VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kuanzia kwenye Kampeni zake mwaka 2015, Dr. Magufuli alijipambanua kuwa ataongoza Serikali ya Magufuli na si Serikali ya CCM. Na akayasimamia maneno yake ya kwenye kampeni, baada ya ushindi wake, kwa maneno na vitendo. Aliita Serikali ni ya Magufuli na si vingine. Mbunge Mstaafu wa Kilwa Kusini na mtani wangu Suleiman Bungara alias Bwege alizungumzia suala hili Bungeni mapema sana. Msikilize hapa alipozungumza suala hilo Bungeni na hata 'kuisambaratisha' taarifa ya Waziri Jenista Mhagama.
cheka kidogo na huyu Mbunge anayejiita Bwege na hivi vituko vyake - Bing video
Dr. Magufuli, Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM alisema na kutenda kadiri alivyoahidi kwenye kampeni na 'akawaambukiza' makada, viongozi wa chama na Serikali na hata wananchi wa kawaida kuwa hii iliyopo madarakani ni Serikali ya Magufuli. Kuna wakati Hayati Mkapa alikikosoa kitendo hiki cha 'kuhodhi' jina la Serikali. Ikasemwa na kutendwa kuwa Rais ametoa; Rais amechukua; Rais ameanzisha; Rais amejenga; Rais ametugawia na kadhalika. Akatamba Dr. Magufuli.
Sasa tumefika kwenye uchaguzi mkuu mwingine. Wapinzani wamekuja kivingine. Wanamtajataja binafsi Dr. Magufuli kwenye kauli zao. Wanakosea hadi wapigwe vijembe na Waziri Mkuu, Viongozi wa kidini na wengineo? La hasha! hawakosei. Wapinzani wanaendana na yaliyosemwa na kufanywa na hata makada wa CCM kwa miaka yote ya uongozi wa Rais Magufuli. Kama kila jema lililofanywa na Serikali sifa zinamiminwa kwa Rais Magufuli binafsi, kwanini kukosolewa ikosolewe CCM au Serikali kwa ujumla? Mkosolewaji abaki yuleyule msifiwaji.
Natarajia wakati wa kampeni jina la Dr. Magufuli litatawala vinywani mwa wapinzani kama lilivyotawala vinywani mwa makada katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza ya uongozi wake. Mwenyekiti, Rais na Mtani wangu Magufuli akubali matokeo yaliyotokana na matukio. Ajibu mapigo kwa hoja za haja na kuonesha mazuri yake ambayo yamefanyika chini yake. Lakini, kuwakataza wapinzani-akina Lissu na wengine wasimtajetaje si dawa wala sahihi.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa jijini Dodoma)