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete na kujadiliana namna wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kuimarisha Sekta ya Mifugo na Uvuvi hapa nchini.
Waziri Ulega alikutana na Mkurugenzi huyo ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo Machi 23, 2023.

Katika mazungumzo yao, Waziri Ulega alimueleza Mkurugenzi huyo kuwa kipaumbele cha Wizara ni kuboresha maisha ya wafugaji na wavuvi na ndio maana kwa sasa wamejikita katika kuanzisha vituo atamizi kwa vijana ili wafanye ufugaji wa kisasa, kuwawezesha vijana kufuga samaki kwa njia ya vizimba katika ukanda wa ziwa Victoria, kukopesha wavuvi maboti ya kisasa ya uvuvi ili waachane na uvuvi wa kuwinda.

Alisema kuwa wavuvi wengi wamekuwa hawapati mavuno ya kutosha, kutokana na vifaa duni vya kufanyia uvuvi, wanavua samaki kati ya kilo 10-100, ni kiasi kidogo ambacho kinaendelea kuwafanya wavuvi wengi kubaki katika umasikini, lakini wakiendelea kupatiwa boti za kisasa uzalishaji katika sekta ya uvuvi utaongezeka na maisha ya wavuvi yatakuwa bora zaidi.

"Hivyo ili wavuvi wetu waweze kufaidika na rasilimali za uvuvi ni muhimu kuwawezesha vifaa vya kisasa ili waweze kuvua katika kina kirefu cha maji wapate mazao ya kutosha kukuza kipato chao na Taifa kwa ujumla", alisema Mhe. Ulega

Kuhusu Sekta ya Mifugo, Waziri Ulega alieleza kuwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ina maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji wa malisho na ufugaji na hivyo aliwaomba Benki ya Dunia kuona pia namna ambavyo wanaweza kuwezesha uwekezaji.

Kwenye eneo la udhibiti wa magonjwa, Mhe. Waziri alisema kuwa kwa sasa wanajipanga kuwa na Kampeni kubwa ya Kitaifa ya kuhamasisha uchanjaji wa mifugo ili kupunguza vifo vya mifugo kutokana na magonjwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete alimuhakikishia Waziri Ulega kuwa Benki ya Dunia itaendelea kuimarisha ushirikiano ili kuzifanya sekta hizo mbili ambazo zinategemewa na wananchi wengi kuendesha maisha yao kuzalisha kwa tija na kuondoa umasikini miongoni mwao.

Aliongeza kwa kusema kuwa Benki ya Dunia imekuwa ikifadhili miradi ya Wizara hivyo wako tayari kuendelea kushirikiana ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwainua wananchi wake kiuchumi kupitia sekta hizo mbili.

Naye, Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe alisema wako tayari kushirikiana na Benki ya Dunia hususan katika kuongeza ajira za vijana na kina mama kupitia vituo atamizi na ufugaji viumbe maji.
 
Mkuu naona unakuja na taarifa za Bank ya Dunia njoo na aina za Samaki wa baharini au maji baridi tunaokula ili uone hizo ni data tuu samaki ni ghari wanaoweza kumudu kwa maeneo mengi ni wachache sana...
 
Umeisoma vizuri hiyo taarfa? Usipofuatilia taarifa sahihi, utaendelea kulalamika MILELE
 
Pesa waliweka kwenye fixed account benki ya wakulima (TADB) ili KUPIGA RIBA kwa miezi 6 kwanza. Sasa hivi wameanza kusikilizia upepo, wakisikia maneno maneno yamezidi wanatupia kapicha kamoja kwenye ukurasa wao wa twitter kisha wanaendelea kusikilizia

Ukisikia miradi inasimamiwa na serikali ya CCM ujue HAMNA KITU HAPO, pesa inaenda kwenye kazi za chama na nyingine wajanja wananunulia MAJUMBA YA KIFAHARI huko Amerika na Paris

View attachment 2568172
View attachment 2568174
Hapa kupata huu mkopo ndio shughuli nyingine na hizo boti uwezi kwenda deep sea kuvua.

Zanzibar waliweka pesa ya boti zaidi ya 1000 boti zimetengenezwa chini ya kiwango na mpaka sasa hazija leta matokeo chanya
 
CCM ina viongozi wa hovyo sana, wanachowaza ni kuiba mapesa na kujenga mahekalu huko Marekani, Paris na n.k

Hiyo miradi ilipaswa wavuvi wakopeshwe pesa taslimu, kisha wakanunue wenyewe vitendea kazi kulingana na mahitaji yao
 
Pesa waliweka kwenye fixed account benki ya wakulima (TADB) ili KUPIGA RIBA kwa miezi 6 kwanza. Sasa hivi wameanza kusikilizia upepo, wakisikia maneno maneno yamezidi wanatupia kapicha kamoja kwenye ukurasa wao wa twitter kisha wanaendelea kusikilizia

Ukisikia miradi inasimamiwa na serikali ya CCM ujue HAMNA KITU HAPO, pesa inaenda kwenye kazi za chama na nyingine wajanja wananunulia MAJUMBA YA KIFAHARI huko A
CCM ina viongozi wa hovyo sana, wanachowaza ni kuiba mapesa na kujenga mahekalu huko Marekani, Paris na n.k

Hiyo miradi ilipaswa wavuvi wakopeshwe pesa taslimu, kisha wakanunue wenyewe vitendea kazi kulingana na mahitaji yao
Kweli mkuu, hizo boti za mita 5,7 mpaka 12 haziwezi kuleta tija wala kwenda deep sea kuvua.

Njia sahihi ni kuwapa watu mikopo ya vifaa au pesa ya kununua vifaa. Ziwa Victoria tayari lipo full utilized lakini kuna viongozi wanapeleka mikopo ya boti wakati Ziwa Nyasa,Tanganyika hata robo uvuvi haufanyiki
 
Kwa bahati mbaya ni kama HATUNA RAIS tu, anakubali vipi kuruhusu Waziri ambaye hajawahi kuingia ziwani kufanya shughuli za uvuvi afanye kazi ya manunuzi ya vifaa vya wavuvi?
 
Baharini hazihitajiki hizo boti ndogo, bora wawadhamini watu kwa vikundi wapewe pesa wajenge boti kubwa za mbao wanunue engine za inboard hata za kichina (Weichai,Yuchai Cummins zinakuja na marine gearbox kwa wastani wa bei za kawaida) zitaleta tija wavuvi watapata boti kubwa ambayo ina cold room hata wakikaa deep sea week wanarudi na tani kuanzia 5 za samaki na zimetunzwa vizuri.

Hizo boti ndogo waziri itakuwa kalenga uvuvi wa dagaa kwenye uchumi wa buluu. Boti kubwa moja la Mbao linaleta impact kwa wavuvi,wachuuzi,vijana wa kusaidia kazi mpaka kwa wakina mama wa wauza samaki mtaani
 
Pesa waliweka kwenye fixed account benki ya wakulima (TADB) ili KUPIGA RIBA kwa miezi 6 kwanza. Sasa hivi wameanza kusikilizia upepo, wakisikia maneno maneno yamezidi wanatupia kapicha kamoja kwenye ukurasa wao wa twitter kisha wanaendelea kusikilizia

Ukisikia miradi inasimamiwa na serikali ya CCM ujue HAMNA KITU HAPO, pesa inaenda kwenye kazi za chama na nyingine wajanja wananunulia MAJUMBA YA KIFAHARI huko Amerika na Paris

View attachment 2568172
View attachment 2568174
Nchi ina mambo mengi sana nilipambana mpka nikachoka sikupata hata harufu ya boti
 
Back
Top Bottom