Mwenye ushahidi wa dhahiri juu ya ufisadi wa Lowassa aweke hapa hadharani! Tuache porojo!

Mkandara unakwenda nje ya mada. Wanaosamehewa ni wavunjaji sheria.Nipe ushahidi kwamba Tume ya Mwakyembe ilitaka kumhoji Lowassa akakataa?Hizo zingine ni assumptions tu Mkuu. Pinga au kosoa lakini kwa ushahidi Mkuu Mkandara. Swali lako kuhusu miaka ya 1970 nafikiri limejibiwa. Haiwezani Mwalimu Nyerere amuulize mwanafunzi Lowassa swali unalotaka tuamini alimuuliza kuhusu utajiri wake.
 
Mkandara kweli mkuu unataka ujibiwe swali la miaka 1970? Ndio uzushi ninaouzungumzia huo.Mwaka 1971 Lowassa alimaliza form four.Alikutana wapi na Mwalimu Nyerere na kumuuliza kuhusu utajiri wake? Alikuwa ana post gani kitaifa miaka ya 1970?Mpaka aulizwe? Mkandara mkuu huwa na admire uwezo wako wa kuchambua mada lakini na wewe umebebwa na kimbunga cha uzushi bila hata kujiuliza. Is it possible? Ni kweli ?
Alaa kwani katika sifa za Lowassa zinaanzia wapi? sii huko alikoanzia.. maana hapa tunajadili Utajiri wake aliupata vipi na sio muendelezo wa Utajiri wake. Hata kwa yule anayesifiwa kwa unachama nadhani tutaanza kuzungumzia mwaka gani kajiunga na hapo ndipo tutasema jamaa ni mwachama asilia..
 
Hapa ndio uwanja wa kumwaga ushahidi kuhusu huo ufisadi wake, ili na sisi tusiofahamu, tujiepushe naye!
Sasa mmepewa nafasi badala ya kuitumia, mnaanza porojo tena!

Ushahidi tunao wa kutosha. Mkandara kaweka link hapo inayohusu ripoti ya Mwakyembe someni. Ushahidi wa nyaraka tulionao hatutaweka hapa JF kwa sbb tunamsubiri aingie kwenye anga zetu ndio tumuumbue vizuri. Tutamsurubu vzr kwenye anga zetu. Sisi duruni kwetu fitina mwiko, tutasema kweli daima bila kumuonea mtu soni wala haya
 
LOWASA anajinadi mtu wa maamuzi magumu. Swali langu.
1.Watanzania tulikaa gizani kwa miezi 6 tangu kusainiwa kwa mkataba wa Richmond.
2. Kipindi chote cha miezi 6 ya mkataba Richmond haikutekeleza chochote cha mkataba.
3. Mbaya zaidi Richmond walishindwa hata kuleta hata msumari nchini
4. Serikali chini ya kaka Mkuu LOWASA ilisimamia huyu Richmond alipwe pesa hata bila ya kudeliver chochote.
5. Itakumbukwa bwana Mkubwa huyu LOWASA aliweza kuvunja mkataba na city water, pia alimfukuza kazi mhandisi kwenye mkutano wa hadhara.

Ishu hapa kwanini LOWASA aliufyata kufanya maamuzi magumu kwa Richmond???
Hivi maamuzi magumu ya LOWASA ni yepi???

Tumaamini kuwalaza watanzania gizani kwa miezi sita uku tukilipa mil 150 kwa siku ni maamuzi magumu pia.

Ni maadili gani hayo ya kutaka kutunishiana misuli na mwl wako WA darasa/ ni heshima hiyo?/ au ni utovu WA nidhamu!
 
Ushahidi tunao wa kutosha. Mkandara kaweka link hapo inayohusu ripoti ya Mwakyembe someni. Ushahidi wa nyaraka tulionao hatutaweka hapa JF kwa sbb tunamsubiri aingie kwenye anga zetu ndio tumuumbue vizuri. Tutamsurubu vzr kwenye anga zetu. Sisi duruni kwetu fitina mwiko, tutasema kweli daima bila kumuonea mtu soni wala haya
Kamati ya Mwakyembe iliwahi kumuhoji LOWASSA kuhusu huu mnaouita "ufisadi" wake?
 
Mkandara unakwenda nje ya mada. Wanaosamehewa
Mkuu siendi nje ya mada ila nyie ndio mnanitoa kwa kusema Nixon alisamehewa. kwani kusamehewa kunamuondoa makosa ya kuvunja miiko na maadili? Hata kama asingefungwa Jela ama angeshinda kesi ile, bado Nixon alivunja miiko na maadili hivyo asingeweza kuendelea kuwa rais. Nia na madhumuni yangu ni kuwaonyesha kwamba kuna tofauti kati ya kuvunja miiko na maadili ya uongozi na kesi za jinai(Uongozi vs raia) hivi ni vitu viwili tofauti. Akiwa kiongozi Lowassa alikabiriwa na tuhuma za UFISADI na hujuma aloifanya ni UFISADI ambao alilazimika kujiuzuru - Kwisha!
 
