Mwenye ufahamu wa tatizo hili.

Bongo senior

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
291
480
Habari za muda huu pia nitoe pole kwa wote wenye changamoto ya kila aina.
Naomba niwasilishe ombi la msaada kwa kila mwenye uelewa nalo, iko hivi nina ndugu yangu alipata ajari ya pikipiki huko vijijini mguu ukavunjika lakini mfupa haikuachana kabisa ulibaki upande umeshikana na upande imeachana akapelekwa hospital akapata matibabu hiyo ni tangu mwezi wa sita na mpaka sasa anatembea ila changamoto ni kwamba akitembea anahisi kama ile ngozi inakuwa kama sponji au kama anaspring wakati anatembea hali inayomfanya ahisi mguu kama umekuwa mfupi je inasababishwa na nini hii hali?
Nitangulize shukrani na samahani kwa uandishi endapo utamkwaza yeyote pale.
 
Huo mfupa haujaungana by nesi wa zamu

Aende hospital akawaone madaktari bingwa wa mifupa, kama hana pesa na hana bima nifikishie pole zangu.
Shida hapo kwenye bima kwa maisha ya huko alipo kwanza ukiwaambia habari za bima hawaelewi watu wanaishi wapo full of confident kwamba kuumwa kwa mwaka mzima wana uhakika wakutoboa sasa umwambie habari bima haelewi kabisa ni wachache wanaoelewa wanaojua kuumwa si malaria pekee, na upatikanaji wa pesa kwa uko ni mgumu pia. Nilimshauri aende hospital lakini kama hayupo tayari anachotaka kujua changamoto ya hiyo hali tu sijui ana option gani baada ya hapo.
 
kutoka kijijini hadi town ni km ngapi boss?
Huduma nzuri zipo kwenye hospital kubwa asifanye mchezo kabisa
 
Shida hapo kwenye bima kwa maisha ya huko alipo kwanza ukiwaambia habari za bima hawaelewi watu wanaishi wapo full of confident kwamba kuumwa kwa mwaka mzima wana uhakika wakutoboa sasa umwambie habari bima haelewi kabisa ni wachache wanaoelewa wanaojua kuumwa si malaria pekee, na upatikanaji wa pesa kwa uko ni mgumu pia. Nilimshauri aende hospital lakini kama hayupo tayari anachotaka kujua changamoto ya hiyo hali tu sijui ana option gani baada ya hapo.
Huo mfupa haujaunga.....mwambie Dr Evelyn kasema hivo
 
Habari za muda huu pia nitoe pole kwa wote wenye changamoto ya kila aina.
Naomba niwasilishe ombi la msaada kwa kila mwenye uelewa nalo, iko hivi nina ndugu yangu alipata ajari ya pikipiki huko vijijini mguu ukavunjika lakini mfupa haikuachana kabisa ulibaki upande umeshikana na upande imeachana akapelekwa hospital akapata matibabu hiyo ni tangu mwezi wa sita na mpaka sasa anatembea ila changamoto ni kwamba akitembea anahisi kama ile ngozi inakuwa kama sponji au kama anaspring wakati anatembea hali inayomfanya ahisi mguu kama umekuwa mfupi je inasababishwa na nini hii hali?
Nitangulize shukrani na samahani kwa uandishi endapo utamkwaza yeyote pale.

Si rahisi sana kupata jibu mwafaka, kwani inahitaji kujua jinsi alivyopata ajari/mechanism, kiasi cha kuvunjika, aina ya uvunjikaji, jinsi mguu ulivyounga., athari kwa viungo vingine nk.

1: Inaweza kuwa kuna uungaji ambao haukuwa sawa/malunion.

2: Kuna misuli ilipata shida pia wakati wa tatizo.

3: Kuna mishipa ya fahamu kupata shida pia.

NB: Afike hospitali yenye wataalam zaidi ili kufanyiwa tathmini nzuri na tiba ya uhakika.
 
Back
Top Bottom