Mwenye ushahidi wa dhahiri juu ya ufisadi wa Lowassa aweke hapa hadharani! Tuache porojo!

Lowassa angekuwa anahusika na Kashfa ile, angeweza "kukomaa" na uwaziri mkuu wake na bado pasingekuwa na mtu wa kumwajibisha, ila aliachia ngazi ili kuwaridhisheni nyie wachache mliodhani kuwa naye pia ni mhusika. Pinda "amekomaa" na mangapi na mpaka leo anadunda?
Kweli unautaka Urais kwa kuridhisha watu? Kashfa na sio tuhuma sii za kuachiwa ukataka kugombea Uraia. Pinda kajieleza katika kila tuhuma ambazo zimetokana na mfumo mbovu wa Utawala kiasi kwamba mawaziri walioteuliwa na rais ndio walokiuka maadili. Huwezi kumwajibisha waziri mkuu katika tuhuma ambazo wahusika sii waajiriwa wake. Ila kama yeye kahusika moja kwa moja kama Lowassa hapo ingekuwa swala jingine.
Mkuu natazama mpira mengineyo kiporo tutayajadili Kesho..
 
Kuna mtu alijimilikisha ranchi za ufugaji za kitaifa na sasa anaingiza sio chini ya milioni saba kwa siku...je mtu huyu ni nani?kama sio fisadi.

TeamLowassa

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Last edited by a moderator:
Unalazimisha uongo kuwa ukweli? Kwa malengo gani? Wapi akaunti ya Lowassa imeonekana kuingizwa senti yoyote ya richmond? Kwanini Lowassa ahukumiwe bila kuhojiwa? Leo hii unakomaa na ripoti ya mwakyembe kama vile msahafu?

Weka ushahidi ukate mzizi wa fitna!

Mkuu mbona unaleta propaganda?

Kakiuka maadili ushahidi unapatikana kwenye ripoti ya tume huru ya kibunge ya Mwakyembe iliyopewa mamlaka kushughulikia swala hilo.

Ni msahafu ndio,hakuna tume iliyopewa pawa ya kushughulikia swala hilo,aidha utuambie mamlaka gani iaminiwe kuchunguza swala hilo na nguvu izipate wapi??

Na unachekesha zaidi unapodai hakuna hata senti moja iliyoenda kwenye accnt za mamvi,ni claim ya kipuuzi mno,kwa akili yako organized crime hua wanapeleka hela benki ambapo pana paper trail?Pia third party anaweza chukua hela kama front man na yeye akachukua cash...hela inaweza pita mikono ya watu zaidi ya 5 na zaidi ndio imkute yeye.

Unashangaza sana kuongelea mashtaka ya kimahakama wakati tume ilifatilia solely maadili,mahakamani zinaenda taasisi zinazohusika baada ya akina Mwakyembe,I betcha hakikufanyika kitu upande coz ya serikali ya bwana zaifu...

Kadanganyeni vitoto vya kindergarten sisi tunajielewa
 
RICHMOND (GIRE HOUSTON TEXAS)-AMBASSADOR/ Facilitator (Mr. DARAJA)-the President (commanding unit) Dr/Prof Kikwete - Implementer (Mr. Edward Lowasa). Lowasa Kashikwa na ngozi ndiye mwizi.
 
Kweli unautaka Urais kwa kuridhisha watu? Kashfa na sio tuhuma sii za kuachiwa ukataka kugombea Uraia. Pinda kajieleza katika kila tuhuma ambazo zimetokana na mfumo mbovu wa Utawala kiasi kwamba mawaziri walioteuliwa na rais ndio walokiuka maadili. Huwezi kumwajibisha waziri mkuu katika tuhuma ambazo wahusika sii waajiriwa wake. Ila kama yeye kahusika moja kwa moja kama Lowassa hapo ingekuwa swala jingine.
Mkuu natazama mpira mengineyo kiporo tutayajadili Kesho..
Mkuu vuta subira kidogo tu, hili la RICHMOND liliwekwa kiporo pale sheikh Kaluta kwa sababu maalum, ila nina imani kubwa kuwa LOWASSA atateuliwa na CCM kuipeperusha bendera ya chama, hivyo katika muendelezo wa safari hii ya matumaini RICHMOND itaibuka tu, na ukweli wote utadhihirika!
 
