Mwenye dada tuongee inbox

Simplicity.

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
2,636
1,661
Wakuu,

Hii njia sio ya kawaida lakini najua ni effective. Mara nyingi wanaume tunakuwa na taarifa sahihi kuhusiana na tabia za wanawake, hasa ni wanawake wa aina gani wanafaa kuolewa, tena mbaya zaidi hata kama mwanaume amepinda vipi anajua mwanamke anayefaa na asiyefaa.

Kwa muktadha huo, naomba jamaa aliyepo humu, mwenye dada yake swafi kabisa, ambaye anajua anafaa kuwa mke ila sijui inakuwaje haolewi au ndio amefikia umri wa kuolewa, niongee naye kikubwa anipe mawasiliano ya dada yake. Wewe nipe namba kupitia inbox, halafu potea, mambo mengine nitamalizana naye, hasa kama yupo Whatsapp ndio itakuwa rahisi zaidi.

Kuwa muungwana usiniuzie, gumegume ambalo hata ninyi kama familia mnatafuta pa kumtelekezea. Nakuahidi donge nono. Tafadhali niko serious, hakikisha unayeniunganisha naye ni dada yako.

Sifa: Dada yako awe mzuri, yaani awe anatazamika na tabia nzuri, basi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom