Mwenge-Tegeta Road: Poorly designed, poorly constructed! Nani awajibike?

Morogoro road ndio usiseme. Matuta mataa kila baada ya hatua 10.
Nini faida ya matuta?? Kipindi inajengwa au kwenye mchoro matuta yalkuwepo??

Usjiangalie wewe tu na kigari chako. Tazama maisha ya watu wako
 
U-turn barabara kubwa kama hio sio salama. Inabidi utoke nje ya barabara ndio urudi ulipotoka.
Ni kweli, but kiuhalisia uturn zafanyika as we type na zitaendelea,Je usalama upoje,au nini kifanyike?
Kuna Lane Ile sijui inaitwaje huwa inaongezwa pembeni hivi mtu anaekata kona aingie bila kuathiri wanaondelea mbele..
 
road designer , consultant ndio wenye matatizo, contractor anafanya kama anavyoelekezwa kwenye mchoro.
 
Ni kweli,ila mind you tunazungumzia sehemu zingine pia,Je ziko convenient kama hapo Petrol station?
Mfano ukitokea mwenge unataka kuingia makonde upande wa mbezi beach unafanyajr kama sio ku uturn? For convenience purposes ipi njia salama
 
Ile barabara ni kaburi la pamoja kama kwenye vita/mauaji ya kimbari
 
Mkuu umenena.
Waangalizi wa usanifu sijui walikuwa wapi katika kupitia mradi huu.
Sasa ni wazi kuwa kuna watu hasa wahandisi hawafanyi kazi yao.
 
Kuna ile audio clip ya Halima Mdee, Mbunge wa Kawe aliyoitoa majuzi Bungeni wakati akichangia katika bajeti ya wizara ya ujenzi alizungumza mambo ya msingi sana kuhusu ufisafdi na changamoto za hii barabara ya Tegeta - Mwenge- Morocco.
Mwenye nayo msaada aiweke hapa tafadhali.
 
Yaan we shukuru tu imejengwa na haijabanduka bado.., Tabata lami hazichukuagi mwezi, courtesyof Del monte
 
Ni kweli, but kiuhalisia uturn zafanyika as we type na zitaendelea,Je usalama upoje,au nini kifanyike?
Kuna Lane Ile sijui inaitwaje huwa inaongezwa pembeni hivi mtu anaekata kona aingie bila kuathiri wanaondelea mbele..

Inaitwa "Acceleration lane". Kwenye hii barabara ya Mwenge -Tegeta nadhani nimeziona mbili tu, pale junction ya Africana na inapoishia barabara kule Tegeta.
 
We'll said mkuu hii Barabara ina u turn 2 tu, ndo mana mkulu wa wakati ule alisema ukitaka kula lazima uliwe kidogo. Ndo tushaliwa hi yo, tuitumie kwa uangalifu tu
 

Panahitaji taa za kuongoza magari
 
Barabara imekosewa sana na sijui kama tuna hela ya kuongeza barabara za kuchepuka pembeni
 
Wa kulaumiwa ni aliyekuwa waziri wakati huo
 
Ah
Mkalifya umenikumbusha mbali I'd yako imetulia
 
Kupe umesema kweli. Wa TZ wamezoea sana kufanya mambo kiholela. wanataka kila baada ya hatua chache wakatishe barabara. Hata watembea kwa miguu hawatumii zebra crossings wanavuka kila sehemu kiholela. Hata vitu vidogo vya watu binafsi kutimiza wajibu wao wanalalamikia serikali.

 
Tatizo si la watalam ni njaa yetu. Tuliomba msaada ya kujengewa barabara kwa Wajapan. Wao wakatoa masharti moja wapo ni kutojenga njia za mikato na taa za barabarani. Tulikubali masharti na ndicho kilichotokea. So issue si wataalam wetu ni njaa yetu
 
Mbona ya kutoka mwenge kuja morocco hamuijadili? Au zile pesa za sherehe ya uhuru ndio hazikutosha? Barabara ile inajaa maji kupita kiasi. Na ina mawimbi kushinda ya baharini. Hata sielewi hawa wajenzi walitumia akili ya wapi kufanya kazi chini ya kiwango vile. Au mnamkomoa aliyeagiza kupanuliwa kwa barabara hiyo? Waziri mhusika zuia malipo ya upanuzi wa barabara hiyo na eafungulie mashtaka wahandisi wanaojenga barabara chini ya viwango mlivyokubaliana. Nawasilisha japo sina gari wala pikipiki!
 
Kila kitu wanafanya JICA kuanzia michoro mpaka kukabidhi barabara na wana wahandisi wao na kila kitu chao.Shida yetu ni umaskini wetu ndo mana tunapokea kazi zenye makosa kama ile ya Kilwa road
 
Inaitwa "Acceleration lane". Kwenye hii barabara ya Mwenge -Tegeta nadhani nimeziona mbili tu, pale junction ya Africana na inapoishia barabara kule Tegeta.
Kama unatoka mjini, ukifika Africana huo mchepuo unaokuwezesha kufanya right turn unaitwa "deceleration lane" sio acc***
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…