Mwenyekiti atishia kwenda kwa Rais mbele ya Waziri Lukuvi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
3 Mar 2021
Mtoto wa Muasisi wa TANU uso kwa uso na Mh. Lukuvi, matatizo ya ardhi jijini Mwanza



Leo March 03, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Makazi William Lukuvi amekutana na Watumishi wa Jiji la Mwanza idara ya ardhi na wengine, Waziri Lukuvi akiendelea na kikao nje kukawa na Wananchi wenye migogoro wakiwa na mafaili yao wakimgoja

Source: Millard Ayo
 
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.

Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.

Mitano tena!

Haijalishi bado anahaki ya kusikilizwa sio kupuuzwa

Watu hatufanani na uasili hatufanani pia.

Kila mtu ana haiba na silika yake.

Huyu ndivo alivoumbwa.
 
Kuna sehemu nilikaa kijiwe cha mitaani nikisikiliza habari za vijana wanazodokezewa na wahusika wa serikali. Moja ya tatizo ni tamaa ya mwaziri pia. Unamkuta waziri Lukuvi anatatua migogoro ya ardhi kila kona aendako, lakini wakati huo huo yeye mwenyewe anatafuta viwanja na mashamba kila mkoa!

Kwa wadhifa wake, viwanja na mashamba hapati bila kuwatumia maafisa ardhi. Kama ni hivyo, atawezake kuwakemea wanapokuwa wamekosea? Ndo maana matatizo hayaishi!! Waziri ana viwanja Mwanza, Iringa, Arusha, Dar, etc. Lengo ni nini? HAta kama ni haki yake kama raia, ni vibaya kumiliki rasrimali kwa urafi kiasi hicho! Waziri ukishakuwa mrafi, nani akuamini? Ndo maana kila mtu anatamani kumuona rais. Hawa wasaidizi wake ni urafi uliokithili!!
 
MTU ana Jazba ya kuona kuwa anadhulumiwa, waziri alipaswa kuwa Humble na kumvumilia Mwananchi na angempa muda Wa kumsikiliza ili amwelewe.

Badala yake nilichoona ni Waziri anajimwambafai tu, ila Hamna kitu kabisa..
Kila kiongozi wetu anajiona ni mtu mkubwa kuliko raia yoyote! Angekuwa anawapa heshima raia kama yeye anavyoitaka, angevumilia kusikiliza.
 
Mimi naona waziri yupo sahihi kwasababu huyo mzee ameanza kuweka title ya mzee wake ili asikilizwe, badala ya kuweka taarifa zinazoonesha anastahili hiyo ardhi.

kwanini aanze mimi ni mtoto wa muasisi wa Tanu?....Waziri ameogopa kuonekana anapendelea watu ambao ni waasisi wa nchi.

Waziri yupo sahihi japo kuna sehemu amekosea anaelekezwa anakuwa kama hataki kusikiliza hiyo inatokana na jamaa kuwa kama amemdharau
 
Back
Top Bottom