Kamati ya Mwakyembe iliwahi kumuhoji LOWASSA kuhusu huu mnaouita "ufisadi" wake?
Kamati hailazimiki kumhoji mtu, isipokuwa Bunge lingeweza kuwaita wahusika wote wakahojiwa kama tungekuwa na Utaratibu huo. Nchi za wenzetu zinao utaratibu huo yaani kamati ya miiko na maadili inakuwa ni kamati ya Bunge maamuzi mengi yanafanywa na rais mtawala. Sisi hatuna muundo unaolipa Bunge meno ya kuwawajibisha viongozi na ndio maana tunahitaji Katiba Mpya.
 
kama sio lowasa anaye husika aliyehusika ..ni nan..na wiz wa richmond tutajiwe.....
 
Chombo kinachotakiwa kumsafisha Lowassa ni mahakama pekee.Na kwasababu watu wanalindana sana,ndo maana huwezi kusema EL hakuhusika kwenye Richmond.Na pia angalia,karibia wote waliotangaza nia CCM wanatuhuma mbalimbali.Sasa utawezaje kusema Lowasa ni safi?!!!
 
Nixon alisamehewa kwa kosa la jinai Mkuu. Tuwekee ushahidi wa hizo tuhuma. Naona utajiri wake wa 1970 sio kipaumbele tena kwani najua umejua ni uzushi. Tuhuma si zinaweza kuwa za uongo au kutengenezwa. Kwani Mkandara nikikutuhumu ndio kusema tuhuma zangu kwako ni kweli kwa sababu nimekutuhumu? Si lazima nilete ushahidi wa ku back up tuhuma zangu?
 
Kati ya watia nia wanaoshambuliwa zaidi kwa propaganda mfu ni Lowassa. Kuna mambo mawili yanayomfanya ashambuliwe sana. Moja, ni utajiri wake na pili, ni watendaji wa 'business as usual'!

Karibu watia nia wengi (sio wote) waliojiotokeza CCM hadi sasa wamewahi kupatwa na dhoruba za kisiasa kwa namna moja ama nyingine! Lakini hili la richmond la Lowassa limekuwa ruba! Kwa maneno mengine richmond inafanywa moja kwa moja kama vile ni mradi wa Lowassa, kiasi kwamba Lowassa anapachikwa jina la fisadi japo hakuna ushahidi wowote ulio dhahiri!

Mwenye ushahidi wowote ule wa uhusika w Lowassa kwenye ufisadi wowote ule hapa nchini auweke hadharani ili tukate mizizi ya fitna!

=========
Updates
=========

Hadi page ya nne hakuna ushahidi wowote uliopatikana ni ngonjera za team watia nia tu!

Endeleeni kungonyerika nitakuja kutoa updates za pages zingine zitakazofuata!

Lakini fahamu hizi tips kwa wewe usiefahamu.

1. Lowassa asingejiuzulu kama utajiri wake ni wa mashaka. Angebaki kung'ang'ania uwaziri mkuu kwa maslahi mapana ya utajiri wake

2. Serikali ni kubwa na yenye nguvu zaidi kuliko Lowassa. Utajiri wa Lowassa ulianzia enzi za Baba wa Taifa, kama Lowassa angekuwa na utajiri wa mashaka, Baba wa Taifa angeshamtia ndani muda mrefu sana.

3. Kuna mawaziri waandamizi waliowahi kuwa na kesi mahakamani kuhusu masuala ya ufisadi mfano Mramba, Idd Simba na wengine wengi lakini Lowassa hajawahi kuwa na kesi hata ya kuzingiziwa. Usifikiri serikali inamuogopa Lowassa!

4. Lowassa alijiuzulu kwa dhana nzima ya uwajibikaji na kulinda chama chake na serikali yake. Angeweza kukomaa na uwaziri mkuu kama wengine wanavyokomaa mfano Mh Pinda (Operesheni tokomeza ilidunda kwa Pinda, Escrow ilidunda kwa Pinda, Mauaji ya albino ilidunda kwa Pinda, Kauli ya wapigwe tu maana hakuna namna ilidunda kwa Pinda, nk).

=======
updates
=======

Uzi upo page ya tano. Bado hakuna ushahidi. Bado ngonjera ni zilezile kama za from page 1 to 4.

=======
updates
=======

Hii post ni ya Mkandara nimeitoa page ya tano. Nimeileta hapa juu makusudi ili niweze kuitendea haki na jamii yote ijifunze kwa upana wake!

Swali:
------

=====
Jibu
=====
Kama hivyo ni kwanini tume ya mwakyembe haikumhoji kuhusu hili? Balance ya story hii iko wapi???? Kwani Lowassa ahojiki mbona hakuohojiwa ili aeleze in and out?

