Simple sana.
Anayepatia ni CDM, anayepoteza ni machawa wa CCM wala sio CCM.
Hii ni kama kusema mwenendo wa siasa hizi ni CDM vs Machawa wa CCM.
Kuna uzi humu nimeandika kwamba, adui mkubwa wa CDM ni Polisi na wala sio CCM.
Polisi kwa namna nyingine tunaweza kuwaita ni machawa wa CCM. Wapinzani huenda mbali na kuwaita PolisiCCM kwa namna wanavyotumika kufanikisha maswala ya CCM na kuwaumiza wapinzani.
Kwa mwenendo huu ni kama wanakosa ile nguvu radical waliyokuwa nayo wakati wa zile siasa za Magufuli. Watajiona sasa ni wanyonge kuwabughudhi wapinzani hasa CDM kwa kuamini kwamba viongozi wao wapo karibu sana na CCM.
Unadhani nani yupo nyuma ya siasa hizi mpya Tanzania?
Watu wawili: J. Kikwete & Abdulrahaman Kinana.
Kwanini?
1. Soma signals anazorusha Lema, Soma signals alizowahi kurusha Lissu akiwa Belgium, n.k.
2. Hao watajwa wote hapo juu ni waasisi wa siasa za mwenendo huu. Ndio kuna wakati J.K. aliitwa Rais dhaifu na wala hakumaindi hadi leo.
Ni wakati wa J.K. na Kinana ndiko upinzani iliimarika zaidi hapa nchini kuliko nyakati zote.
Je, ina maana CCM kama chama hawapotezi?
CCM wanapoteza. Kwa sababu ndani ya mfumo wa utawala na siasa nchini wapinzani ni wengi mno, lakini wanaogopa kuwa front.
Hivyo, kwa hali hii walau watapata 'relief' kwa kiasi chake na kuwa kidogo huru kutokandamiza upinzani kama ilivyozoeleka.
Kitu gani kimepangwa kwa mbali sana ambacho watu wengi hawakioni?
Hiki:
Siasa za CCM ziwe karibu na nguvu sawa na za upinzani. Ili ikitokea Kiongozi aina ya Magufuli akitwaa madaraka basi aweze kuthibitiwa ipasavyo na mfumo ulio huru wa kisiasa hasa kutoka upinzani.
Kwa maana kwamba, ujio wa aina ya urais wa Magufuli uliwatisha mno the 'senior citizens' na kuwafanya wawe wanyonge kulikopitiliza wasiamini kwamba waliwahi kuwa viongozi wakuu hapa nchini. Ilikuwa ni fedheha sana.
Swali linalowasumbua:
Je, tutafanyaje siasa za nchi yetu ili kusiwepo tena room ya marais wa aina ya Magufuli kuibuka na kuendesha nchi kwa mfumo ule?
Jibu rahisi:
Wanaamini hivi. Ni kujitahidi kuimarisha mifumo ya kisiasa ili vyama vya upinzani hususan CDM kiwe na nguvu imara kiasi kwamba akitokea Kiongozi wa juu kukengeuka basi wapinzani waweze kushughulika naye.
Hii ni kwa sababu hata kipindi cha ubabe wa Magufuli at least wapinzani walijitahidi kumkabili ingawa walikuwa na mazingira magumu zaidi. Ilhali wana CCM waliendelea kumtetea na kumpigania badala ya kumfunga speed governor. Take note of this!
Inaonekana kwamba this time around CDM itavuna wabunge wengi zaidi kuliko kipindi chochote kile.
All the best