Mwenye ushahidi wa dhahiri juu ya ufisadi wa Lowassa aweke hapa hadharani! Tuache porojo!

TUACHE HABARI AMBAZO HAZINA MAANA YOYOTE ILE MWENYE TAARIFA SAHIHI JUU YA UHUSIKA WA MOJA KWA MOJA WA MH LOWASSA.
TUNAKUOMBA UTUWAKEE HAPA TUJIRIDHISHE KUROPOKA KWA WATOTO WA KIUME HAKUPENDEZI/ LETS TALKS WITH DIRECT EVIDENCY/i
 
Mzee Alhaji Mwinyi alijiuzulu akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani .Je ni yeye aliyefanya mauaji Shinyanga? Kumbukeni bado alikuja akawa Rais wa Awamu ya Pili maarufu kama Mzee ruksa.
hakuna mahala Mwinyi alikataa kuhusika, Kiongozi yeyote anayekubali uwajibikaji kwa jambo lolote lililotokea ndani ya usimamizi wake ni hatua moja ya uongozi bora. Japo Mwinyi hakutoa amri ya mauaji hayo lakini alilazimika kujiuzuru kwa sababu matukio ya Polisi yalikuwa chini ya wizara yake hakufanya maamuzi kama Lowassa alopendekeza Richmond ipewe tender badala ya mashirika mengine akielewa kabisa kwamba Richmond ni shirika la kuchapisha vitabu. Inabidi tuwaelimishe ya kwambaa UFISADI maana yake ni UHALIBIFU wa aina yoyote sii lazima uwe wizi wa fedha - KUHUJUMU UCHUMI ni Ufisadi pia.
 
TUACHE HABARI AMBAZO HAZINA MAANA YOYOTE ILE MWENYE TAARIFA SAHIHI JUU YA UHUSIKA WA MOJA KWA MOJA WA MH LOWASSA.
TUNAKUOMBA UTUWAKEE HAPA TUJIRIDHISHE KUROPOKA KWA WATOTO WA KIUME HAKUPENDEZI/ LETS TALKS WITH DIRECT EVIDENCY/i
Toka lini raia wakaombwa ushahidi? kwani hiyo kazi yao kusaka ushahidi. Tume ya Mwakyembe ilikwisha tupa ushahidi yeye aukane!.
 
Misibishane kwa mambo yasio na maana,anaetakiwa kudhibitisha hilo ni yeye mwenyewe Lowasa,Kama hakuhusika na Richmond,amtaje muhusika ili tumjue,sio Ana babaika tu,amtaje ili ajiweke guru,ukweli umuweka MTU huru.

Hiyo logic ya wapi?Anayezushiwa ndio athibitishe? Mantiki yako ni kwamba mtu akituhumiwa upande wa mashtaka unamwambia thibitisha tuhuma sio za kweli. Au unatafuta ushahidi wa tuhuma hizo.Hizi ni tuhuma zisizo na maana. Ni uzushi tu.Wekeni ushahidi mhusika ni nani kama upo.
 
Kwani Lowassa kuwa mtumishi wa umma ni dhambi kua tajiri? watumishi wangapi wa umma, tena wa nafasi za chini kbs wanafanya na biashara na wanakuwa vzr kiuchumi? Richmond mnaikuza na kufanya as if ndo issue ya kumchamfua Mzee.

Sio kosa lako, Kampuni kulipwa milioni 150 kwa siku na watanzania wakaendelea kuteseka na kukosa umeme miaka sio jambo dogo.

Au 2007 ulikuwa bado shule ya msingi? maana kila aliyekuwa na uelewa anajua alichofanya Lowassa. Uongozi tanzania ni mtamu mno, hakuna kiongozi anayejiuzulu kirahisi rahisi tu. Huyu aliwekwa kona mbaya, na CIA walishaieleza Serikali uhusika wake. Kwani alichofanya kosa ni kuihusihsa Marekani kwenye utapeli wake. Anuani ya Richmond huko Texas ilikuwa ni defunct printing business, sio kampuni ya kuzalisha umeme. Kwa lugh rahisi, Ndugu Lowassa alitengeneza kampuni hewa kupitia madalali wake ili kupiga hela za serikali. Na kuonesha hana aibu kwenye wizi, asilimia kubwa ya matapeli walio bize kuiibia serikali yetu kila ikisinzia wako naye bega kwa bega, kuanzia Rostam, Chenge, Karamagi, Tibaijuka na wengine wengi. Hiyo listi sio wapuuzi, wanajua mzee mpigaji ndio msalie mtume yao, kwani akiingia ikulu wanaanza upya kupiga.

usione wanaiita safari ya matumaini, ni matumainii ya wachache ya kuendelea kutuibia.

Yani huyu CCM kumpitisha ni kujitafutia kazi zisizo za ulazima za kupita nchi nzima kumsafisha,kwa pesa nyingi sana na ahadi tele. wakimaliza kumsafisha ndio waanze kumuombea kura. Nilishasema CCM wakimpitisha huyu Tapeli Lowassa, halafu UKAWA wakashindwa General Election, watakuwa mabwege wa mwisho duniani.
 
Mkandara ushahidi upi huo wa Tume ya Mwakyembe uliomzungumzia Lowassa personally?Tuwekee hapa.
Soma report ya Tume ya Mwakyembe. Kumbuka nyie mnadai ushahidi katika jambo la maadili. kama Lowassa angefikishwa mahakamani kwa makosa ya wizi ama kuhusika na wizi hapo mngedai ushahidi lakini katika swala la maadili ni maamuzi ya kiongozi kinyume cha maadili na ushahidi ni maneno yake, saini yake, amri yake ama kushindwa kusimamia utendaji ipaswavyo. Hivyo ushahidi upo katika mambo yote yanayohusu shirika gushi kupewa tender kwa njia za mkato! (report ya tume). Kiongozi anayekiuka miiko na maadili sio lazima awe mwizi, Nixon alitondolewa madarakani kwa njia hiyo.
 
