Mwenge wa Uhuru wazindua kituo cha redio Chalinze FM 97.5

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
325
414
Wiki hii Mwenge wa Uhuru ulifika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani kumulika na kukagua miradi ya maendeleo ambapo ilizindia Kituo cha Redio cha Chalinze FM 97.5 chini ya kauli mbiu yake ya 'Sauti ya Jamii'.

Chalinze FM iko katika Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Chalinze na Kituo hicho cha Redio kimeanzishwa kwa gharama zilizopatikana kupitia mapato ya Halmashauri.

Mbunge wa Jimbo hilo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akimkaribisha Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Abdalla Shaibu Kaim kuzungumza ndani ya Redio hiyo amesema Kituo hicho kimeanzishwa ili kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali na zile za ndani ya Halmashauri, kuhabarisha umma na kuwaunganisha Watanzania wote.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Ndugu Kaim amesifu uwekezaji huo mkubwa wa Halmashauri ya Chalinze na kuwapongeza na kuzindua rasmi redio hiyo.
FB_IMG_1684478341882.jpg
FB_IMG_1684478337236.jpg
FB_IMG_1684478332893.jpg
 
Safi.
Hivi Chalinze ndio Wilaya au Bagamoyo?
Naona kama Bagamoyo inamezwa na Chalinze.
 
Back
Top Bottom