Mwenye kidonda anaua nzi wote

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
758
1,000
Wanahitaji wengi zaidi na zaidi na msipokoma mtaisha kweli. Jamani mwenyekidonda hajali idadi ya inzi wanaokufa yeye anaangalia kidonda chake tu na hukilinda. Narudia tena inzi wataisha wote kama hamtaacha kufuata kidonda cha huyo mtu. Nani hajui maumivu ya kidonda?

Inzi huenda hawajui maumivu yake ila kumbukeni ni bora kushinda jalalani kuliko kishinda ndani kwa mwenye kidonda tena chenye maumivu. Ila kidonda kina usaa mwingi huenda mwenye kidonda atakufa kesho, kwa hiyo msubiri hadi kesho. Japo madaktari wanasema kesho atapona ila nyie inzi endeleeni kuamini kesho mwenye kidonda atakufa na kama sio kesho basi kesho kutwa, Acheni haraka.

Na madaktari ndio kazi yao hiyo kusema mgonjwa atapona, Sasa nashangaa nyie kuendelea kusubiri daktari aseme mgonjwa hatapona. Hatasema hadi mgonjwa afe kweli maana nae anaogopa isije aka.

Ndugu wa mgonjwa sio wote wanaompenda mgonjwa ila hawawezi sema eti ww mgonjwa bora ufe,sio tamaduni yetu. ILA INZI MTAISHA WOTE.
 
andjul

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
17,304
2,000

Nzi hawawezi kukoma kutua kwenye kidonda, ndani ya kundi la nzi hao kuna kundi ambalo halitui kwenye kidonda,huwavuta karibu wenzao, linajizungusha jirani tu, iwe usiku kuwe mchana, hili kundi linaloshindwa kuvumilia harufu kali ya kidonda ndio huuawa.

Kwani mwenye kidonda anapata maumivu ya kindonda?! Labda afe kwa kukehereka kwa harufu, japo huzoeleka...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom