Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC atua nchini

Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC atua nchini

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
attachment.php

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwendesha Mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa(ICC) Bibi Fatou Bensouda ikulu jijini Dar es Salaam.

attachment.php

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa(ICC) Bibi Fatou Bensouda(Wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kushoto ni Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bibi Angellah Kairuki(Wanne kushoto) na kulia Mwendesha Mashtaka mkuu wa Serikali Bwana Feleshi

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda, ametua nchini jana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya ICC imekuja ikiwa ni miezi sita tangu Serikali ya Tanzania ilipopelekwa katika mahakama hiyo, iliyoko The Hague, Uholanzi kwa madai ya kukiuka haki za binadamu.

Malalamiko hayo maalumu yalipelekwa ICC na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Septemba 28 mwaka jana, baada ya kutokea kwa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi na watu wengine 23.

Taarifa ya LHRC ilieleza kuwa pamoja na watu hao kuuawa, Serikali ilishindwa kuwachukulia hatua wahusika.

Mbali na kuishtaki Serikali ICC, kituo hicho cha Sheria na Haki za Binadamu pia kilipeleka mashtaka kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk Hellen Kijo-Bisimba, alisema kuwa walifungua mashtaka hayo ili kuzitaka mamlaka hizo za kimataifa kufanya uchunguzi na kuichukulia hatua stahiki za kisheria dhidi ya Serikali ya Tanzania.

Jana Rais Jakaya Kikwete alikutana na Bensouda na kufanya mazungumzo na baadaye walipiga picha za pamoja nje ya Viwanja vya Ikulu, akiwa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi.

Katika maelezo yake Bisimba alisema: “Tumepeleka mashtaka 24 ICC tangu Septemba 28 mwaka huu, ambayo yanahitajika kufanyiwa uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikiwalinda viongozi wake wanaokiuka haki za binadamu.”

“Tunatarajia kuona uwajibikaji wa viongozi wote wa Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa njia yoyote ile. Hatua hizo au uwajibikaji huo ni pamoja na kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani,” aliongeza Dk Bisimba.

Gazeti hili lilipomtafuta Jaji Werema kuzungumzia ujio wa Bensouda alisema kuwa Mwendesha Mashtaka huyo alikuwa mgeni wa Rais Kikwete, hivyo hawezi kueleza kilichozungumzwa.

“Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja Tanzania,” alisema Werema.

Kama ilivyokuwa kwa Werema, naye Feleshi alikwepa kuzungumzia ujio huo wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, huku akisema jambo hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Ikulu.

LHRC ilichukua hatua hiyo kutokana na kuongezeka kwa mauaji ya raia wakiwa katika mikono ya vyombo vya dola, huku Serikali ikigwaya kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika.

Pamoja na hatua ya kushtakiwa kwa Serikali katika mamlaka hizo, Bisimba alisema kuwa bado wanataka kuona viongozi wote wa Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa namna yoyote na mauaji ya Mwangosi na raia wengine wakiwajibishwa. 

Alifafanua kwamba kuanzia Januari hadi Septemba mwaka jana, jumla ya watu 24 waliuawa na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama. 

Dk Bisimba alisema tangu mwaka 2001 hadi sasa, kituo hicho kimekuwa kikifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya mauaji yanayoendelea kufanywa na vyombo vya dola na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wahusika. 

Tayari watu wanne nchini Kenya wamefikishwa ICC wakikabiliwa na mashtaka ya kuhusika na vurugu zilizosababisha vifo vya mamia ya watu katika uchaguzi mkuu uliopita nchini humo.
 E & P
Dondoo

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Septemba 28 mwaka jana kilipelekwa malalamiko Maalum ICC kuhusu mauaji ya watu 24.

Serikali inalalamikiwa kushindwa kuzuia na kuwachukulia hatua wanaohusika na mauaji ya watu 24 waliuawa katika wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou Bensoud pamoja mengine kuulizia

source: mwananchi gazeti
 
ongoza.jpg

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda alipofika Ikulu jijini Dar es Salaam

Mwananchi
 
"Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja Tanzania," alisema Werema.

Malaika Israeli mtoa roho kaja kumsalimia binadamu... alafu binadamu huyo anajisifu kupata 'mgeni mwema'...
Subirini akirudi kwao akadiscuss na vimalaika vyake, then kaz mtaisikia...
 
kwani mzee wa kaya hajafunguka tu kuhusu ugeni huo?
 
"Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja Tanzania," alisema Werema.
 
Hii mahakama ya sijui ICC ama ICTR ni kupoteza muda na pesa za walipa kodi tu. Hakuna jipya hapo Arusha zaidi ya kuchezea pesa za watu na muda
 
Anavyopenda picha....., ngoja wamnyoroshe.., anadhani ni Naomi Campbell huyo.
 
Mwelekeo murua wa kuhimizwa kwa vitendo kuzingatiwa kwa UTAWALA WA SHERIA badala ya UTAWALA WA MTU uko njiani kutufika nchini Tanzania.
 
Wabongo bana,
Haendi mtu yeyote Netherlands!
Kwenye scale ya Gross human right abuse Africa achalia mbali duniani, Tanzania bado ni maraika na kikubwa zaidi, nchi na makampuni ya wakubwa wa magharibi yanapata kila kile wakitakacho (exploitative investment).
Kushangilia ni kama kupiga ngoma isiyokuwa na wachezaji
 
Ajiandae kumpokea #; na timu yake 2016 the Hague!
 
Last edited by a moderator:
Ziara ya 'kujitambulisha kwa JK' inakuja siku chache baada ya ziara CJ Mutanga na Kibaki nchini na siku moja kabla uchaguzi Kenya. Pia ikumbukwe Uhuru na Raila wamezuru nchi siku za karibuni.
 
“Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja Tanzania,” alisema Werema.

source: mwananchi gazeti

Eeh, huyu jamaa sidhani kama kasomea sheria kweli, maana hata kutoa argument hajui-Kwa hiyo moja kati ya majukumu yake ni kutembelea nchi na kusalimia mara tu baada ya kuteuliwa!?
 
Wawe wanatoa taarifa bhana,hiz ziara za ghafla mtajamuua jk wetu na pressure bure
 
Nikiteuliwa kuwa boss kazini nitakwenda kumtembelea rais,kama icc ilivyo fanya.
 
Back
Top Bottom