bulicheka 4
JF-Expert Member
- Mar 22, 2020
- 915
- 1,019
Lukuvi ni corrupt na ni mzandiki wa kupuuzwa naapa atapata tabu sana kwa dhuluma zake Mzee wa watu na hati inayo paswa ku renew anamwambia akafungie vitumbua tena mbele ya kadamnasi
Tatizo clip haijaanza mwanzo kabisa, Ila Kuna watu hawawezi kuzungumza bila kufoka, inawezekana ndivyo alivyo, yote kwa yote Kama Kiongozi inapaswa kuwa mwenye hekima Ili uweze kuendana na watu woteMimi naona waziri yupo sahihi kwasababu huyo mzee ameanza kuweka title ya mzee wake ili asikilizwe, badala ya kuweka taarifa zinazoonesha anastahili hiyo ardhi.....
kwanini aanze mimi ni mtoto wa muasisi wa Tanu?....Waziri ameogopa kuonekana anaoendelea watu ambao ni waasisi wa nchi......
waziri yupo sahihi japo kuna sehemu amekosea anaelekezwa anakuwa kama hataki kusikiliza hiyo inatokana na jamaa kuwa kama amemdharau
Ulevi wa madaraka na ushamba unamsumbua mheheHuyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.
Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.
Mitano tena!
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.
Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.
Mitano tena!
Naye lakini ana kosa, kwa nini aanze kutambia uasisi wa babake? Kwani kama angeeleza kwa staha ingekuwaje?..huyo mwananchi ana HAKI ya kusikilizwa.
..nimesikitika jinsi Waziri alikataa kumsikiliza.
..kwasababu mwananchi alikuwa moto, waziri alipaswa kuwa baridi.
Makosa mawili hayafanyi kosa moja likawa sahihi, sasa yeye angechukulia ni udhaifu au kuathirika kisaikolojia kutokana na kuhisi hajapata haki yake na kwa miaka mingi.Naye lakini ana kosa, kwa nini aanze kutambia uasisi wa babake? Kwani kama angeeleza kwa staha ingekuwaje?
Rais mwenyewe Jiwe? Hana urafiki muulize mwanafunzi wake Kenge LugolaWaziri hakutakiwa kujibu kwa kejeli "nenda kamuone Raisi", hii lugha haijakaa vyema, hata kama ni mna urafiki bado atabaki kuwa Rais.
Anamwambia mwananchi kuwa hamuogopi Rais, alitaka aende ila yeye hamsikiliziLakini kwa nini Lukuvi hakutaka kumsikiliza? Usanii umegonga mwamba. Halafu lukuvi anasema "nenda kamuone Rais" ... hasira imemponza
Labda yeye ana urafiki wenye mizizi zaidiRaisi mwenyewe Jiwe? Hana urafiki muulize mwanafunzi wake Kenge Lugola
Na unasemaje kuhusu Rais kutamani kila kitu kiwe Chato!Ndo maana kila mtu anatamani kumuona rais.
Kwa wadhifa wake, viwanja na mashamba hapati bila kuwatumia maafisa ardhi. Kama ni hivyo, atawezake kuwakemea wanapokuwa wamekosea? Ndo maana matatizo hayaishi!! Waziri ana viwanja Mwanza, Iringa, Arusha, Dar, etc. Lengo ni nini? HAta kama ni haki yake kama raia, ni vibaya kumiliki rasrimali kwa urafi kiasi hicho! Waziri ukishakuwa mrafi, nani akuamini? Ndo maana kila mtu anatamani kumuona rais. Hawa wasaidizi wake ni urafi uliokithili!
LOoo, nimekukubali.Ukiitizama hii video kwa makini ukiwa neutral kabisa utagundua huyo mwananchi ana changamoto kidogo ktk akili yake,hana utulivu kabisa.
Ndg Lukuvi alipaswa kuwa mtulivu kwa kuliona hilo angeahirisha kumsikiliza kwa kumuambia tu kwa utulivu wewe jambo lako ni zito tuonane pale ofisini.
Akija ofisini unachukua mabarua yake hayo unamuambia kaa hapo kunywa chai usizungumze,unazisoma ukielewa unatoa uamuzi.
Uongozi ni pamoja na uvumilivu wa kumudu personality za Watu.