Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC atua nchini

Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC atua nchini

kimenuka......kimenuka......
.

hakika kimenuka
 
Eeh, huyu jamaa sidhani kama kasomea sheria kweli, maana hata kutoa argument hajui-Kwa hiyo moja kati ya majukumu yake ni kutembelea nchi na kusalimia mara tu baada ya kuteuliwa!?

Kwa kweli baadhi ya "remarks " za huyu Bwana zinanifanya nitilie shaka uwezo wake kisheria na kutafakari.
Angekuwa kwenye private practice kamwe nisingemwajiri kunitetea!
 
Kimenuka ......, kuna watu wameanza kuvaa pemper. "chezea ICC weye" walifungulie mwanahalisi fasta ku pozaa hasira zetu .
 
Kama mnazani amekuja kwa ajili ya Tanzania then you're less updated!
Kwanza ni few weeks ago tu kulikuwa na majadiliano uwezekano wa kesi za Kenya zilizo ICC kufanyika ama Kenya au Tanzania! Wengi wanaona kufanyika Kenya si busara kwa kuzingatia umaarufu wa wahusika! Hivyo, kama option itakuwa ni kuziondoa Netherlands na kuzileta EA, basi favorable place ni Tanzania!

Ukichukua ukweli huo, ukachanganya na sakata la hivi majuzi pale Jaji kutoka Kenya alivyofanyia mizengwe huko kwao ili asije Tanzania, then unaweza pata jibu! Sio hivyo tu, kuna viongozi kadhaa kutoka Kenya ambao wamekuja TZ siku za karibuni! But all in all, ziara hii ya Fatouma inaishia huko huko Kenya hapo kesho 04.03.2012!

Then, you can connect the dots!
 
Huyo AG naye angesema tu hajui,sasa suala la kusema amekuja kusalimia kwani hilo ni mojawapo ya majukumu yake? Mimi ningejiuliza masuala kadhaa...kwanini aje sasa? Je,anapanga timu ya uchunguzi kwenye uchaguzi wa Kenya? Je,ni kweli amekuja bila sababu ya msingi hapa Tanzania? Ni nchi ngapi amewahi kwenda bila sababu ya msingi (isiyohusiana na haki za binadamu)? Je,Tanzania kumekuwa na uvunjifu wa haki za binadamu unaohitaji ushiriki wa taasisi za kimataifa? Kwa nini mgeni huyo amekuja kimya kimya?
 
Mbona mwanasheria mkuu na DPP waziri wa katiba walikuwepo?au nawao walitembelewa?naamini alikuja kisheria zaidi na muda ukifika mambo yote yatakua wazi time will tell
 
8E9U3870.jpg


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa(ICC) Bibi Fatou Bensouda(Wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kushoto ni Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bibi Angellah Kairuki(Wanne kushoto) na kulia Mwendesha Mashtaka mkuu wa Serikali Bwana Feleshi
 
8E9U3836.jpg

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwendesha Mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa(ICC) Bibi Fatou Bensouda ikulu jijini Dar es Salaam.

Angalia mkoa wa Kikwete, sura ya wasiwasi, kidole kinamwasha, yaelekea hakuamini kama kweli ujumbe umefikishwa kwa wahusika, hapa anatafuta ya maneno ya kumpamba mama wa watu. Kazi kweli kweli.
 
Hapa hakuna ubishi lazima kimenuka, pamoa na kituo cha haki na binadamu, balozi za nje hapa kwetu lazima zinapeleka matukio yote machafu wanayofanya hawa wahuni wa hii serikali ya Tz.

Wataona kama mzaha baada ya muda utasikia watu wananyakuliwa mmoja baada ya mwingine.

Kichaa Werema anasema mama kaja kutembea? Alimualika yeye? Hivi huyu Werema ana akili sawasawa
 
Aliyefungua kesi hiyo kutoka kituo cha haki za binadamu nchini ni Mwanamke na huyo Mwendesha mashtaka kutoka huko ni Mwanamke pia naona ngoma nzito kwa Kiwete, makoti yanaanza kupwaya.
 
....Gazeti hili lilipomtafuta Jaji Werema kuzungumzia ujio wa Bensouda alisema kuwa Mwendesha Mashtaka huyo alikuwa mgeni wa Rais Kikwete, hivyo hawezi kueleza kilichozungumzwa.

“Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja Tanzania,” alisema Werema.

Kama ilivyokuwa kwa Werema, naye Feleshi alikwepa kuzungumzia ujio huo wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, huku akisema jambo hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Ikulu.......

source: mwananchi gazeti

Kama kawaida yake Werema anamung'unya maneno, anadai hakuwa mgeni wake kwa hiyo hawezi kusema lolote (kwenye bold) alafu anatuambia alikuja kusalimia, je alitumwa na nani atuambie kuwa huyo mgeni alikuja kusalimia? Kweli nimekubali Werema anatumia kichwa chake kufugia nywele.

Yangu macho!
 
Hahahaha! Asante sana candid scope namsoma J. K ana BCBG(wenge) la kufa ndani ya muda mchache kashapoteza 14kg
 
“Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja Tanzania,” alisema Werema.

Ni mwana sheria na ni jaji ! Yaani mtu atoke all the way kuja kusalimia ?
Pengine ataomba uraia ccm imteue ugombea 2015
 
Back
Top Bottom