Mwenye uzoefu na Marekani msaada nahitaji

Upo sahihi mkuu unachotakiwa ni kutoa njia kwa vijana wafanye nini ili wafike huko na kuishi bila kuvunja sheria kama unajua kama haujui tulia tuu watapata njia maana hakuna lisilowezekana wala msiwakatishe tamaa kabisa...

Kuna mtu kaomba kujua process ya kupata immigrant visa. Nimempa "from the horses mouth".

Mimi baharia ingawa wa nchi kavu na sikuwepo ughaibuni enzi za mtoto wa Gorbachev Vale wa Pereas, lakini nishawahi kusaidia mpaka watu waliofika nchi za watu kibichibichi hawana sehemu za kufikia miji mikubwa, kwa hiyo habari za kuoneshana njia kwetu ni utamaduni, hata kwetu Dar Wasukuma waliokuwa wanakuja mara ya kwanza mjini hawana pakufikia walifikia sana.

Sina roho ya Kangi Lugola, ningekuwa na roho hiyo ningekuwa bongo nasota bado.

Kwa hiyo kupigiana mapande watu kusafiri si kitu ambacho sikijui. Ila nasisitiza tu dunia imebadilika, zile safari za kiskauti skauti za 1997 mpaka 2000, enzi ya kabla ya 9/11 masharti nafuu kujichanganya rahisi, kwa sasa hata ukifika US, bila makaratasi ya kueleweka sisemi huwezi kufanikiwa, kuna vichaa kibao wanakomaa, ila utapata tabu sana na unaweza kuona tabu hazina maana, au ukaishia jela.

Kwa hivyo sitaki kuonekana navunja watu moyo.

Tunahitaji kuongeza wanajeshi huku.

Ila safari inabidi ipangwe kwa akili na si kukurupuka,unaweza kufanya mistake moja tu katika mipango yako ikaku cost siku zote.
 

OK vizuri nachosisitiza zile njia unazoziona ni rahisi kwao kutoka toa madini vijana waje na wewe unapata Baraka kwa kufanya hivyo najua unafanya hivyo maana ndio tabia zetu wasafiri amini ninachokuambia watu wengi wanajua kusafiri hasa kuja USA ni ngumu sana kumbe njia zinabadilika kila kipindi hasa kwa wanaoishi huko ndio wanajua njia maana wanapokea wageni kila kukicha...
 
Nimependa sana ulivyomjibu. Kuna wadau humu wanasahau kuwa tunatofautiana uelewa na kumkashifu.
 
Nimependa sana ulivyomjibu. Kuna wadau humu wanasahau kuwa tunatofautiana uelewa na kumkashifu.
Kumdharau mtu usiyemjua wala kujua mchango wake katika jamii ni kitu kibaya sana, moja ya sababu ya umasikini wetu.

Mimi napenda kuongea na washua fulani waliokaa kwenye system na wanaojua dunia inavyoenda ili kuchota busara zao.

Nilikuwa naongea na mshua mmoja wa siku nyingi, kasafiri dunia nzima kwa shughuli za kiserikali. Nikawa namuuliza kuhusu hizi attitudes za serikali ya Tanzania kuhusu kuwekeana ngumu kwenye safari (hii ilikuwa kabla ya Kangi Lugola kusema maneno yake kuhusu human trafficking, so it was not about that).

Mshua akawa anasema tuna historia ya ujamaa iliyotufanya tuwe na mamabo haya, pia tuna wivu wivu wa kijinga sana. Amenieleza kwamba hata enzi zao kwenye East Africa Community Wakenya na Waganda walikuwa wanasaidiana sana kukitokea nafasi za kwenda nje kusoma na kutafuta maisha, Tanzania ukijulikana unafanya mipango ya kwenda nje unaonekana kama msaliti.

Baadhi ya hizi attitudes zipo mpaka leo, na hata kama naelewa officially Kangi Lugola anaongelea kuhusu human trafficking, a legitimate issue, unofficially hizi checks zinatumika ku frustrate watu wenye legitimate reasons kusafiri.

Mimi kwetu tuna historia ya kusaidiana muda mrefu sana, kuna watu wamepata kufanya shughuli za maana sana hapo mjini Dar, wamepitia kwetu.Wamekuja mjini hawana pa kufikia lakini kwa sababu ni jirani, rafiki, rafiki wa rafiki huko nyumbani bush, wamepatia sehemu ya kuanza maisha Dar, angalau pa kufikia, halafu, wakajichanganya kivyao.Leo na wao mabosi wakubwa na wao wamesaidia familia zao na watu wengine wengi. Maisha ni kusaidiana.

Sasa mtu niliyekua huku nayaona haya, maisha yangu tu nilivyokua na kuona wazee wangu wanaishi hivi ni fundisho kubwa kwamba usimdharau mtu anayehitaji kuoneshwa njia leo, muoneshe halafu mpe nafasi apigane mwenyewe, akishindwa, wewe ushafanya sehemu yako ya kumuonesha njia, akishinda, hiyo ni habari nzuri.
 
Ndio Mkuu Nimekuelewa Ahsante Sana
 
Mkuu kuhusu kuka kihalali usiwe na hofu sina mpango wa kuingia kwa njia zisizo halali na ninaona mnaongea Sana kuhusu visa pia ondoen hofu visa yenyew watatoa tu hiyo hainitii hofu ila nilikua t nataka nijue ni sehemu gani nzuri ya kufikia na upatikanaji wa kazi ni mziri coz ukiingia kiharam hata upatikanaji wa kazi ni utakua mgumu
 
Well said...inawezekana mtu ana ambitions but uwe na proper plan...us sio mahΓ li pa kukimbilia. ...home is best.
 
Unajua dola 2000 wewe???
Au unaongea tyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…