Agent zote kubwa duniani +intepol wanajuwa uchafu wa huyo mtu. Mwanaume kunyamaza kimya pamoja na vitimbwi mke wake anamfanyia sio kwamba amelishwa limpwata bali ni kujuwa thaman ya uwanaume wake. Mh Lowasa kuto pelekwa mahakaman sio kwamba anaogopwa na serikali bali ni utashi wa kisiasa na hekima za mwenye nchi kwa sasa. Hakuna mwanaume ataanza simulia habari za undan wa mke wake labda awe kichaa. Lowasa ata akipata watu B1. Usafi wake niwamashaka na uwenda as
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana, yaani tumejiwekea wenyewe utaratibu wa namna ya kuwajua wezi, majambazi, wala rushwa e.t.c.....hivi ni MAHAKAMA ipi ambayo imemhukumu LOWASSA kwa UFISADI?

Hivi hapa tz kuna kitu kinaitwa mahakama? Rushwa iliyojaa na dhulma za wazi wazi huzioni au macho yako yameziba?

Mimi simzungumzii EL nazungumzia hiyo mahakama unayosisitizia ambayo magabachori wanawalipa hao wajamaa na wewe ngozi kama yangu ukaishia kudhulumiwa

(sorry for being off point kwenye mjadala)
 
Lowasa ni fisadi papa na kibaka mzoefu.Ushaidi mwl nyerere,ripoti ya mwakyembe,Marafiki zake chenge na rostam.Pia ukwapuaji viwanja na lunch za taifa.Lowasa ni kibaka kama ingekuwa china angekuwa ametuliwa na bomu au kunyongwa adharani au kuchomwa moto

We kweli mwehu, badala ya kuweka ushahidi we unaharisha hapa, shame on you! chuki nyingine hazina maana...
 
Kokolo hili haliachi kitu ... hahaha .... Ngoma inogile ..
RICHMOND (GIRE HOUSTON TEXAS)-AMBASSADOR/ Facilitator (Mr. DARAJA)-the President (commanding unit) Dr/Prof Kikwete - Implementer (Mr. Edward Lowasa). Lowasa Kashikwa na ngozi ndiye mwizi.
 
Kama mnafikiri hayupo wa kuthibitisha tuhuma zake basi mpitisheni awe mgombea wa Urais nasi tutathibitisha kwenye Sanduku la Kura

Lowassa ndiye mtaji kwa CCM kwani ndo mwanasiasa mwenye social capital kubwa kuliko wote kwa sasa. hii ni pamoja na upinzani. Mbowe mwenyewe anathibitisha hilo
 
Wewe kweli mwehu.... no wonder mnawekewa the Hague wakati wauaji wakuu wanaachwa kupeta ... wazungu worshippers mnalaana .... mnaona FBI, CIA MI6 no wa maana .... wako kwaajili ya nchi zao...
Agent zote kubwa duniani +intepol wanajuwa uchafu wa huyo mtu. Mwanaume kunyamaza kimya pamoja na vitimbwi mke wake anamfanyia sio kwamba amelishwa limpwata bali ni kujuwa thaman ya uwanaume wake. Mh Lowasa kuto pelekwa mahakaman sio kwamba anaogopwa na serikali bali ni utashi wa kisiasa na hekima za mwenye nchi kwa sasa. Hakuna mwanaume ataanza simulia habari za undan wa mke wake labda awe kichaa. Lowasa ata akipata watu B1. Usafi wake niwamashaka na uwenda as
 
Miaka yote ameshindwa kujitetea sasa ndio apate wa kumtetea aende front yeye ajitete uliyeanzisha mada je una uhakika alikwisha kukuelezeeni undani wa jambo la richmond au mnatumika tu
 
Ushahidi ni report ya Mwakyembe. Riport imemtaja Bungeni na vyombo vya habari vyote nchini vimemtangaza. na yeye alikiri na akaamua kujiudhuru uwaziri mkuu kwa fedheha kubwa na tangia hapo hajakanusha wala hajalalamika katika chombo chochote cha kutoa haki kuwa amesingiziwa.

Ushahidi mwingine ni mifedha anayotumia kujifaharisha ambayo haijulikani vyanzo vyake halali. atokeze hadharani kuelezea ni vipi amepata utajiri huo na atoe vielelzo vya kodi aliyolipa Serikalini kama ana biashara halali inayomuingizia kipato
 
Back
Top Bottom