Mwenye ushahidi wa dhahiri juu ya ufisadi wa Lowassa aweke hapa hadharani! Tuache porojo!

Mkuu vuta subira kidogo tu, hili la RICHMOND liliwekwa kiporo pale sheikh Kaluta kwa sababu maalum, ila nina imani kubwa kuwa LOWASSA atateuliwa na CCM kuipeperusha bendera ya chama, hivyo katika muendelezo wa safari hii ya matumaini RICHMOND itaibuka tu, na ukweli wote utadhihirika!
Mkuu wewe unataka nini zaidi ikiwa Lowassa mwenyewe kakubali mbele ya waandishi wa habari akimjibu Manyerere (tazama video yake) amekiri kwa kujisifia kuwa mradi ule ulikuwa safi kabisa na mitambo ilikuwa state of art ulosifiwa na rais wa Marekani wakati hata hilo kadanganya, unataka nini zaidi?. He confessed on record nakala tunayo.

Hizi sio tuhuma ni KASHFA za kiongozi na hakuna mahala alipopinga kwamba hahusiki na zaidi ya hapo alikuwa waziri mkuu alopitisha mkataba ule wapewe nani..Nukuu kibao katika report ya tume unataka nini zaidi? JK sio mjinga wa Kuachia report ile ilopelekwa kwake kwanza aje airuhusu ipelekwe bungeni wakati inamhusu yeye. Jk alijua fika Lowassa kahusika na alimwambia ajiuzuru mapema kabla halijafika mbali. Alitumia uungwana wake leo mnataka kubadilisha na hata kuwatisha familia yake ati mkiingia madarakani watakiona cha moto jamani, jamani kuweni na utu japo kidogo.
 
Lowassa ndiye mtaji kwa CCM kwani ndo mwanasiasa mwenye social capital kubwa kuliko wote kwa sasa. hii ni pamoja na upinzani. Mbowe mwenyewe anathibitisha hilo

Umasikini wa watanzania hauondolewi na social capital nyie punguwani wahed(courtesy of FaizaFoxy ), unaondolewa na sera madhubuti,watanzania wamekaa mkao wa kula kusubiri sera, nyi mnaleta hadithi za paukwa pakawa, matumani yameenda yamerudi.

Sasa kama tunachagua umaarufu kwenda ikulu si tungemchagua Diamond platnumz, maana yeye ni maarufu ndani na nje ya Tanzania.

Tunachagua kiongozi, sio social capital
 
Last edited by a moderator:

Duh Ahahaha! hii kali kushinda tena tumwambie Diamond amrudie Wema ndio itashika moto kabisa itambidi Lowassa naye atoe CD yake ya kibau ukata...
 
Kati ya watia nia wanaoshambuliwa zaidi kwa propaganda mfu ni Lowassa. Kuna mambo mawili yanayomfanya ashambuliwe sana. Moja, ni utajiri wake na pili, ni watendaji wa 'business as usual'!

Karibu watia nia wengi (sio wote) waliojiotokeza CCM hadi sasa wamewahi kupatwa na dhoruba za kisiasa kwa namna moja ama nyingine! Lakini hili la richmond la Lowassa limekuwa ruba! Kwa maneno mengine richmond inafanywa moja kwa moja kama vile ni mradi wa Lowassa, kiasi kwamba Lowassa anapachikwa jina la fisadi japo hakuna ushahidi wowote ulio dhahiri!

Mwenye ushahidi wowote ule wa uhusika w Lowassa kwenye ufisadi wowote ule hapa nchini auweke hadharani ili tukate mizizi ya fitna!

=========
Updates
=========

Hadi page ya nne hakuna ushahidi wowote uliopatikana ni ngonjera za team watia nia tu!

Endeleeni kungonyerika nitakuja kutoa updates za pages zingine zitakazofuata!

Lakini fahamu hizi tips kwa wewe usiefahamu.

1. Lowassa asingejiuzulu kama utajiri wake ni wa mashaka. Angebaki kung'ang'ania uwaziri mkuu kwa maslahi mapana ya utajiri wake

2. Serikali ni kubwa na yenye nguvu zaidi kuliko Lowassa. Utajiri wa Lowassa ulianzia enzi za Baba wa Taifa, kama Lowassa angekuwa na utajiri wa mashaka, Baba wa Taifa angeshamtia ndani muda mrefu sana.