Mkandara ushahidi upi huo wa Tume ya Mwakyembe uliomzungumzia Lowassa personally?Tuwekee hapa.
Pengine cha kushangaza zaidi ni CCM kuweza kukubali watu waliokiuka miiko na maadili ya Uongozi kwa KUHUJUMU UCHUMI wa nchi hii kuchukua fomu ya kugombea Urais!
 
Niliwahi kusema kuwa chuki na ghiliba za kisiasa plus interest za nchi kubwa za Dunia hii ndo zinapelekea Lowassa kuundiwa zengwe ... bahati mbaya sana Watanzania wa leo wanaongozwa kwa hisia na si facts ... Lowassa ndo kiongozi pekee mwenye kujua deals za maharamia na kutumia Rasilimali zetu kwa manufaa ya wananchi!! Kuna watu wanakinga kiasi kikubwa sana cha fedha kutoka Egypt via USA ili kutunza maji ya Lake Victoria... Watanzania tulinyimwa kutumia maji hayo; waliokuwa wanapewa fedha za kuchimba visima virefu walikuwa wanakula... Ilipotokea Lowassa ametekeleza mradi wa KASHWASA jamaa wakaona sana deal lao limevurugwa ...!!! Watanzania kuweni Makini sana na hawa EHM mnao waona Wazalendo! Jiulize kwanini ESCROW ya akina Membe, Pinda, Nchemba et al Imepoozwa na kuonekana Fitna za Richmond ndo ya Ukweli ?.... Itoshe kusema Lowassa tunamuhitaji kuliko yeye anavyohitaji kuwa Rais wetu ...
 
Lowassa alikiuka maadili yepi? Kujiuzulu? Mbona Mwinyi aliwajibika? Ukweli umedhihirika kuwa Tatizo ilikuwa uwaziri Mkuu .. period!!! Richmond, Dowans, Symbion ni ile ile ... hadi Clinton na Obama walipokuja ndo mkanyamazishwa kama kibatari ... Crystal Clear ninyi watu wa Vatican mnashida ...mnajiona wabora sana mbele ya wengine wakati ninyi ndo MAFISADI PAPA ...
Soma report ya Tume ya Mwakyembe. Kumbuka nyie mnadai ushahidi katika jambo la maadili. kama Lowassa angefikishwa mahakamani kwa makosa ya wizi ama kuhusika na wizi hapo mngedai ushahidi lakini katika swala la maadili ni maamuzi ya kiongozi kinyume cha maadili na ushahidi ni maneno yake, saini yake, amri yake ama kushindwa kusimamia utendaji ipaswavyo. Hivyo ushahidi upo katika mambo yote yanayohusu shirika gushi kupewa tender kwa njia za mkato! (report ya tume). Kiongozi anayekiuka miiko na maadili sio lazima awe mwizi, Nixon alitondolewa madarakani kwa njia hiyo.
 
Soma report ya Tume ya Mwakyembe. Kumbuka nyie mnadai ushahidi katika jambo la maadili. kama Lowassa angefikishwa mahakamani kwa makosa ya wizi ama kuhusika na wizi hapo mngedai ushahidi lakini katika swala la maadili ni maamuzi ya kiongozi kinyume cha maadili na ushahidi ni maneno yake, saini yake, amri yake ama kushindwa kusimamia utendaji ipaswavyo. Hivyo ushahidi upo katika mambo yote yanayohusu shirika gushi kupewa tender kwa njia za mkato! (report ya tume). Kiongozi anayekiuka miiko na maadili sio lazima awe mwizi, Nixon alitondolewa madarakani kwa njia hiyo.

Maelezo yako yapo vague.Nixon aliondolewa madarakani kwa kujua na kuficha uvunjaji wa sheria. Ofisi za chama cha Democrats zilivunjwa na FBI ikafanya uchunguzi na ushahidi ukapatikana na watu walioshiriki wakapatikana. Ushahidi huo wa kuhusika kwa Nixon ndio kulifanya ajiuzulu akiogopa kuwa impeached. Turudi kwetu umesema maadili. Tupeni ushahidi usio shaka na sio hearsay kwamba Lowassa alishiriki personally?
 
umerudi team lowasa mana jana ulitamka kuwa haupo tena team lowasa au ndo unataka ukanywe nae chai?
Hebu weka hilo Tangazo hapa! Mzushi mkubwa wewe, mimi mpaka sasa naamini kuwa hakuna mwingine anayefaa kuwa Rais zaidi ya LOWASSA, na ndiye Rais ajaye!
 
Maelezo yako yapo vague.Nixon aliondolewa madarakani kwa kujua na kuficha uvunjaji wa sheria. Ofisi za chama cha Democrats zilivunjwa na FBI ikafanya uchunguzi na ushahidi ukapatikana na watu walioshiriki wakapatikana. Ushahidi huo wa kuhusika kwa Nixon ndio kulifanya ajiuzulu akiogopa kuwa impeached. Turudi kwetu umesema maadili. Tupeni ushahidi usio shaka na sio hearsay kwamba Lowassa alishiriki personally?
Mkuu swala la Nixon ni kutokana na kukiuka miiko na maadili ya Uongozi, japo hazifanani kwa uhujumu wenyewe lakini pengine pitia hapa ujue kilichotokea. Kukiuka miiko na maadili hakuhitaji ushahidi wa mahakamani..Ushahidi soma report ya Mwakyembe Hapa niseme nini zaidi. Lowassa aliwajibika kutokana na kuhusika kwake na sakata la Richmond - kwisha..
 
Back
Top Bottom