Mwenyekiti UWT Taifa, Mary Chatanda afurahishwa na kikundi cha Wanawake wanaofuga Ng'ombe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
MWENYEKITI UWT TAIFA NDUGU CHATANDA AFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA KIKUNDI CHA WANAWAKE WANAOFUGA NG'OMBE WILAYANI MKALAMA

Mwenyekiti wa UWT Taifa ndugu Mary Pius Chatanda amefurahishwa na utekelezaji wa mradi wa kikundi Cha wanawake Tunza kilichopo Mkalama Mkoani Singida ambacho kimenufaika na fedha za Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kupewa sh milion 20,000,000.00.

Akizungumza leo alipotembelea mradi huo Wanawake wa Kikundi Cha Tunza Mwenyekiti Chatanda amewaomba wanawake hao kuendelea na Uzalishaji wa Ng'ombe ambao umeweza kuendelea kulipa fedha hizo za Halmashauri kwa wakati.

"Wanawake wenzangu niwapongeze sana kwa Uzalishaji wa mifugo hii ambayo imeleta tija kubwa katika kikundi chenu ambacho kimekuwa kinazalisha maziwa kwa wingi na yananunuliwa katika Wilaya ya Mkalama na Wilaya jirani kweli nyie ni Jeshi kubwa niwapongeze sana"

UWT IMARA JESHI LA MAMA KAZI IENDELEE

WhatsApp Image 2023-08-14 at 10.37.23.jpeg
 
Back
Top Bottom