3. Kuna mawaziri waandamizi waliowahi kuwa na kesi mahakamani kuhusu masuala ya ufisadi mfano Mramba, Idd Simba na wengine wengi lakini Lowassa hajawahi kuwa na kesi hata ya kuzingiziwa. Usifikiri serikali inamuogopa Lowassa!

4. Lowassa alijiuzulu kwa dhana nzima ya uwajibikaji na kulinda chama chake na serikali yake. Angeweza kukomaa na uwaziri mkuu kama wengine wanavyokomaa mfano Mh Pinda (Operesheni tokomeza ilidunda kwa Pinda, Escrow ilidunda kwa Pinda, Mauaji ya albino ilidunda kwa Pinda, Kauli ya wapigwe tu maana hakuna namna ilidunda kwa Pinda, nk).

=======
updates
=======

Uzi upo page ya tano. Bado hakuna ushahidi. Bado ngonjera ni zilezile kama za from page 1 to 4.

=======
updates
=======

Hii post ni ya Mkandara nimeitoa page ya tano. Nimeileta hapa juu makusudi ili niweze kuitendea haki na jamii yote ijifunze kwa upana wake!

Swali:
------

=====
Jibu
=====
Kama hivyo ni kwanini tume ya mwakyembe haikumhoji kuhusu hili? Balance ya story hii iko wapi???? Kwani Lowassa ahojiki mbona hakuohojiwa ili aeleze in and out?

Ahsante sana kwa maswali yako mazuri. Hope, hapa umefunguliwa mwanga wa mengi kuhusu Lowassa. Karibu sana!

=======
updates
=======

Hizi ndio baadhi ya posts za ushahidi:

1. Nitajie mapungufu matano ya kibinadamu alionayo lowasa kama binadamu

2.Nitajie mapungufu matano ya mheshimiwa lowasa kama kiongozi mapungufu ya kiuongozi....

Tangu 2011 tunaskia sifa zake tuu sasa naomba unijuze mapungufu au Lowasa ni malaika hana kasoro...
 
1. Nitajie mapungufu matano ya kibinadamu alionayo lowasa kama binadamu

2.Nitajie mapungufu matano ya mheshimiwa lowasa kama kiongozi mapungufu ya kiuongozi....

Tangu 2011 tunaskia sifa zake tuu sasa naomba unijuze mapungufu au Lowasa ni malaika hana kasoro...

Mkuu wewe unataka nini zaidi ikiwa Lowassa mwenyewe kakubali mbele ya waandishi wa habari akimjibu Manyerere (tazama video yake) amekiri kwa kujisifia kuwa mradi ule ulikuwa safi kabisa na mitambo ilikuwa state of art ulosifiwa na rais wa Marekani wakati hata hilo kadanganya, unataka nini zaidi?. He confessed on record nakala tunayo.

Hizi sio tuhuma ni KASHFA za kiongozi na hakuna mahala alipopinga kwamba hahusiki na zaidi ya hapo alikuwa waziri mkuu alopitisha mkataba ule wapewe nani..Nukuu kibao katika report ya tume unataka nini zaidi? JK sio mjinga wa Kuachia report ile ilopelekwa kwake kwanza aje airuhusu ipelekwe bungeni wakati inamhusu yeye. Jk alijua fika Lowassa kahusika na alimwambia ajiuzuru mapema kabla halijafika mbali. Alitumia uungwana wake leo mnataka kubadilisha na hata kuwatisha familia yake ati mkiingia madarakani watakiona cha moto jamani, jamani kuweni na utu japo kidogo.

Naona una undugu na Kinjekitile wa humu Jr maana nae ni kinara wa kukumbatia ufisadi unaonuka harufu mbaya.
 
Naona una undugu na Kinjekitile wa humu Jr maana nae ni kinara wa kukumbatia ufisadi unaonuka harufu mbaya.