Ahsante sana kwa maswali yako mazuri. Hope, hapa umefunguliwa mwanga wa mengi kuhusu Lowassa. Karibu sana!

=======
updates
=======

Hizi ndio baadhi ya posts za ushahidi:

Lowassa asitupotezee muda watz. Rubbish, sweep and throw in the bin
 
Kamati ya Mwakyembe iliwahi kumuhoji LOWASSA kuhusu huu mnaouita "ufisadi" wake?

Hawakumhoji. Lkn ktk link ya M.M Mwanakijiji, Dr.Mwakyembe anaeleza vzr kabisa kwa nini hawakufanya hivyo. Sikiliza vizuri maelezo yanajitosheleza kabisa. Lakini kikubwa walikuwa tayari wameshapata ushahidi wa kutosha kabisa kutoka kwa wasaidizi wake kiasi cha kwamba hakukuwa na haja tena ya kumhoji yeye hasa kulingana na nafasi yake. Hata hivyo, kamati ya Mwakyembe haikumwambia Waziri Mkuu ajiuzulu au awajibike, bali ilimwambia kuwa ajipime na kuona mwenyewe kama anastahili kuendelea kutumikia nafasi hiyo au la. Yeye akaamua kujiuzulu ili mambo yaishe au mjadala uishe
 
Akiwa ni kiongozi msafi siyo fisadi, anapata wapi pesa za kununua nyuma nje ya nchi na ndani ya nchi!? Anapata wapi pesa za kujisafishia makanisani na misikitini!? Kama siyo fisadi kwanini alilipa gharama za kuwasafisha kutoka mikoa mbalimbali macadre waliohudhuria siku yake ya kutangaza nia!? Kama yeye siyo fisadi ni msafi na ni tajiri kwanini anatumia gharama kuingia ikulu!? Anataka aingie ikulu kwa faida ya nani!? Kama cyo ana agenda mbaya, kama anataka kuiletea Tanzania neema kuna haja gani ya yeye kutumia team na pesa!? Haiingii akilini hiyo
 
Mbinu zinatumika hata hizi za kuja jamiiforums kwa kufikiri lbda yataanikwa hapa.

Tatizo lingine ni kwamba je itakuaje endapo Edward atashindwa kupita kwenye mchujo maana amejitahidi sana kuwekeza makanisani, misikitini na hata kwenyevijiwe vya waendesha vibajaji, patamu hapo.

Je wafadhii watachukulia kirahisi kushindwa huko au watafsnya hila mahala fulani?
 
Nixon alisamehewa kwa kosa la jinai Mkuu. Tuwekee ushahidi wa hizo tuhuma. Naona utajiri wake wa 1970 sio kipaumbele tena kwani najua umejua ni uzushi. Tuhuma si zinaweza kuwa za uongo au kutengenezwa. Kwani Mkandara nikikutuhumu ndio kusema tuhuma zangu kwako ni kweli kwa sababu nimekutuhumu? Si lazima nilete ushahidi wa ku back up tuhuma zangu?
Mkuu mimi najibu tu hoja ya mwanzisha mada ambaye kasema moja ni Utajiri wake. Utajiri wa Lowassa umeanza toka miaka hiyo 1970s na nimeweka aloziweka tuhuma hizo, mwalimu Nyerere, hivyo yeye Lowassa atueleze alipataje Utajiri huo miaka hiyo wakati akiwa mtumishi wa serikali? Sii anataka kuwa rais bana, kwani kuna ubaya gani akijisafisha na tuhuma maana hutakiwi kuongoza nchi na tuhuma ambazo wewe unazikana. Utajiri hua na mwanzo na ndio maana nikaweka swali hilo!
 
Kamati hailazimiki kumhoji mtu, isipokuwa Bunge lingeweza kuwaita wahusika wote wakahojiwa kama tungekuwa na Utaratibu huo. Nchi za wenzetu zinao utaratibu huo yaani kamati ya miiko na maadili inakuwa ni kamati ya Bunge maamuzi mengi yanafanywa na rais mtawala. Sisi hatuna muundo unaolipa Bunge meno ya kuwawajibisha viongozi na ndio maana tunahitaji Katiba Mpya.
Lowassa angekuwa anahusika na Kashfa ile, angeweza "kukomaa" na uwaziri mkuu wake na bado pasingekuwa na mtu wa kumwajibisha, ila aliachia ngazi ili kuwaridhisheni nyie wachache mliodhani kuwa naye pia ni mhusika.Ili mpate faraja kwa muda tu. Pinda "amekomaa" na mangapi na mpaka leo anadunda? Sasa Lowassa anakuwa Rais wa TANZANIA, haya yote aliyashayasemehe!
 
Back
Top Bottom