Mwenye nyumba kanipa siku mbili tu, la sivyo...

Mwenye nyumba kanipa siku mbili tu, la sivyo...

Pole, utamaduni wetu ni kuchangia harusi ili tukale na kunywa;
Pengine wapo wenye uwezo wao watakusaidia.
 
uzi haukuwa hcit chat ulikuwa jukwaa la biashara, umehamishiwa chit chat na mods kuja huku, so kama unaweza msaidie

Ulikuwa Chit chat na ndio maana nikang'aka kwanza maana jukwaa lile huwa limekaa kimizaha mizaha...

Bila shaka baada ya mleta uzi kulalamika ndio umeletwa hapa sasa...hata hivyo sina uwezo wa kutoa msaada wowote.
 
Mkuu pole sana ila nakushauri weka namba zako wazi bila aibu kwa maana una shida na kuomba msaada si dhambi. Ukiweka namba zako wazi naamini utafanikiwa ndani ya siku moja kupata hiyo pesa ndogo.

Ukificha watu wanaweza kukuhisi vibaya.Weka mambo wazi upate msaada. Hata katika mataifa makubwa mambo kama haya yapo na watu husaidiana. Wewe si wa kwanza kuomba msaada kwahiyo ACHA aibu.

Nakuombea kwa Mungu.
 
Pole kaka, ila kiushauri ni kwamba sheria ya makazi hasa kwa mpangaji unahaki ya kukaa hio nyumba ndani ya miezi mitatu baada ya mkataba wako kuisha ili upewe fursa ya kujipanga kuweza kuhama!!

Hivyo kama mkataba wako uliisha jan 16 basi ujue miezi yako mitatu kisheria ita expire 17 April.

Muombe na umueleze hayo landlord wako akigoma nenda serikali za mtaa kwa msaada zaid, USINYANYASIKE SHERIA INAKULINDA!!!
 
Pole ndugu 400000 /= huna hata dhamana Maana Dunia ya sasa bila dhamana kupata mkopo ni Ngumu!
 
Hivyo kama mkataba wako uliisha jan 16 basi ujue miezi yako mitatu kisheria ita expire 17 April.

sheria ya wapi hiyo mkuu inayoruhusu kukaa miezi mitatu bila kulipa pango
 
hahaha......Nikikumbuka bili niliyolipa jana Bar na Bajeti niliyotenga kwa Familia yangu kwa ajili ya Valentines day nikicompare na Kodi ya mshkaji ya nyumba kwa Mwaka unaweza hisi kwenye haya Maisha Mungu hayuko fair kabisa.

Mungu kweli hayupo fair japo kafanya hivi kwa sababu fulani
 
Mungu kweli hayupo fair japo kafanya hivi kwa sababu fulani
I agree with you 100% lazima Mungu anazo sababu zake utakuta mchizi hata fungu la kumi hajawahi toa tokea ameanza kujiingizia kipato....Kijana azidishe maombi ni mapito tu anapitishwa kama mtumishi wa bwana Ayubu.
 
kabisa mkuu ... wengi utoaji hawana wanapenda kupokea ila all in all ndiyo maisha
 
Pole kaka ningekushauri kutafuta chumba cha bei ya chini ili uweze kupanga mipango yako vizur hali ya kifedha kama siyo mzuri panga hata chumba cha Giza then mambo yakitengemaa tafuta room nzuri
 
Back
Top Bottom