Mwenge-Tegeta Road: Poorly designed, poorly constructed! Nani awajibike?

Inaitwa "Acceleration lane". Kwenye hii barabara ya Mwenge -Tegeta nadhani nimeziona mbili tu, pale junction ya Africana na inapoishia barabara kule Tegeta.
Inaitwa Decceleration lane kama unatoka barabara kuu kuingia pembeni. Acceleration lane ni ile unapotoka pembeni kuingia njia kuu.
 
Kosa liliopo ni kuwa hakuna service road ambayo mtu unatakiwa uchepuke unapokaribia njia ya kuingi nyumbani si upite mbele ukageuze!
 
WIZARA YA UJENZI KICHAKA CHA RUSHWA NA UCHAKACHUAJI ....kuanzia barabara hewa ,mabarabara yaliyojengwa chini ya kiwango kwa hali ya juuuuu...na ommition ya baadhi ya vitu very basic kwa urban roads za mijini
IE
Barabara ya Kilwa ilijengwa chini ya kiwango ....lami gauge ndogo sana ,mashimo yalianza hata kabla haijakamilika ,hata baada ya kurudia bado walichakachua tena
Sehemu kubwa ya Kilwa rd haina Mitaro ya maji ....na hata alama za barabara
Barabara ya kilwa haifa traffic lights hate mojo...
barabara haina miundombinu ya maji ya bomba kwa ajili ya kunyeshea hasa kwenye round abouts ...wala hakuna miti imeoteshwa
Hakuna service road

Barabara ya Tegeta ndio nayo kichwa kuuma
Hakuna miondombinu ya maji ya kunyeshea kitu kinacholazimisha pale lUGALO jeshini huwalazimu kubebana na maji kila asubuhi , na hali ni hiyo kulazimu manispaa ya Kinondoni kubeba maji na malori ya maji kunyeshea majani ..kitu ambacho huhatarisha hata watumiaji wa barabara kutokana na malori ya maji kusimama ovyo

Barabara nayo haina taa za usalama hata moja ...ni giza mtindo mmoja
mitaro ipo lakini michache
drainage hasa maeneo ya masana hakuna ilitakiwa kuweka culverts na kuongoza hadi kwenye mto ...
service road baadhi ya maeneo zipo kwingine hazikumaliziwa

Barabara ya Morogoro iko kwenye hali mbaya baadhi ya maeneo na upande wa mwendo kasi ..ni nyembamba kiasi kuwa ni tabu hata malori kukata kona
 

Pale unatakiwa upige L turn yaani ukipiga kona kulia hakikisha umetoka mpaka service road iliyopo nje tu ya ofisi ya Tanesco Mbezi Beach/Imalaseko supermarket ya zamani then ndiyo upinde tena kuelekea Mwenge ukiwa Service road utaendelea mbele mpaka ufike NBC Bank
 

Usipotoshe umma, soma maelezo yangu hapo juu nimemjibu kiongozi fulani halafu utaona jinsi gani umepotoka.
 
Sijawahi kuona highway inajengwa hakuna hata traffic light kwenye junction.

Bagamoyo road ni majanga tupu
 
Watanzania bana, kila mtu ni mtaalamu wa kila kitu. Si ajabu mleta uzi unaweza kuwa mtaalamu wa linguistics lkn unakosoa design na construction ya barabara!!!
Anyway, Tupe vigezo vya kitaalamu vyilivyokiukwa katika design na construction ya barabara tajwa.
 
Ahh yess ile service road pale...
 
Ni kweli Mkuu. Ninafikiri suluhisho moja ni kuweka traffic lights na barbara ya tatu unapokaribia junction kama ya Tanki Bovu kama pale Namanga unapotoka Bagamoyo Road kwenda Kimweri Avenue.
 
Hii barabara aloichora kwanZa kabisa acharazwe viboko hadharani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…