Yuko busy anasubili ushahidi ba sisi tunasema tunaomba Mungu apitishwe ba chama chake ndiyo atajua kuwa t unamjua uchafu wake tangy akiwa AICC, alivyoiiba NMC na kuikosakosa GT ili kuiunganisha na Yana kifupi ngoja apitishwe
 
Mie nadhan mwenye ushahidi na tuhuma hizi AMA maelezo tofauti atakuwa Lowassa mwenyewe,lakini Mbona katika mkutano wa safari ya matumaini hakuchimbua suala hili na kuweka peupe?sasa tunamtaka nani amsemee mambo ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe!!!!
 
kinachoendelea hapa ni mwendelezo uleule wa matumizi ya noti kumsafisha lowasa. lakini chombo pekee kinachosafisha watu ni mahakama lowasa kajiuzulu uwaziri mkuu kwa tuhuma ya richmond. je kasafushwa? watanzania tutaendelea kudanganywa mpaka lini nahawa wanasiasa maslahi?
 
Yuko busy anasubili ushahidi ba sisi tunasema tunaomba Mungu apitishwe ba chama chake ndiyo atajua kuwa t unamjua uchafu wake tangy akiwa AICC, alivyoiiba NMC na kuikosakosa GT ili kuiunganisha na Yana kifupi ngoja apitishwe
Badala ya kuweka ushahidi, unazidi kuandika porojo!
 
Hahahahahha hivi ameamka je Leo afya yake Mzee!tusiseme ya ushahidi bila kumjulia Hali Mzee vibaya hivyo hahahaha!!!
 
Mie nadhan Yeyote anayetafuta Urais kwa udi na uvumba maswali ya mtihani wake anajitungia!mwenyewe kwani vigezo vya uongozi vipo wap kwahiyo yeyote na asiye na doa anyooshe suti zake za kuvaa Ikulu maana anaweza Ingia,ila mwenye mawaa pale finyu kwake Kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano !tunataka kujenga taifa siyo kumfurahisha Mtu hapa hata ambaye hafai!mtu Kama anampenda Mtu ambaye sauti za wengi za sema anamadudu kiuadilifu basi wewe umpendaye mkapige Naye picha ila si Urais
 
na wewe tuletee ushahidi unaonyesha lowassa amewahi kemea au kuchukizwa na ufidadi
 
Team Lowasa ninajuwa mnatumia udhaifu wa serikali na umasikin wa watanzania kusaka urais, sii kwel mnania ya dhati kuja kutawala taifa hili na hakuna asie mjuwa Rostam Azizi kaz yake ni nini na jins gan serikal fulan imekuwa ikimtumia ili kuweka serikal kwa ajili ya masilah binafsi, Rostam alipandikizwa kwa kikwete na thx God usalama wa taifa na cia+mossad wakamshitukia na ndio ikawa mwisho wake ktk serikal ya kikwete. Sasa itakuwa ni serikal ya mazuzu kumruhusu Lowasa ktk kivul cha Rostam. Hakika dunia itatushanga na mwisho wa yote tusishangae yalio tokea misri yakatokea na Tz. Tujiulize kwa nin egpt inataka kumnyonga Morsi. Ukishajuwa ndipo ujuwe hata Lowasa hawez ikimbia hiyo adhabu. Naiman jeshi kupitia idara za taifa watapindua nchi ili kumuondoa Lowasa jambo ambalo ni hatari.
 
Wewe unataka ushahidi wa aina gani?.

Kujiuzulu tu ni ushahidi tosha weee unataka upi mwingine
 
Mie nadhan mwenye ushahidi na tuhuma hizi AMA maelezo tofauti atakuwa Lowassa mwenyewe,lakini Mbona katika mkutano wa safari ya matumaini hakuchimbua suala hili na kuweka peupe?sasa tunamtaka nani amsemee mambo ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe!!!!

Unategemea Lowassa mwenyewe ajitie kitanzini kwa kueleza anavyohusika kwenye kashfa mbalimbali? Lazima azikwepe mfano, ya Richmond amesema tatizo lilikuwa uwaziri mkuu ulioratibiwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wanamchukia. Baadae akasema alijiuzulu kwa maslahi ya chama. Sisi hatutaki wanaoweka maslahi ya chama mbele bali maslahi ya taifa.

Waliotuhumiwa na Escrow kuna aliekubali? Kila mmoja alikana kuhusika wengine wakisema fedha hazikuwa za umma, hela za mboga, za kanisa n.k. Kwahiyo mara nyingi huwezi kupata ushahidi credible kutoka kwa mtuhumiwa mwenyewe. Inabidi uje na ushahidi wako utakaoonyesha uongo wa ushahidi wa mtuhumiwa, utakaoonekana ni wa kweli beyond reasonable doubt ndo unatakiwa ukubaliwe.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom